Watahiniwa 566,840 kufanya Mtihani kidato cha 4 Nov 14

Watahiniwa 566,840 kufanya Mtihani kidato cha 4 Nov 14

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), limesema jumla ya watahiniwa 566, 840 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne, utakaoanza kesho Jumatatu Novemba 14 2022 katika shule za Tanzania Bara na Zanzibar.

Limesema kati yao watahiniwa 533,001 ni shule na 31, 839 wa kujitegemea .Kati ya hao watahiniwa wavulana ni 247,131 sawa na asilimia 46.19 na wasichana 287,870 sawa na asilimia 53.81.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athuman Amasi, ameeleza hayo leo Jumapili Novemba 12, 2022 wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maandalizi ya mtihani huo, akisema kila kitu kinakwenda vizuri ikiwemo mitihani kufika kwenye mikoa na vituo husika.

Amasi amesema katika idadi hiyo wapo watahiniwa wenye mahitaji maalumu 852 kati ya 480 wana uhoni hafifu, 62 wasioona, 19 wenye ulemavu wa kusikia, 152 wenye mtindio wa akili na 139 wana ulemavu wa viungo.

"Mwaka 2021 idadi ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 538,024 hivyo kuja ongezeko la jumla ya watahiniwa 28,816 sawa na asilimia 5.36 kwa mwaka 2022 ukilinganisha na mwaka 2021.

"Maandalizi ya mtihani huu wa kesho yamekamilika ikiwa ni pamoja kusambazwa kwa mtihani, vijitabu vya kujibia na nyaraka zote muhimu zinazohusu mtihani katika mikoa ya Tanzania na Zanzibar," amesema Amasi.

Amasi amesema mtihani wa kidato cha nne ni muhimu kwa wanafunzi na jamii kwa sababu ina pima umahiri wa wanafunzi katika masomo yote aliyojifunza kwa muda wa miaka minne.Pia amesema matokeo ya mtihani huo yanatumika katika chaguzi za wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu ya sekondari na fani mbalimbali

Chanzo: Mwananchi
Nawatakia kila laheri
 
Hivi hakuna muda limit wa kukaimu nafasi fulani? Mbona huyu mzee anakaimu hii nafasi muda mrefu sana?
 
Kuna demu atafanya hiyo mitihani nilikuwa Nampa kila atakacho ila akaniacha.

KMMK sasa namuombea auone moto kwenye mtihani wa kwanza tuu, aone maruweruwe, Maths ajibu kama Geography, English ajibu kama Biology, wenzake wakitumia penseli kuchorea yeye atumie bic, karatasi ya kujibia aandike mashairi ya ule wimbo wa kuachwa kutoka kwa Marioo

Yani yule mataco natamani hata avunjike mguu akiwa anaelekea kufanya hiyo mitihani.
Muombee mema tu ndugu yangu.Kipochi chake si ulikienjoy wakati ule? Nipm namba yake kwanza.
 
Muombee mema tu ndugu yangu.Kipochi chake si ulikienjoy wakati ule? Nipm namba yake kwanza.
Kipochi chenyewe nimekigusa mara moja tuu, ngoja amalize mitihani then nimchek kumtakia heri japokuwa ameniacha
 
Bora wahitimu tupate namba D

Kuna shule sio inaitwa Temeke secondary school sitegemei kukosa zero 100+ naongea kwa uhakika zero zikiwa chini ya hapo nipewe life ban JF
Kuna kamoja kanaitwa Irene nishakaseti tayari nasubiria kamalize tu.
 
Bora wahitimu tupate namba D

Kuna shule sio inaitwa Temeke secondary school sitegemei kukosa zero 100+ naongea kwa uhakika zero zikiwa chini ya hapo nipewe life ban JF
Vip madogo wanadaga sanaa
 
Wale mnaotarajia kuoa namba E mkutane hapa .
 
Back
Top Bottom