Watahiniwa 63,583 wa Kidato cha 4 wamefeli kwa kupata Division 0

Watahiniwa 63,583 wa Kidato cha 4 wamefeli kwa kupata Division 0

Tunako kwenda hata akifaulu mwanafunzi mmoja wao itakuwa safiii tu...
 
Kwa jinsi ilivyo serikali kutojali hao wanafunzi inaoona wamefeli wataachwa wakafilie mbali bila kuwaandalia mpango endelevu wa kuendeleza maarifa waliyoyapa kwa miaka yote minne. Serikali huwa haijiulizi hao maelfu ya hao wanafunzi huwa wanaenda wapi baada ya kufeli? Ina deal na wachache inaoona ndio wamefauli huku ikiacha nguvu kazi ipotelee kusikojulikana. Wale wanafunzi wanaofeli bado ni lulu kwa taifa wasibezwe na kudharauliwa
Kwa hiyo Unataka Serikali ifanyeje?,si Kuna VETA jamani?.
 
Jumla ya Wanafunzi waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha 4 mwaka 2022 walikuwa 534,753 lakini waliofanya Mtihani huo ni 522,217 ambapo Wasichana walikuwa 280,251 na Wavulana 241,966. Tafsiri ya haraka ni kuwa zaidi ya wanafunzi 12,000 hawakufanya Mtihani wa kumaliza Kidato cha 4.

Kiwango cha ufaulu katika Matokeo hayo kilikuwa kama ifuatavyo. Waliopata Daraja la I, II na III ni 192,348 wakati waliopata Daraja la IV ni 264,627 na Waliofeli kwa Daraja 0 ni 63,583.

Chanzo: NECTA
Serikali haina mfumo rasmi namna ya kuwa okoa hiki kizazi cha div iv na zero coz ingekua mofumo rasmi hii nchi tungekuwa mbali sanaaa
 
Siyo vizuri kuwa-grade wanafunzi.

Kwamba; hawa wamepata division one na hawa zero wakati mazingira ya kujifunza, uwezo wao darasani, n.k. ni tofauti.

Huko ni kuwafanyia marketing wanaopata division one waonekane ni bora zaidi ya waliopata sifuri.

Matokeo yake wengine wanakariri tu ili wapate division one badala ya kujifunza waelimike.

NECTA waachane na huu mfumo.
Ulitaka wafanyeje?

Hakuna sehemu duniani mitihani haifanyiki, hakuna sehemu duniani grading haipo
 
Elimu yetu ya Tanzania inazidi kushuka kiwango siku hadi siku imagine waliopata div 0 na div 4 ukiwaunganisha ni zaidi ya asilimia 50 ya watahiniwa wote.
 
Serikali haina mfumo rasmi namna ya kuwa okoa hiki kizazi cha div iv na zero coz ingekua mofumo rasmi hii nchi tungekuwa mbali sanaaa
serikali imekuwa ikipoteza nguvu kazi kwa huu mfumo mkongwe wa elimu inaoukumbatia licha ya kupitwa na wakati
 
Back
Top Bottom