Watakatifu ni wazungu waliokufa zamani. Waafrika waliokufa zamani eti ni mizimu

Ni upumbavu wa hali ya juu wazee wetu waliotangulia mbele ya haki kuitwa mizimu halafu wale wazungu kuitwa watakatifu, nakereka sana.

Utasikia mtakatifu Yohana utuombee. Halafu sisi tukiwaambia wazee wetu watuombee mnasema tunaabudu mizimu.

Halafu sipendi kabisa mnavyosema sisi ni wapagani. Sisi sio wapagani, ndio maana tunatambua uwepo wa Mungu Mkuu tuliye mwita kwa majina mbalimbali mfano Mulungu, Nguluvi nk.

Tunaomba mheshimu imani yetu. Makafiri na mapagani ni nyie mnaoabudu dini za magabachori
😍😍😍😍😍😍😍😍😍😍
 
"Huwezi amini siku hiyo tulichukua kondoo mkubwa tukaenda kwenye mti mmoja mkubwa pale kijijini,tukawalilia wazee kuomba mvua..huwezi amini katika lile kundi kuna watu walikuja na miamvuli kabisa,na kweli wakati wa kurudi hata kijijini hatukifika mvua ikanya..."
Wale wazee wa zamani walikua watakatifu, nendeni wakati huu mkaombe muone kama mtapata mvua
 
Ni upumbavu wa hali ya juu wazee wetu waliotangulia mbele ya haki kuitwa mizimu halafu wale wazungu kuitwa watakatifu, nakereka sana.

Utasikia mtakatifu Yohana utuombee. Halafu sisi tukiwaambia wazee wetu watuombee mnasema tunaabudu mizimu.

Halafu sipendi kabisa mnavyosema sisi ni wapagani. Sisi sio wapagani, ndio maana tunatambua uwepo wa Mungu Mkuu tuliye mwita kwa majina mbalimbali mfano Mulungu, Nguluvi nk.

Tunaomba mheshimu imani yetu. Makafiri na mapagani ni nyie mnaoabudu dini za magabachori
Tatizo ni sisi wenyewe tunaita mizimu ya mababu zetu sasa watasemaje😃 halafu nao mizimu wawe wanaongea kostaarabu basi sio kuja kwa kutishana namna hii😃😃😃😃
 
Ni upumbavu wa hali ya juu wazee wetu waliotangulia mbele ya haki kuitwa mizimu halafu wale wazungu kuitwa watakatifu, nakereka sana.

Utasikia mtakatifu Yohana utuombee. Halafu sisi tukiwaambia wazee wetu watuombee mnasema tunaabudu mizimu.

Halafu sipendi kabisa mnavyosema sisi ni wapagani. Sisi sio wapagani, ndio maana tunatambua uwepo wa Mungu Mkuu tuliye mwita kwa majina mbalimbali mfano Mulungu, Nguluvi nk.

Tunaomba mheshimu imani yetu. Makafiri na mapagani ni nyie mnaoabudu dini za magabachori
Kabla ya kuandika ulitakiwa ujue chimbuko la dini, zilianzia wapi, kwa taarifa yako hakuna dini iliyoanzia ulaya, japo kwenye siasa zako ipo, ukristo na uisilamu ulianzia sehemu moja na Muhamad na Yesu walizaliwa na kuishi uarabuni, ni waatabu.

Majina yanayotumika kwenye dini hizi ni aina moja tofauti ni uandishi na utamkwaji kulingana na lugha za watu, Yohana ni kiswahili na John ni kiingereza, ukienda ujerumani au uhispania hautatakuja yakiandikwa au kutamkwa hivyo.

Nifafanulie uhusika wa mwingereza kwenye ukristo uliyemtolea mfano ni upi.
 
Kabla ya kuandika ulitakiwa ujue chimbuko la dini, zilianzia wapi, kwa taarifa yako hakuna dini iliyoanzia ulaya, japo kwenye siasa zako ipo, ukristo na uisilamu ulianzia sehemu moja na Muhamad na Yesu walizaliwa na kuishi uarabuni, ni waatabu. Majina yanayotumika kwenye dini hizi ni aina moja tofauti ni uandishi na utamkwaji kulingana na lugha za watu, Yohana ni kiswahili na John ni kiingereza, ukienda ujerumani au uhispania hautatakuja yakiandikwa au kutamkwa hivyo.

Ukristo wa asili ulijifia zamani kwa sasa umebaki utapeli wa warumi tu na watoto wake vi dhehebu vingine
 
Muingereza kaleta u Anglican. Pia King James Bible version.
Mbaya zaidi kitabu cha Yakobo wanakiita James ili kumuenzi mfalme wao
 
Ukristo wa asili ulijifia zamani kwa sasa umebaki utapeli wa warumi tu na watoto wake vi dhehebu vingine
Gwajima is watching you.

1638252507671.png
 
Ukiwatumikia wao na miungu yao ya uongo unakuwa mtakatifu
 
Wapo Watakatifu Waafrika wengi pia wakiwemo mashahidi wafia dini wa Uganda kina Kalori Lwanga na wenzake.Shida kwa Africa Ni upatikanaji wa taarifa sahihi kwa wakati.

Hata JPM kwa kauli zake na msimamo wake juu hatua za kukabili uviko 19 na kujitoa kwake, aliokoa maisha ya wengi kwa Imani thabiti kwa Mungu.

Kigezo hicho Pekee mbali ya madhaifu yake mengine anaweza kutangazwa Mtakatifu.
Mnalazimisha Shetani kuwa Malaika? Magufuli awe matakatifu muuaji yule!!
 
Utakuwa huna taarifa sahihi! Afrika Kaskazini kuna watakatifu wengi tu. Mt. Augustino hakuwa Mzungu!
 
Ni upumbavu wa hali ya juu wazee wetu waliotangulia mbele ya haki kuitwa mizimu halafu wale wazungu kuitwa watakatifu, nakereka sana.

Utasikia mtakatifu Yohana utuombee. Halafu sisi tukiwaambia wazee wetu watuombee mnasema tunaabudu mizimu.

Halafu sipendi kabisa mnavyosema sisi ni wapagani. Sisi sio wapagani, ndio maana tunatambua uwepo wa Mungu Mkuu tuliye mwita kwa majina mbalimbali mfano Mulungu, Nguluvi nk.

Tunaomba mheshimu imani yetu. Makafiri na mapagani ni nyie mnaoabudu dini za magabachori
Kuna Mtakatifu Kizito, Mtakatifu Lwanga nk. Hao ni wazungu?
 
hivi ni wakina nani wanao gawa huo utatifu jamani....???
Huwa ni hatua na mchakato mrefu saana. Huchukua karne na zaidi kutangazwa kuwa Saint. Ukiachilia mbali akina Mtakatifu Theresa wa calcuta, Mtakatifu Papa Paul VI ( sina uhakika). Ambao mchakato wao ulichukua muda mfupi ni chini ya miaka 40. Wametangazwa kuwa Watakatifu tayari.
 
Watu wanajitungia njia nyingi sana za kujifariji faraja hewa.
 
Mambo ni mengi.
Mzungu akija huku hata hana mia ataitwa mtalii au mwekezaji.
Kesheshe ni mtu mweusi aende kwao anaitwa muhamiaji haramu
 
Back
Top Bottom