Watakuhukumu Kutokana Na Mitazamo Ya Misingi Ya Imani Zao

Watakuhukumu Kutokana Na Mitazamo Ya Misingi Ya Imani Zao

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,237
Reaction score
1,744
Matendo 28
3 Paulo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni, na kuuweka motoni, nyoka akatoka kwa ajili ya ule moto akamzongazonga mkononi.
4 Wenyeji walipomwona yule nyoka akilewalewa mkononi, wakaambiana, Hakosi mtu huyu ni mwuaji; ambaye ijapokuwa ameokoka katika bahari haki haimwachi kuishi.
5 Lakini yeye akamtukusia motoni asipate madhara.
6 Wao wakadhani ya kuwa atavimba au kuanguka chini kwa kufa ghafla; na wakiisha kumwangalia sana, na kuona kwamba halimpati dhara lolote, wakageuka, wakasema kwamba yeye ni mungu.

Zipo kauli hututisha sana tunaposikia watu wakisema maneno magumu juu yetu, kuna watu hawapo tayari kutusaidia ila wanatushangaa na kutuona tunaenda kufa kwa kile kitu kimetupata katika maisha yetu.

Kuna maeneo tunaweza kuyapitia katika maisha yetu, watu wakaona tunapitia hayo kwa sababu tumemkosea Mungu, na wengine wanaona hatutaweza kuvuka juu ya mambo magumu yanayotukabili wakati huo kutokana na utumishi wetu.

Paulo anakutana na changamoto ya kupandiwa na nyoka katika mkono wake, watu badala ya kumsaidia, wao wakawa wanawaza mambo yao, wakawa wanasemezana wao kwa wao mambo ambayo si ya kweli, wakiamini hawezi kuachwa salama na nyoka.

Nyoka huyo wanamjua ana sumu kali, akikung'ata huwezi kupona, akili zao wanajua ni adhabu ya mungu wao, mitazamo ambayo kila mmoja anaweza akawa nayo mahali popote pale anapokuwepo.

Tunaweza tukawa na mitazamo sahihi juu ya imani zetu, na tunaweza tukawa na mitazamo potofu juu ya imani zetu, kinachotufanya tuwe na mitazamo hii ni mafundisho tuliyonayo katika maisha yetu, au msingi uliojenga imani zetu.

Mitazamo yetu inajengwa na kile tunachojilisha kila siku, ikiwa mtu anatumia muda mwingi kujifunza juu ya miungu, imani yake itajengeka katika imani ya miungu, na ikiwa mtu anajikita zaidi kujifunza neno la Mungu, imani yake itajengeka katika msingi sahihi juu ya Mungu.

Japokuwa wapo watu wanatumia biblia hii hii unayotumia wewe, ila wanapotosha au wamepotoshwa, wanachokiamini ni kama kipo ndani ya neno ila kinapingana na neno la Mungu.

Tunapaswa kujenga imani yetu katika chanzo sahihi ili tuwe na mtazamo sahihi juu ya Mungu na watumishi wake, tukiwa na mitazamo isiyo sahihi wale walio sahihi tutakuwa tunawaona kwa namna isiyo sahihi. Sio kana kwamba hao tunaowaona hawapo sahihi ni kweli, inawezekana pasiwepo na ukweli wowote kutokana na mitazamo iliyojengwa na fundisho potofu.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma neno na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Ukiona nyuzi nyingi humu JF kuhusu dini na iman bas ujue kuna jambo linaendelea uko mtaani.

Naomba kujuzwa nini kinaendelea maana hizi nyuzi za dini na iman zimekua nying sana

Mi nilishaacha kufuatilia habari za Tanzania muda mrefu sana saiv najua habari za Usa kuliko ata za hapa kwetu
 
Back
Top Bottom