Watalii kutokuja tena Tanzania?

Watalii kutokuja tena Tanzania?

Fundi,

Unajichanganya vibaya sana. Unawa hukumu hao waarabu kuwa wanawinda "kirambo" Sasa kutembea na bastola ishakuwa uharamia!. Wangapi Tanzana wanatembea na bastola as long as taratibu za kumiliki silaha zimefuatwa tatizo lipo wapi?

Kama ni mavazi ndio uwindaji wa kirambo unataka kuwapangia hata cha kuvaa?

Tatizo lako wewe ni mdini SANA na michango yako humu inathibitisha hivyo. Ndio maana unauliza eti Eddie na uislamu wapi na wapi, nani kakwambia kama mimi muislamu? Kwanini ukejeli jina na kuli nasibisha na dini.

Tuambie sheria gani imevunjwa kwa hao jamaa kubeba bastola? Sheria gani imevunjwa kwa hao jamaa kuwinda kirambo rambo? yaani kubeba silaha nzito kama riffle iwe sawa kosa liwe kubeba bastola!

Acha kuzungusha sema kinacho kukera.

Wangapi Tanzania wanatembea na bastola kiunoni na rifle mkononi hata kama wanazimiliki kisheria?

Hapa hatuzungumzii sheria bali morals na ethics za hawa wanaojifanya wawindaji. Hata kama wamemilikishwa sehemu kisheria lakini haituzuii sisi kukemea matendo ambayo tunaona ni ya ovyo. Au unadhani hao wakina Barrick wanaopigiwa kelele kila siku hawana haki ya kisheria kufanya wafanyayo? Sheria zetu ni dhaifu na kila mtu anatakiwa kujua hivyo.

Kinachonikera ni nyie kuingiza udini hata pasipo haja. Sasa unakana dini yako wakati unamshangaa muislamu mwenzio kwa kuikemea tabia mbovu bila kujali rangi au dini ya watu wanaohusika.

Tofauti na wewe, mimi sijawahi kukataa kuwa ni mmisheni. Pamoja na hivyo sijasita kuwakemea wenye dini kama yangu. Wewe, usie mdini, lini mara ya mwisho umemkemea muislamu mwenzio? Au waislamu hawafanyi maovu? Waovu ni wakina Benjamin na Edward peke yao?

Acheni upuuzi wenu wa kuingiza dini kila mahali. Mtatufikisha pabaya.

Amandla.......Eddie usiye muislamu!
 
BTW, uwindaji wa ki-rambo si mavazi peke yake. Pamoja na hiyo bastola ni kuning'inia nje kwenye gari ambalo inaelekea kwenda kasi!

Amandla....
 
He is the crown prince of Dubai on a paid hunting holiday in Tanzania, whats the big deal?He doesnt own loliondo. How many people carry hand guns in TZ?Some tanzanians have used in to shoot their fellow Tanzanians. Whatever you say here, arabs have the money and bongo needs it. Stop crying like babies and show some repect to the ones who feed your A**es.
 
Omar,
Stop crying like babies and show some repect to the ones who feed your A**es.
Wow!... kumbe mwenzetu shoga!.. duh ndio maana....samahani mkuu ni haki yako ya kimsingi kuulilia- haaa haaa haaa!
 
Wangapi Tanzania wanatembea na bastola kiunoni na rifle mkononi hata kama wanazimiliki kisheria?

Hapa hatuzungumzii sheria bali morals na ethics za hawa wanaojifanya wawindaji. Hata kama wamemilikishwa sehemu kisheria lakini haituzuii sisi kukemea matendo ambayo tunaona ni ya ovyo. Au unadhani hao wakina Barrick wanaopigiwa kelele kila siku hawana haki ya kisheria kufanya wafanyayo? Sheria zetu ni dhaifu na kila mtu anatakiwa kujua hivyo.

Kinachonikera ni nyie kuingiza udini hata pasipo haja. Sasa unakana dini yako wakati unamshangaa muislamu mwenzio kwa kuikemea tabia mbovu bila kujali rangi au dini ya watu wanaohusika.

Tofauti na wewe, mimi sijawahi kukataa kuwa ni mmisheni. Pamoja na hivyo sijasita kuwakemea wenye dini kama yangu. Wewe, usie mdini, lini mara ya mwisho umemkemea muislamu mwenzio? Au waislamu hawafanyi maovu? Waovu ni wakina Benjamin na Edward peke yao?

Acheni upuuzi wenu wa kuingiza dini kila mahali. Mtatufikisha pabaya.

Amandla.......Eddie usiye muislamu!

Kweli ukipenda pengo huita mwanya.... yaani hiyo bastola iliyokaa kwenye ala yake ndio imepelekea wewe kusema inatisha as if imekuwa pointed kwa mtu! Nani asiejua kama hali ya usalama ipo tete si tu katika mbuga (mwituni huko kwenye majangiri nk ) bali hata mijini. Binafsi nimesafiri mara kadhaa kwenye msafara ambao miongoni mwetu walikuwa na bastola kwa ajiri ya usalama wetu.

Eti tusizungumzie sheria. je unataka tufuate nini kama si sheria. Kama sheria zetu mbovu sasa kosa la nani mwarabu?

Halafu unaleta habari za moral and ethics zipi hizo? unakereka kwa mtu kuvaa kanzu tu unaita kirambo rambo hao "watalii" vichupi wanao randa kila siku mitaani wana morals gani?

Unae ingiza udini ni wewe unaedai ninam shangaa muislamu "mwenzangu" sijui ulijuaje kama mimi muislamu na huyu pia ni muislamu mwenzangu. Inahitaji kuwa mdini kumjua mdini! Unang'ang'ania nikuonyeshe lini nilikemea muislamu mwenzangu nani kakuambia mimi muislamu?

Wangefanya waarabu haya pasinge tosha hapa

Rhino.jpg

Hivi sisi ni stupid?
Ukweli ni kwamba mimi binafsi napenda wild animal statistic za haraka zinaonyesha mikumi nimeenda mara 2, Serous mara moja, ngorongoro 2 serengeti 3 times.
hivyo ninapenda sana wanyama sasa basi mimi kusema hiyo yote ni kwamba nimesikitishwa saana na ualibifu wa mazinga sasa kama ukiangalia barabara zinajengwa majani yanatolewa alafu hao watu wanapiga malisasi yao ambapo yanasababisha wanyama kukosa amani horn tu ya gari haitakiwa lkn hao jamaa wanakaa humo polini ili wazungu watoke marekani kuja kuwaona.

Hivi kweli mtu na akili yako mmarekani anawezakuja na roho nyeupe akazunguka mbugani huku waraabu wakiwa na mabunduki yao humo,
sana sana wanaweza kuambiana kuwa huko sio sehemu salama kutokana na warabu wenye siraha walioko humo maana hao watu huwa wanao uwezo wakufanya kituchochote kile hivyo tunajifukuzia wazungu wanao tuletea dola bila madhara maana zao huwa ni picha hawajengi wala kuua wanyama.
Kingine hii picha inaonyesha fika kuwa hao wazungu wanamtibu huyo faru maana faru wote Tanzania wanalindwa na ulinzi mkali.
Sema hauna picha mimi ntaweka picha zingine za wazungu wakiwinda na kuua wanyama wetu nntaziweka muda sio mrefu.
 
He is the crown prince of Dubai on a paid hunting holiday in Tanzania, whats the big deal?He doesnt own loliondo. How many people carry hand guns in TZ?Some tanzanians have used in to shoot their fellow Tanzanians. Whatever you say here, arabs have the money and bongo needs it. Stop crying like babies and show some repect to the ones who feed your A**es.

Aaaah jamani kweli leo hii warabu watulishe sisi, wakati huko kwao wanachapwa na mmalekani kisha wanapewa viloba vya maindi vilivyo andikwa USA tena wanavipokea kwa mikono miwili,

Watarii ni wazungu bwana.
 
Wangefanya waarabu haya pasinge tosha hapa

Rhino.jpg

Hii ni mbuga gani Tanzania wanawinda faru na twiga?

Sheria ya Uwindaji inatamka kuwa mgeni lazima aambatane na "Professional Hunter - PH" pamoja na Askari Wanyamapori (Game Scouts) wanapokwenda kuwinda. Kwenye picha ya wale waarabu, je lile kundi linajumuisha PH na Game Scouts? Siku hizi tuna Game Scouts kutoka Saudi Arabia?
 
Mzungu wa Grumeti ameishasemwa sana.Hususan kutokana na kitendo chake cha kuwazuia wa-Hadzabe kuwinda katika eneo alilomilikishwa. Lakini hata siku moja hajawahi kushtakiwa kwa uwindaji wa ki-Rambo usiongalia sustainability ya eneo lake.

Tunajitahidi kuangalia pande zote na kutomuonea haya yeyote bila kujali rangi, dini au nguo alizovaa! Tunapokosea tusahihisheni kwa kutoa mifano inayoendana na hoja. Kama kuna mahali mwingine anafanya uwindaji wa aina hii, mwanikeni hapa bila kujali dini, jinsia, rangi yake nae tutamchambua.

Amandla........

Kuna wa-Hadzabe kule Ikoma/Makundusi - Serengeti? Never mind! Mwekezaji Grumeti Reserve Ltd. anayemiliki hoteli za Singita-Sasakwa Lodge na Farufaru ni tofauti kabisa na hawa waarabu. Mwekezaji wa Grumeti ni conservationist by all standards. Amekodishwa vitalu viwili au vitatu vya uwindaji lakini hawindi na analipa ada yote (100%). Ametoa ajira kwa watanzania wenzetu. Analipa kodi kutokana na biashara ya hoteli. Anafadhili miradi mbalimbali ya uhifadhi ikiwemo mafunzo kwa maafisa wanyamapori na reintroduction of rhino into Serengeti ecosystem (which is very expensive). Last time I checked, kampuni hii ilitangaza kuanzisha mpango wa kutoa scholarship kwa vijana 6 wa kitanzania in " prestigious American universities" kila mwaka. I don't know the progress on this commitment.

To the contrary, waarabu si wahifadhi. Conservation is not in their DNA. Ndani ya Pori la Selous, kuna kitalu kinaitwa Madaba. Kitalu hiki kimekodishwa kwa Kampuni la Usangu Safaris/TAWICO. Hawa jamaa ni waarabu wako Arusha pale. Wamefanya uharibifu sana na mara nyingi wamekwaruzana na maafisa wanyamapori on the ground. Hawa maafisa huishia kushindwa kwa sababu wakubwa wao unakuta walishapokea bahasha. Waarabu ni waharibifu tu wa bioanuai. They neither adhere to hunting regulations nor stick to the hunting quota. Hawa wa Loliondo watakuwa waharibifu zaidi kwa sababu hatuna watu wetu pale kuangalia ni nini kinafanyika. I have no reason not to believe that they are overexploiting wildlife resources in that particular habitat patch. Uwindaji na uhifadhi si uisilamu na ukristo. Ni sayansi!
 
Hii picha ni ya south Africa

Ninakubali. Huyo faru anaonekana bado yuko hai [angalia miguu ya mbele]. Na South Africa, watu wanafuga hawa kama ng'ombe. So, uwindaji unafanyika kwenye ranch za watu binafsi. So, property right is well defined. Huwezi kuingia kwenye ranchi na kuanza kuwinda mnyama ambaye hujaruhusiwa kuwinda kwa kuwa mmiliki wa ranchi analinda mali yake ipasavyo. Kwa mmiliki wa ranchi, kumpoteza faru mmoja ni sawa na kupoteza ng'ombe wako wa maziwa anayekuingizia kipato. Hapa kwetu uwindaji unafanyika mbugani. And wildlife is a state property. It is owned by nobody so to speak. Matokeo yake tunayaona: overexploitation!
 
Hii hali ilivyo sasa mbugani waarabu kuweka makazi yao namna hii , Kweli Mmarekani ataweza kuja mbugani na hali ikiwa hivi jamani hii mbona kubwa kuliko ni kwanini tujipotezee mapesa ya wazungu wakati wazungu toka enzi na enzi ndio ambao wamekuwa wakitusaidia,
sisi hata kama hatwendi mbugani kuangalia maliasili zetu ni uwezo tu ila tunazipenda sana tena sana ningependa

Huyu Mmarekani unayedai kuwa ataogopa kuja si ndiyo huyo Mmarekani anaye controll nchi zote za kiarabu na ni swahiba wa dhati wa hawa Waarabu?.

Nasshindwa kuelewa unapodai wazungu wanatusaidia...kwa taarifa yako hakuna mzungu anayetusaidia bali ni wanarudisha walichochota.

Mbuga ziheshimiwe waachwe wanyama pekeyao wasiletewe usumbufu.
Lakini kwanini nyinyi tu jamani mbona Kenya haya mambo hayapo? are we stupid? %%%%#####**** griiiiiiiiiiiiiii

Sasa unatakaje?Waarabu,Wamarekani wasije? Na unaposema haya mambo Kenya hayapo...je ni unahakika?
 
Nilivyosema:

Inatisha.

Amandla.......

Ulivyosema:

Fundi mdini unatishwa na nini?
Aliyeingiza neno dini nani katika mjadala huu kama si wewe?

Akasema Mkandara ambaye hata siku moja hajaficha imani yake:

Duh, Hizi picha inabidi tujiulize mara kumi kumi...Yaani hakuna mtu wetu kuangalia kinachofanyika...bastola ya nini ktk uwindaji jamani...something isn't right!
Ulivyomjibu kuonyesha kuwa Mkandara anasaliti imani yake.

Udini tu hamna lolote!

Of all people hata wewe Mkandara?
Ulivyokazia kuwa mimi ni mdini ati kwa sababu nimesema hiyo hali inatisha!

Tatizo lako wewe ni mdini SANA na michango yako humu inathibitisha hivyo. Ndio maana unauliza eti Eddie na uislamu wapi na wapi, nani kakwambia kama mimi muislamu? Kwanini ukejeli jina na kuli nasibisha na dini.

Unae ingiza udini ni wewe unaedai ninam shangaa muislamu "mwenzangu" sijui ulijuaje kama mimi muislamu na huyu pia ni muislamu mwenzangu. Inahitaji kuwa mdini kumjua mdini! Unang'ang'ania nikuonyeshe lini nilikemea muislamu mwenzangu nani kakuambia mimi muislamu?

Eddie ni kifupi cha majina ya wamisheni (Edward, Edmund, n.k.). Kwa hiyo wewe ni m-misheni?

Hii si mara ya kwanza wewe kuchangia kama ilivyo kwangu. Katika uchangiaji bias ya mtu inaonekana. Wewe yako dhahiri anapoguswa muislamu au yule unayekisia ni muislamu, unapandisha. Sasa kama si muislamu basi ni muislamu wannabe. Lakini hata hiyo siiamini maana ungekuwa m-misheni, rastafarian, buddhist, m-hindu, atheist, m-bahai, ungekana na kutaja dini yako. Lakini kwa sababu unaogopa kukufuru kwa kuikana dini yako unabakia kuuliza rhetorical questions kama "nani ka kwambia mimi ni muislamu".

Ukweli ni kuwa uwe muislamu au usiwe, it makes no difference to me. Views zako ni bigoted. Kama nia yako ni kutetea waislamu, umechagua the wrong issue. Mkandara yuko right. Hawa jamaa wawe wazungu, waarabu au whatever wanachofanya ni immoral na inabidi kilaaniwe.

Nilikuwepo.

Amandla......
 
warababu warabu warabu, siku zote mswahili atalalamika kuhusu mwarabu lakini mzungu kila anacho fanya ni sawa. hawa wazungu walitawala TZ na nini maendeleo mliopata? mliachwa na umasikini wenu na dreams za kwenda majuu kubeba maboksi. Waliwalimisha wakati wa ukoloni sasa wana wabebesha maboksi.
Stop the slave mentality of thinking mzungu is superior and better than everyone else.
 
Hakika umesema maana utalii unachangia kipato cha taifa letu,
japokuwa ni kivutio ila ni kitu tunacho jivunia sana, Hao wakisha tualibia hatuta waona tena hapa kwetu watatucheka na kutudharau.
 
warababu warabu warabu, siku zote mswahili atalalamika kuhusu mwarabu lakini mzungu kila anacho fanya ni sawa. hawa wazungu walitawala TZ na nini maendeleo mliopata? mliachwa na umasikini wenu na dreams za kwenda majuu kubeba maboksi. Waliwalimisha wakati wa ukoloni sasa wana wabebesha maboksi.
Stop the slave mentality of thinking mzungu is superior and better than everyone else.

Ommy acha hizo wewe,
Mzungu yupo juu vitu vyake tunaviona sema kinachoponza wenzetu wachache ni Uroho maana hata kwenye madini watu tungekuwa tunafaidi ila uroho ndio unasababisha mambo yawe magumu.

Haya angalia nchi zilizo tawaliwa na wazungu mfano south, hata kenya ilitawaliwa kidogo kwani sisi tunawafikia wakenya kimaendeleo?
eeeh haya jaribu kuangalia mikoa ambayo hapa Tanzania warabu achilia mbali kukaa , kupita tu! mfano Tabora, Tanga n.k eeeh nadahani jibu unalo mfano Tanga ilikuwa inakila kitu ipo pwani ardhi nzuri lakini sasa kuingiza umwinyi watu hawafanyi kazi kabisaa leo hii watu watoka mwanza kwenda kulima Tanga kunani.

Wazee wetu nimekuwa nikiwasikia wakiwasifia wajerumani saana na sio waarabu wakisema wamefundishwa uinjinia na mjerumani wanajivunia.

Wazungu ndio wako mbele kimaendeleo kuliko waarabu na mchango wao ktk dunia ni mkubwa sana
 
warababu warabu warabu, siku zote mswahili atalalamika kuhusu mwarabu lakini mzungu kila anacho fanya ni sawa. hawa wazungu walitawala TZ na nini maendeleo mliopata? mliachwa na umasikini wenu na dreams za kwenda majuu kubeba maboksi. Waliwalimisha wakati wa ukoloni sasa wana wabebesha maboksi.
Stop the slave mentality of thinking mzungu is superior and better than everyone else.

Hao wakina Barrick ni waarabu? Marehemu John Nolan alikuwa muarabu? Huyo George W ni muarabu?

Unadhani slave mentality ni kwa wazungu peke yao? Au mnaamini kuwa utumwa ni biashara iliyofanywa na wazungu peke yao? Acheni hizo.

Amandla......
 
Nilivyosema:

Ulivyosema:

Aliyeingiza neno dini nani katika mjadala huu kama si wewe?

Akasema Mkandara ambaye hata siku moja hajaficha imani yake:

Ulivyomjibu kuonyesha kuwa Mkandara anasaliti imani yake.

Ulivyokazia kuwa mimi ni mdini ati kwa sababu nimesema hiyo hali inatisha!

Eddie ni kifupi cha majina ya wamisheni (Edward, Edmund, n.k.). Kwa hiyo wewe ni m-misheni?

Hii si mara ya kwanza wewe kuchangia kama ilivyo kwangu. Katika uchangiaji bias ya mtu inaonekana. Wewe yako dhahiri anapoguswa muislamu au yule unayekisia ni muislamu, unapandisha. Sasa kama si muislamu basi ni muislamu wannabe. Lakini hata hiyo siiamini maana ungekuwa m-misheni, rastafarian, buddhist, m-hindu, atheist, m-bahai, ungekana na kutaja dini yako. Lakini kwa sababu unaogopa kukufuru kwa kuikana dini yako unabakia kuuliza rhetorical questions kama "nani ka kwambia mimi ni muislamu".

Ukweli ni kuwa uwe muislamu au usiwe, it makes no difference to me. Views zako ni bigoted. Kama nia yako ni kutetea waislamu, umechagua the wrong issue. Mkandara yuko right. Hawa jamaa wawe wazungu, waarabu au whatever wanachofanya ni immoral na inabidi kilaaniwe.

Nilikuwepo.

Amandla......

Sasa kama it makes no difference to you kwa nini unang'ang'ania kunivisha uislamu? Ndio maana nikakwambi wewe ni mdini kwa sababu unaposoma post akili yako inakupeleka huko na haupo huru katika michango yako.

Mtu ambaye kanzu tu unaita mavazi ya kirambo rambo, bastola iliyokaa kwenye ala yake ni urambo rambo, umejaa chuki na unaongozwa na jazba.

Sasa unasumbuliwa na jina Eddie unadai la kimisheni, fine Im happy na jina langu kinachokusumbua ni hiyo kasumba na udini wako basi.

Utahangaika sana tu
 
Rambo na kanzu? You are a fool, Eddie of whatever faith. Wewe ndiye uliyeingiza suala la dini mahali ambapo halipo halafu sasa unataka kunitwisha mzigo mie? Ulinihukumu kuwa ni mdini hata kabla sijataja neno Rambo!

Inferiority complex inakusumbua kiasi unakana dini yako mahali ambapo hakuna anayekujua! Jina Eddie ni la ki-misheni, sasa wewe ni m-misheni? Kigugumizi cha nini?

Sijaanza leo kuhangaika na sitaacha.

Amandla.......
 
Back
Top Bottom