Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Fundi,
Unajichanganya vibaya sana. Unawa hukumu hao waarabu kuwa wanawinda "kirambo" Sasa kutembea na bastola ishakuwa uharamia!. Wangapi Tanzana wanatembea na bastola as long as taratibu za kumiliki silaha zimefuatwa tatizo lipo wapi?
Kama ni mavazi ndio uwindaji wa kirambo unataka kuwapangia hata cha kuvaa?
Tatizo lako wewe ni mdini SANA na michango yako humu inathibitisha hivyo. Ndio maana unauliza eti Eddie na uislamu wapi na wapi, nani kakwambia kama mimi muislamu? Kwanini ukejeli jina na kuli nasibisha na dini.
Tuambie sheria gani imevunjwa kwa hao jamaa kubeba bastola? Sheria gani imevunjwa kwa hao jamaa kuwinda kirambo rambo? yaani kubeba silaha nzito kama riffle iwe sawa kosa liwe kubeba bastola!
Acha kuzungusha sema kinacho kukera.
Wangapi Tanzania wanatembea na bastola kiunoni na rifle mkononi hata kama wanazimiliki kisheria?
Hapa hatuzungumzii sheria bali morals na ethics za hawa wanaojifanya wawindaji. Hata kama wamemilikishwa sehemu kisheria lakini haituzuii sisi kukemea matendo ambayo tunaona ni ya ovyo. Au unadhani hao wakina Barrick wanaopigiwa kelele kila siku hawana haki ya kisheria kufanya wafanyayo? Sheria zetu ni dhaifu na kila mtu anatakiwa kujua hivyo.
Kinachonikera ni nyie kuingiza udini hata pasipo haja. Sasa unakana dini yako wakati unamshangaa muislamu mwenzio kwa kuikemea tabia mbovu bila kujali rangi au dini ya watu wanaohusika.
Tofauti na wewe, mimi sijawahi kukataa kuwa ni mmisheni. Pamoja na hivyo sijasita kuwakemea wenye dini kama yangu. Wewe, usie mdini, lini mara ya mwisho umemkemea muislamu mwenzio? Au waislamu hawafanyi maovu? Waovu ni wakina Benjamin na Edward peke yao?
Acheni upuuzi wenu wa kuingiza dini kila mahali. Mtatufikisha pabaya.
Amandla.......Eddie usiye muislamu!