Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Heshima sana wanajamvi.
TRA wametangaza ajira mpya 1,574.
Hili ni jamba zuri sana vijana wetu watapata ajira za uhakika zenye mishahara mizuri na nafasi kubwa ya kutengeneza kipata cha ziada kupitia urefu wa kamba zao.
Kitu wasichakijua WATANGANYIKA katika ajira hizo WAZANZIBAR wametengewa nafasi 331 huku WATANGANYIKA MACHOGO wakitengewa 1243 tu.
Idadi ya watu TANGANYIKA ni zaidi ya 64 Million idadi ya watu ZANZIBAR ni 836,000.
Hizi hesabu nimejaribu kuzipiga,kugawanya,kuzidisha nimetoka kapa.
Huu upuuzi uliletwa na Mchengerwa katika bunge hili linalomaliza muda wake WABUNGE wetu hawakuhoji,hawakudadisi,hawakuuliza waligonga meza kama kawaida yao.
Wakati LISSU akishangaa idadi ya wabunge wa ZANZIBAR kuchanguliwa na wastani wa watu 11,000 tu wakati wabunge wa TANGANYIKA wanachaguliwa na idadi ya watu 300,000 na kuendelea angejiuliza na kudadi inakuwaje WAZANZIBAR wanatengewa nafasi 331 katika taasisi moja tu.Siku BOT wakitangaza ajira utaratibu ni huo huo.
Lissu badala ya kutazama nafasi za kisiasa pekee yake angetazama pia suala zima la ajira katika hii JMT.
Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano
Sheria ya Utumishi wa Umma Na.8 ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003 zimeweka utaratibu wa wazi wa ajira katika Utumishi wa Umma na kuondoa dosari zilizokuwepo. Serikali ya Jamhuri ya Muungano imekuwa ikitoa fursa sawa za ajira kwaWananchi wote wa Tanzania ambao wanaomba na kuwa na vigezo kama Elimu, Uzoefu na Sifa husika. Kuhusu nafasi za watumishi wa kawaida kwenye taasisi za Muungano, utaratibu wa muda wa mgao wa ajira uliokubalika kutumika ni asilimia 79 kwa Tanzania Bara na asilimia 21 kwa Tanzania Zanzibar. Utaratibu huu unatekelezwa kwa mujibu wa Waraka wa Serikali wa tarehe 10 Mei, 2013.