Watanganyika tunapakwa mafuta kutayarishwa kupokea ripoti ya Chande, kila mtu anaisemea mazuri - mshayajua matokeo!

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Wakuu,

Mmeona tunavyoandaliwa kisaikolojia kuipokea ripoti ya tume ya Chande? Chawa washalipwa kuja kuisema mazuri - 'ripoti ya chande itakuja kuliponya taifa' - we ulikuwepooo?

Wameanza na viongozi wa dini, chawa chawa wapuuzi, eti wanamtumia hadi jaji kuja kueleza upuuzi wao! Tutaendelea kuona hii maneno ya kusifia tume hadi siku ya kutoka hakafu tunaangushiwa mzinga!

Nna wasi wasi na hiki kilichofanyika kwa CHADEMA na kuruhusiwa kufanya siasa ni humo humo tu na huenda Lissu afuatie halafu mzigo kama nilivyosema nyuma wanaenda kuangushiwa vyombo vya ulinzi kwamba waliact kwa kufuata oda zao na kwamba Samia alikuwa hajui na ndio maana hata miili ya waliouliwa haijulikani ilipo kwasababu waliofanya mauaji hayo sio "Serikali".

Atawaomba msamaha Watanzania na kutegemea mambo yaishe kama kawaida.

Ila katika hii miaka 5 - 6 nimejua kuna watu wanaakili ndogo hata kuzidi funza serikalini, mtu yuko na fuvu lake na anaona hiki anachokifanya ni bonge moja la plan na itafanikiwa kabisaaa?! Nakojoaaaaa
 
Kilichofanyika ni katika kujisafisha,, so lazima walainishe mazingira maana report ni ngumu
 
Inajulikana maana wanakuja kwa kasi sana
 
So far kwa ule ushahidi waliokua wakitoa wahanga kabla ya tume feki kuzuia waandishi ni dhahiri hakuna namna yakujinasua kwa watawala na wakumbuke watanzania sio wajinga
 
Mm pia.nimeshangaa mno yanajifanya yanaona y mbele.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Ukiwa huna akili ni huna tu hata mipango yako inakua ya kizezeta zezeta 🤣🤣🤣Sifuri bin zero a.k.a tufe....
 
Of course itakuwa ni nzuri ndio, nzuri kwao. Ila sisi watanganyika tunajua hii michongo Mingi Iko kwa ajiri ya kufukia fukia maana wanadhani itawasaidia lakini haitokuja kuwa sawa tena
 
Duuh!!! Kupakwa futa tena ? Mimi simo labda maccm ndiyo wanapakwa futa.
 
So far kwa ule ushahidi waliokua wakitoa wahanga kabla ya tume feki kuzuia waandishi ni dhahiri hakuna namna yakujinasua kwa watawala na wakumbuke watanzania sio wajinga
Hasa ushahidi kuwa watun waliuliwa wakiwa majumbani kwao kama yule Bimkubwa wa Magomeni, na pia kitendo cha watu waliohai kupelekwa mochwari wakafie huko jambo ambalo pia lilimkuta Bimkubwa wa Magomeni, hili ni dole limezama maungoni kabiisa kwa mtawala.
 
Wanajisumbua, wanadhani walioandamana ni chadema kumbe ni vijana ambao wqna uchungu na Tanganyika yao.
Chadema hata wakiungana nao bado waliofiwa na ndugu zao wana uchungu na kilichotokea.
 
Wameanza na viongozi wa dini, chawa chawa wapuuzi, eti wanamtumia hadi jaji kuja kueleza upuuzi wao! Tutaendelea kuona hii maneno ya kusifia tume hadi siku ya kutoka hakafu tunaangushiwa mzinga!
Kwani wanao mpango wa kuitoa na kuitangaza hiyo ripoti itakayotolewa na hiyo tume?

Labda iwe inazungumzia habari za "kukinukisha" na lawama zote kwa wengine kasoro wahusika wa maovu hayo.

Ninachoona hapa ni sherehe ya kukabidhi hiyo ripoti; na vimaneno vichache vitakavyotolewa kusifu kazi nzuri iliyofanyika.

Zaidi ya hapo hakuna la ziada.

Hii tume iliundwa kupoza mambo na kununua muda; na kutafuta wakulaumiwa kuondoa uhusika wa watuhumiwa wenyewe.

Haitakuwa na mchango wowote wa kubadili hali yetu mbovu tuliyo nayo sasa.

Njia sahihi ya kuponya ni kuwajibishwa watenda maovu ambao wameshikilia mamlaka pasipo uhalali.

Hiyo ripoti iwe chachu ya kuwatia nguvu waTanzania kuleta mabadiliko chanya nchini mwetu..
 
Hayo hutayasikia tena mkuu 'PRIEST'.

Hakuna ripoti ya Tume ya aina hii itakayoweza kuyazungumzia machungu ya namna hii.

Walishasema wenyewe; kazi ni "kuponya" kwa njia yoyote ile, hata ya hadaa tu.

Kinachofuata sasa utakuwa ni mchakato wa "MARIDHIANO", FEKI.

Hivi hiyo ripoti itaeleza miili ya waTanzania hawa ilipofukiwa?
Hao watu wa tume wanajuwa? Walipata nafasi ya kupelekwa maeneo ya hiyo miili ilipo?
 
Ukiwa huna akili ni huna tu hata mipango yako inakua ya kizezeta zezeta 🤣🤣🤣Sifuri bin zero a.k.a tufe....
Miaka yote ya huyu mwanamke shetani imekuwa hasara kwa taifa hili. Hakuna 'focus' ya aina yoyote kwa jambo muhimu kuhusu maendeleo ya nchi hii!

Na yote haya ni kama hayatuhusu!
 
Kuna hawa vichaa wanaojiita BAKWATA.

Walaaniwe wao na vizazi vyao kwa kutumia mgongo wa Dini kutetea ushetani uliofanyika tarehe 29 October.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…