Watangazaji wa kizazi hiki wanakera mpaka basi. Hivi wanaokotwa wapi hawa viumbe?

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Habari wanaJF?

Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha na maneno mengi. Kwa mujibu wa utafiti binafsi nilioufanya hivi karibuni, usikilizaji wa redio na utazamaji wa TV umepungua sana miongoni mwa wafuatiliaji wa habari. Hili halijatokea kwa bahati mbaya bali ni kwa sababu ya kupungua usahihi wa taarifa na ubora wa watangazaji. Sote ni mashahidi jinsi Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na Voice of Kenya (VoK) zilivyokuwa na watangazaji nguli ambao huchoki kuwasikiliza.

Watangazaji wengi wa redio na TV zinazochipukia kama uyoga hapa nchini wanakera mno kwa utangazaji wa ovyo na unaokosa weledi. Ukisikiliza redio na kutazama TV, hasa hizi zinazoitwa Redio/TV za Kijamii, utahisi kichefuchefu na huwezi kuendelea kusikiliza kwa zaidi ya dakika 5! Wanachotangaza ni zaidi ya utumbo. Na kibaya zaidi, hawa makanjanja hawakupitia kabisa kwenye vyuo vya uandishi wa habari. Inasikitisha mtangazaji kutoongea Kiswahili fasaha unabaki unajiuliza: hivi huyu mtu alienda shule kweli au ameokotwa jalalani? Na kama alienda shule, je, huko alienda kujifunza ujinga au maarifa? (FaizaFoxy, 2015). Yaani hawa viumbe hawawezi kabisa kujieleza kwa Kiswahili na Kingereza fasaha.

Zamani haikuwa rahisi mtu yeyote kujipenyeza kwenye utangazaji ikiwa hajui Kiswahili na Kiingereza fasaha. Na si hilo tu, mtangazaji anatakiwa kuwa na uhakika wa jambo analolitangaza. Juzi nilipata hasira sana niliposikia mtangazaji wa mpira akiutangazia umma kuwa mmiliki wa sasa wa Klabu ya Chelsea ni Roman Abramovich. Wanajiropokea tu ilmradi tonge liingie kinywani.

Utakuta mtu ana lafudhi mbovu na uelewa mdogo kama mbegu ya hardali lakini bado anang’ang’ania kuwa mtangazaji. Ni aibu kubwa. Yaani pale inapotaikiwa kuweka “r”, yeye anapachika “l”, kwa mfano mpira anatamka mpila. Ni aibu iliyoje! Na pia ni wazuri sana kwenye upotoshaji kwa mfano neno wimbo, hutamka nyimbo……..mfano: Leo nawachezea nyimbo moja ya Diamond inayoitwa Kantangaze. Ovyo kabisa!

Kwa ujumla, nchi hii ina watangazaji wenye uelewa finyu na upeo mdogo wa utangazaji. Natoa wito kwa serikali na vyombo vinavyohusika kudhibiti maudhui ya vyombo vya habari kufanya kazi yao kikamilifu ili kuzuia upotoshaji huu unaofanywa na baadhi ya watangazi makanjanja. Aidha, kiwango cha elimu na weledi wa mtu anayefaa kuwa mtangazaji kipitiwe upya. Watangazaji wasiokidhi vigezo wachujwe na kutupwa nje ya ulingo wa utangazaji. Tumechoshwa na upotoshaji.

Your browser is not able to display this video.

Pia soma: Jicho la tatu la Sango Kipozi katika fani ya utangazaji nchini
 
Habari wanaJF?

Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha na maneno mengi. Kwa mujibu wa utafiti binafsi nilioufanya hivi karibuni, usikilizaji wa redio na utazamaji wa TV umepungua sana miongoni mwa wafuatiliaji wa habari.
Naam ni dunia kwa ujumla
Hili halijatokea kwa bahati mbaya bali ni kwa sababu ya kupungua usahihi wa taarifa na ubora wa watangazaji.
Una Uhakika !!!!

Na sio kwamba vyanzo vimeongezeka na watu kutumia simu / gadgets zao kupata news / video on demand ?

Zamani kama unataka kujua matokeo ya mpira huko vijijini na wewe upo mjini ni kusubiri kipindi cha michezo (nina uhakika kipindi hicho hata ungepata mtu wa kukupigia redio call hata kama angekuwa na kigugumizi ungeweza kumsikiliza hata kama angekuwa anatoa neno moja kwa dakika ishirini....)

Just calling it..., as it is....
 
Mkuu hili jambo nimelifanyia utafiti kwa kusikiliza redio na TV mabalimbali na kwa kuwahoji wasikilizaji. Ni kweli wengi wamechelea kufuatilia taarifa za redio na TV za jamii kwa sababu ya upotoshaji na utangazaji wa ovyo.
 
Hii inaletwa na Kuwepo kwa mitandao ya kijamii. Karibu habari zote unazipata mitandaoni, Hata ukisema usikilize radio ama tv ni kama kurudia yale yale.
maana simu zinajitosheleza video picha , sauti na maelezo kiujumla.
 
Kweli kabisa mtoa mada, hili ni janga kubwa sana kitaifa hususani kwenye hivi vituo vya redio na tv zinazoitwa za burudani, ni madudu tu kuanzia kwa watangazaji hadi hawa wanaoitwa ma presenter
Asante kwa kunielewa mkuu. kumbe tupo wengi tunaokerwa na upotoshaji huu unaofanywa na makanjanja.
 
Hii inaletwa na Kuwepo kwa mitandao ya kijamii. Karibu habari zote unazipata mitandaoni, Hata ukisema usikilize radio ama tv ni kama kurudia yale yale.
maana simu zinajitosheleza video picha , sauti na maelezo kiujumla.
Mkuu, mimi nazungumzia kuhusu upotoshwaji wa maudhui na ubora mdogo wa matangazo unaochangiwa na uwepo wa makanjanja wengi wengi kwenye vyombo hivi vya habari. Na jambo hili nimelifanyia utafiti, sijakurupuka. Wakati mwingine mtu unaona bora upate taarifa sahihi hapa JF au kwenye mitandao mingine ya kijamii kuliko kusikiliza redio na TV zinazoboa na kupotosha taarifa.
 
Mkuu hili jambo nimelifanyia utafiti kwa kusikiliza redio na TV mabalimbali na kwa kuwahoji wasikilizaji. Ni kweli wengi wamechelea kufuatilia taarifa za redio na TV za jamii kwa sababu ya upotoshaji na utangazaji wa ovyo.
Ingawa unayosema yana ukweli lakini inabidi tu- Call a Spade a Spade...., Hii industry ipo katika transition, business models inabidi zibadilike, Competition imekuwa kubwa na consumption / concentration span ya mlaji imekuwa fupi.., sekunde mbili hauja-mshika mlaji tayari kabonyeza remote kwenda pengine..., kwenye Video on demand ndio watu wapo...

Pia Big Network News zimekuwa propaganda machines, badala ya kuangalia habari / news unapewa opinions za a given network kulingana na mlengo wao... (and this is world over) kwahio mlaji inabidi ufanye mwenyewe upembuzi yakinifu
 
Ajila chache lkn tukimchukua mtangazaji alisomea kabisaaa kazi ya utangazaji itabidi tumlipe pesa nzuuuuli ,bor tuokote okote tu hawa hawa.

Sent from my TECNO BD1 using JamiiForums mobile app
Na hiki ndicho kinaua industry in a fraction of a second. Wamiliki wengi wa redio wanaotegemea kuajiri watangazaji makanjanja wanajimaliza wenyewe kibiashara. Kama ukitaka kuteka wateja lazima uwekeze kiukwelikweli, sio masikhara.
 
Mkuu nakuelewa vizuri sana. Lakini competition ikiwa kubwa inabidi mmiliki ajiongeze kuboresha huduma ili awe tofauti na wenzake. Hapa ndipo atakapovutia wateja (wasikilizaji/watazamaji); vinginevyo kama ataendelea kuajiri makanjanja hawezi kufika mbali.
 
Kimsingi media industry imeingiliwa na washenzi. Kwa mfano mmiliki wa hii online TV angepewa hata kesi ya uhujumu uchumi ahangaike nayo
Washenzi kama hawa ndio wanatakiwa kupukutishwa kwenye industry ili kuboresha huduma za utangazji na utoaji habari sahihi. Kama tukiendelea kuwaxhekea tutavuna mabua na tusimlaumu yeyote bali sisi wenyewe kwa kuwaacha wapuuzi hawa waendelee kutamba.
 
Tatizo pia mitandao ya kijamii imewavuruga wamiliki wa redio na TV kwahiyo mtu anaangalia aajiri tu wafanyakazi wa bei rahisi ili kwenda sawa na hali ya kiuchumi. Pia sisi watanzania karibu wote tunapenda mambo ya kimbea mbea na udaku ndo maana inabidi wenye media waajiri watu watakaoenda sawa na mahitaji ya soko. Inawezekana Juma Lokole au Baba Levo ni watangazaji wa bei ghali kuliko wenye vyeti vya DSJ au UDSM kwasababu wanafit sokoni. Mimi naona twende tu hivihivi ili mradi hakuna sheria ya nchi inayovunjwa.
 
Mimi nimeacha kabisa kusikiliza na kuangalia yaani ni kichefu chefu.na hakuna chombo kinachotoa uangalizi yaani duhh basi tuu 😢😢
 
Mwijaku naye mtangazaji
Juma Lokole naye mtangazaji
Baba Levo
Orodha ni ndefu.

Hali ni shaghalabaghala
 
kabla sijamaliza kusoma, hiyo zamani unayosemea wewe kulikuwa hakuna JF na vitu kama hivyo hatukuwa na vishikwambwi tulikuwa tunasubiria saa2 ifike twende kwa mjumbe kusikiliza habari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…