tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Habari wanaJF?
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha na maneno mengi. Kwa mujibu wa utafiti binafsi nilioufanya hivi karibuni, usikilizaji wa redio na utazamaji wa TV umepungua sana miongoni mwa wafuatiliaji wa habari. Hili halijatokea kwa bahati mbaya bali ni kwa sababu ya kupungua usahihi wa taarifa na ubora wa watangazaji. Sote ni mashahidi jinsi Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na Voice of Kenya (VoK) zilivyokuwa na watangazaji nguli ambao huchoki kuwasikiliza.
Watangazaji wengi wa redio na TV zinazochipukia kama uyoga hapa nchini wanakera mno kwa utangazaji wa ovyo na unaokosa weledi. Ukisikiliza redio na kutazama TV, hasa hizi zinazoitwa Redio/TV za Kijamii, utahisi kichefuchefu na huwezi kuendelea kusikiliza kwa zaidi ya dakika 5! Wanachotangaza ni zaidi ya utumbo. Na kibaya zaidi, hawa makanjanja hawakupitia kabisa kwenye vyuo vya uandishi wa habari. Inasikitisha mtangazaji kutoongea Kiswahili fasaha unabaki unajiuliza: hivi huyu mtu alienda shule kweli au ameokotwa jalalani? Na kama alienda shule, je, huko alienda kujifunza ujinga au maarifa? (FaizaFoxy, 2015). Yaani hawa viumbe hawawezi kabisa kujieleza kwa Kiswahili na Kingereza fasaha.
Zamani haikuwa rahisi mtu yeyote kujipenyeza kwenye utangazaji ikiwa hajui Kiswahili na Kiingereza fasaha. Na si hilo tu, mtangazaji anatakiwa kuwa na uhakika wa jambo analolitangaza. Juzi nilipata hasira sana niliposikia mtangazaji wa mpira akiutangazia umma kuwa mmiliki wa sasa wa Klabu ya Chelsea ni Roman Abramovich. Wanajiropokea tu ilmradi tonge liingie kinywani.
Utakuta mtu ana lafudhi mbovu na uelewa mdogo kama mbegu ya hardali lakini bado anang’ang’ania kuwa mtangazaji. Ni aibu kubwa. Yaani pale inapotaikiwa kuweka “r”, yeye anapachika “l”, kwa mfano mpira anatamka mpila. Ni aibu iliyoje! Na pia ni wazuri sana kwenye upotoshaji kwa mfano neno wimbo, hutamka nyimbo……..mfano: Leo nawachezea nyimbo moja ya Diamond inayoitwa Kantangaze. Ovyo kabisa!
Kwa ujumla, nchi hii ina watangazaji wenye uelewa finyu na upeo mdogo wa utangazaji. Natoa wito kwa serikali na vyombo vinavyohusika kudhibiti maudhui ya vyombo vya habari kufanya kazi yao kikamilifu ili kuzuia upotoshaji huu unaofanywa na baadhi ya watangazi makanjanja. Aidha, kiwango cha elimu na weledi wa mtu anayefaa kuwa mtangazaji kipitiwe upya. Watangazaji wasiokidhi vigezo wachujwe na kutupwa nje ya ulingo wa utangazaji. Tumechoshwa na upotoshaji.

Pia soma: Jicho la tatu la Sango Kipozi katika fani ya utangazaji nchini