Watangazaji wa kizazi hiki wanakera mpaka basi. Hivi wanaokotwa wapi hawa viumbe?

Hili suala Jana BAKITA walikua wanalizungumzia kwenye kipindi cha Radio, wakagusia baadhi ya maneno ambayo yanatumika vibaya na waandishi wa habari,

Mfano neno :

Taradadi na Kwenda Matiti

Hayo maneno yanatumika vibaya

Taradadi ni neno la kiarabu linalomaanisha kua na wasiwasi juu ya Jambo fulani

Kwenda matiti ni neno la kibantu lenye maanaa ya kuishia/kwisha

Utakuta mtangazaji anatangaza anasema :

Muda ume taradadi

Badala ya kusema

Muda umeenda matiti

Vijana wengi kwenye tasnia ya Habari hususani hawa chipukizi hawana Kamusi ya Kiswahili Sanifu hilo nalo ni tatizo na hawakisomi Kiswahili wakakijua vizuri kabla hawajaingia kwenye uandishi wa habari mwisho wa siku wanatulisha madudu,
 
Hii inaletwa na Kuwepo kwa mitandao ya kijamii. Karibu habari zote unazipata mitandaoni, Hata ukisema usikilize radio ama tv ni kama kurudia yale yale.
maana simu zinajitosheleza video picha , sauti na maelezo kiujumla.
tena unapata full data wakati kwenye redio wanajali muda zaidi
 
siku hizi wamekuwa wanajali zaidi muonekano zaidi ya maudhui!
 
Ladha za akina Sued Mwinyi, charles Hilary , Ben kiko, tumbo risasi, siwatu luwanda, kumchaya, Stan katabalo, simba nyamaume, restituta bukoli, sarah dumba, sauda simba, sango kipozi, salim mbonde , David wakati, steven chisunga, pascal Mayalla, Abou Liongo, ahmed jongo, Abisai steven huku taste ya ngoma za mzee nyunyusa zikitangulia kabla ya habari, watangazaji wanatangaza hadi hutamani wamalize
 
upo sahihi kwa asilimia 100 mkuu. nikupongeze kwa utafiti uliofanya.
Charles hillary ameshawahi kusema ' huwezi kuwa mtangazaji mkubwa/nguli kwa kutangaza habari za burudani'
 
WAZIRI MWENYE DHAMANA YUPO NA ANAWASIKILIZA
 
Kikaja kizazi cha Radio Free Afrika sauti ya Afrika ulikua unawakuta watu kama Fredrick Bundala, Zubeir msabaha, taji liundi, gabriel zacharia, samadu maduhu, rebecca mulesi, Rahab fungo, Baruan Muhuza, kid bway, fredwaa, mukhsin mambo, gamba na wengine wengi, baada ya hao clouds ikatake over sasa wao wakawa zoazoa kama kokoro wakajificha kwenye creative na habari ikaishia hapo
 
Wale ni Form four wali feli, ni weupe sana kichwani na wanajua sana vitu vifuatavyo.
1. Udaku, mambo ya kufamaniana na kadhalika.

2. Michezo simba na Yanga

3. Mambo ya kusifia hasa CCM mambo ya kijipendekeza

4. Maada za Familia hasa Ma house Girl.
 
Kweli kabisa mtoa mada, hili ni janga kubwa sana kitaifa hususani kwenye hivi vituo vya redio na tv zinazoitwa za burudani, ni madudu tu kuanzia kwa watangazaji hadi hawa wanaoitwa ma presenter
Kule hakuna Watangazaji, wale angalia tu aina ya vipindi, ni weupe kichwani acha kabisa,
 
Sasa watu aina ya lokole nao wamekuwa watangazaji

Ova
Hapo sasa. Watu wa ovyo kabisa wasiokuwa na kitu kichwani wala kuwa na maadili ya utangazaji eti nao wamevamia utangazaji. Ovyo kabisa!
 
Mimi nimeacha kabisa kusikiliza na kuangalia yaani ni kichefu chefu.na hakuna chombo kinachotoa uangalizi yaani duhh basi tuu 😢😢
TCRA wanapaswa kusimamia maudhui ya media zote lakini wamebung'aa tu hapa JF kuwinda watukanaji na kuwapiga faini. Nchi ya ovyo sana hii.
 
kabla sijamaliza kusoma, hiyo zamani unayosemea wewe kulikuwa hakuna JF na vitu kama hivyo hatukuwa na vishikwambwi tulikuwa tunasubiria saa2 ifike twende kwa mjumbe kusikiliza habari.
Mkuu, ukimaliza kusoma utang'amua kuwa naongelea maudhui inayopotoshwa na makanjanja waliojichomeka vyumba vya habari huku wakiwa hawana uwezo wa kiutangazaji. Ndio maana tumegeukia alternative means baada ya kuona kwenye redio na TV hakuna taarifa zinazoeleweka.
 
Kimsingi media industry imeingiliwa na washenzi. Kwa mfano mmiliki wa hii online TV angepewa hata kesi ya uhujumu uchumi ahangaike nayo
View attachment 2411411
Freedom of Speech tukianza kufungia watu kwa kigezo hiki tutafungia wote kwa vigezo vyovyote...
I might disagree of what you say But I will defend to the death your right to say it”

By the way wewe kama unakwenda kwa mdau kama huyo kupata concrete news nadhani tatizo lipo kwako na sio kwa mtoa habari...., What next utachukua ushauri wa ki-afya kutoka kwa Tom and Jerry ?
 
Bila shaka wewe ni miongoni mwa wale mnaotetea haki za mashoga. Yaani mtu anayezua taarifa za uongo kama hizo nae asifungiwe wala kuchukuliwa hatua zozote? Ingekuwa mpendwa wako aliyekutoka kazushiwa hivyo ungekaa tu kimya?
 
Bila shaka wewe ni miongoni mwa wale mnaotetea haki za mashoga. Yaani mtu anayezua taarifa za uongo kama hizo nae asifungiwe wala kuchukuliwa hatua zozote? Ingekuwa mpendwa wako aliyekutoka kazushiwa hivyo ungekaa tu kimya?
Kwa kweli wanahabari wanaotoa taarifa za uwongo na zinazoleta taharuki kwenye jamii yafaa wachukuliwe hatua kali za kisheria bila kuwaonea huruma yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…