Utangazaji wa kutangaza kila movement ya mpira unatoka kwa huyu kwenda kwa yule mechi nzima kama vile uko redioni ambao bado inafanywa na Azam umepitwa na wakati.
Utangazaji wa kisasa ni wakati mchezo unaendelea, kutoa tathmini ya mchezo ulivyo, uchezaji wa timu na mchezaji mmoja mmoja hasa pale anapohusika katika tukio la mchezoni, taarifa muhimu za nyuma zinazohusiana na mchezaji au timu zinazoendana na matukio ya mchezoni na kuchanganya na kutangaza movement za mipira (hiko kinachofanywa kiasi kikubwa na watangazaji wetu) kwa kiasi fulani wakati mchezo unaendelea