Watangazaji wengi wa radio hawajui kingereza

Watangazaji wengi wa radio hawajui kingereza

Radio ya kiswahili, kiingereza cha nini?. Tatizo hata hicho kiswahili nacho shida tupu. Chetu hatukijui vizuri tunarukia vya wengine!
 
Umejibu muruwaa The BOSS
Kama hawatakiwi basi wasizungumze. Ila kwa kweli ni vema kuwahimiza vijana wajifunze kiingereza kwani wanaongeza fursa zaidi za ajira huo ndio ukweli la sivyo wanaweza amini baadhi wanapendelewa kumbe tu wamepata fursa kwa sababu ya kuwa na lugha zaidi ya moja. Aidha si kama miaka ya nyuma angalau sasa hivi kuna sehemu za kujifunza/ kujinoa hiyo lugha ya kiingereza, wa sacrifice matumizi mengine wajifunze kuongeza FURSA!
 
Kingereza cha nni wewe tunaoskiliza tabu kikielewa na pia wanaotaka kuvuka boda kiajira wajiongeze ila kama ni kibongobongo kiswahili kinatoa

Watu wengine wanavoshobokea kingereza utandhani oxygen

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kama hawatakiwi basi wasizungumze. Ila kwa kweli ni vema kuwahimiza vijana wajifunze kiingereza kwani wanaongeza fursa zaidi za ajira huo ndio ukweli la sivyo wanaweza amini baadhi wanapendelewa kumbe tu wamepata fursa kwa sababu ya kuwa na lugha zaidi ya moja. Aidha si kama miaka ya nyuma angalau sasa hivi kuna sehemu za kujifunza/ kujinoa hiyo lugha ya kiingereza, wa sacrifice matumizi mengine wajifunze kuongeza FURSA!
bora uwaeleze maana ubishi umewajaa tu
 
Huwa nawasikia. Kwa kiswahili kizuri (si fasaha) hawajambo. Tatizo huja pale wanapotamka maneno ya kingereza, ni aibu. Nashauri waajiri wawe wanatilia maanani hii lugha pia maana hao watangazaji wanaaibisha taaluma zao.

Kweli kabisa.Na pia mi najiuliza,kwa nini kwenye tuongee magazeti wanapofika gazeti la kiingereza wana litafsiri kiswahili wakati wasomaji ni wanaojua kiingereza,hivi mzungu kwa mfano ataelewaje ukimtafsiria kiswahili au hawataki wanunue au ndo kuogopa kuchapia?
 
Off course sio lugha yao ya asili ni ya mkoloni. Kule uingereza na Marekani ni aibu zaidi, watangazaji karibu wote hawajui kiswahili.....

tehtehteh......
JF never boring, kwa hisani ya The Boss
 
Kweli kabisa.Na pia mi najiuliza,kwa nini kwenye tuongee magazeti wanapofika gazeti la kiingereza wana litafsiri kiswahili wakati wasomaji ni wanaojua kiingereza,hivi mzungu kwa mfano ataelewaje ukimtafsiria kiswahili au hawataki wanunue au ndo kuogopa kuchapia?
naona kuna baadhi ya watangazaji walipitia hii post. Nawasikia wanajitahidi kweli kuongea kingereza
 
Hata kiswahili hawajui kuna siku nilikuwa nasikiliza Radio nikasikia Mtangazaji anasema ohoo MTONYO , MARA WANANGU WENYEWE , MARA MCHIZI , Nikaishia kutoka kapa ! so hata Kiswahili ni kigumu vile vile
 
Kiingereza cha kazi gani na redio na tv zetu ni za kiswahili ?

Mimi hakuna kitu kinaniumiza kama kumsikiliza mtangazaji anayekibananga kiswahili..haswa kama anachotangaza ni jambo muhimu na inanilazimu kumsikiliza.

Otherwise huwa nahamisha stesheni pindi ninapogundua mtangazaji ni kanjanja asiyejua kiswahili fasaha na haswa anayechanganya R na L.
 
Huwa nawasikia. Kwa
kiswahili kizuri (si fasaha) hawajambo. Tatizo huja pale wanapotamka
maneno ya kingereza, ni aibu. Nashauri waajiri wawe wanatilia maanani
hii lugha pia maana hao watangazaji wanaaibisha taaluma zao.

Kwani ni lazima waongee kiingereza kama asilimia 80 ya wasikilizaji wao ni watumiaji wa kiswahili?
 
Kwani ni lazima waongee kiingereza kama asilimia 80 ya wasikilizaji wao ni watumiaji wa kiswahili?
Ishu si kuongea kingereza, bali kujua kingereza kwa ufasaha. Wapo ambao husema maneno ya kingereza redioni wakajikuta wanachemka vibaya. Ni bora wabaki kwenye kiswahili mwanzo mwosho kama lugha za watu hawazijui vizuri
 
Back
Top Bottom