Watangazaji wetu kwanini hamjifunzi majina/maneno fulani yanatamkwaje?

Nadhani wewe pia huelewi matamshi halisi yanatokana na lugha halisi.KISHWAHILI UTATAMKA AJAX WENYEWE WOHOLANZI WANATAMKA AYAX.MFANO MSUKUMA AKITAMKA MASANJA NI TOFAUTI NA MZUNGU.ILA UNATAKIWA UJITAHIDI UTAMKE KAMA WENYEWE.
 
Kama ningekuwa mtangazaji ningehakikisha natafuta matamshi sahihi.
 
Nadhani wewe pia huelewi matamshi halisi yanatokana na lugha halisi.KISHWAHILI UTATAMKA AJAX WENYEWE WOHOLANZI WANATAMKA AYAX.MFANO MSUKUMA AKITAMKA MASANJA NI TOFAUTI NA MZUNGU.ILA UNATAKIWA UJITAHIDI UTAMKE KAMA WENYEWE.
Kama ni mpenzi wa mpira utagundua hata Waingereza wanatamka Ayax
Real Madrid Waingereza wenyewe wanatamka real sio ril
 
I sense inferiority complex[emoji16] kiswahili ni lugha kubwa dunia hii naomba kuanzia leo ujivunie hilo
 
Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zenye maana na zilizokubaliwa na jamii ya watu fulani ili zitumike katika kuleta mawasiliano.
Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu kwa sababu zilitokea kama bahati tu kwa binadamu. Hakuna lugha bora zaidi duniani, kwa kuwa lugha zote zina ubora, mradi zikidhi matakwa ya jamii husika.

Kusudi kuu la lugha ni kuwasiliana na kuelewana, na sio kupimana uwezo wa kujua mambo, huwezi mlazimisha mreno aongee kichaga kama mchaga anavyoongea kichaga.. mimi sioni kusudi lako kuandika uzi huu.
 
Kama huoni kusudi si ungepita kimya tu. Maelezo meeeengi OP.
 
Hii inanikera sana mimi. Mwandishi wa habari anapaswa kujifunza kuandika sawasawa na kutamka sawasawa majina ya watu/vitu/nchi/miji n.k. Angalau zamani tulijifunza hayo shule za msingi.
 
Wanakera kinoma utafikiri hawana hata maboss wanaojua mambo. Kuna jamaa wa Sibuka FM huwa anatangaza mechi huwa anajidai anajua sana na mbwembwe kiabo ila UTI anaitamka "yutihai"

Wanaboaga kinoma wapewe semina elekezi
 
...Hilo eneo la Bwagamoyo lilikuwa na maana yake na hilo neno, yaani watumwa wote walokuwa wakifika hapo kutokea bara waliambiwa wabwage mioyo yao hapo.

Ilikuwa ni sehemu ya kuaga Afrika kwenda utumwani huko uarabuni
Haswa, ni sawa na ilivyo Badagry (Nigeria) na Gorée (Senegal) au Elmina Castle (Ghana) kwa watumwa waliosafirishwa magharibi.
 
mimi wananiacha hoi utasikia mchezaji Messi ana dhamani ya dola ..... badala ya thamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…