Watangazaji wetu kwanini hamjifunzi majina/maneno fulani yanatamkwaje?

......wabrazil wao herufi "J" humaanisha "H"..mfano yule mchezaji nafikiri alikuwa Manchester United..Jesus..wao wanatamka Hesus!
Kispanyola j inatamkwa h.. Sasa kwa brazil sijui km kireno na kispain vinafanana..

Tunapata wakina huan mata, hames Rodriguez etc
 
Hujaelewa nini kinazungumzwa hapa. Ushasasikia watangazaji wa Kiingereza wakitamka Jose Mourinho,Juan Mata au Thierry Henry? Wanatamka kwa jinsi inavyotamkwa kwa lugha za wahusika. Na hapa nazungumzia watangazaji si watu wa mtaani.
Sizungumzii accent, kutamka lesesta badala ya lesta sio accent.
 
Mimi neno dubai kila mtu analitamka kivyake,wengine nahisi kawa wanalitamka vile ili kuupandisha status ya eneo.
 
Kuna matako mmoja yuko Generation FM alikuwa anasema "boss wa cash money butt man amekutana club na Lil Wayne"
Hapo kwenye butt man alikua anamaanisha Birdman.
Hao wa kwenye hivyo vipindi vya Muziki ndio tatizo kubwa sanaaa, yaani wengi wanapenda Umarekani alafu Umarekani unawakataaa. Wengi ni. Vilaza ambao wanajifanya wanajua kila kitu wakati hamna Kitu!
 
kuna mtangazaji mmoja alikuwa anatangaza ishu za uingereza si akataja Cheshire? akaitamka kiswahili yaani "Cheshire"
 
Nimekumbuka mwl wangu wa primary akitamka: Greenwich
Griniwichi!
 
UNGEMSIKIA MTANGAZAJI ALIYESOMA NENO DO (doh) OR (o) DIE (diye) ALIYATAMKA KWA KISWAHILI KAMA YALIVYOANDIKWA.
 
Bado narudia,sijaona kosa kubwa la mtangazaji wa kiswahili,nilichogundua tunataka mswahili atamke kwa lafudhi ya nchi husika,hilo haliwezekani kwa sababu hata mzungu (kulingana na taifa lake)hawezi tamka maneno ya kiswahili kwa lafudhi ya kiswahili lazima atagongagonga lafudhi,ndio maana kuna mataifa j wanaita h,eg mtangazaji mmoja aliyekuwa redio one alikuwa anaitwa josef ndamalya,kwenye taarifa ya habari anajitambulisha kama josef ndamalya,,kwenye mipasho utasikia anajiita hozee ndamalya
 
mkuu usichanganye mafaili yaani mtangazaji asiwe na general knowledge of the world ? sasa kutakuwa na tofauti gani na any layman kuwa mtangazaji? huko chuo kozi aluzofundishwa zina maana gani? elimu yake ya sekondari A level ya historia ,geografia na lugha inamsaidia nini?
 
Unakomaa huku hata huelewi nini kinazungumzwa. Sijazungumzia lafudhi aka accent hapa nazungumzia makosa ya matamshi kabisa mfana Leicester inatamkwa Lesta sasa mtu anatamka lesesta,hapa sio lafudhi ni kukosea kabisa.
 


Wanaboa sana haswa Tunu Hassan na Maulid Kitenge wa EFM, mi namshangaa sana Maulid. Jamaa uwa anasafiri sana ila kutamka majina ya miji ya watu au majina ya wachezaji kwake ni shida sana tena anatamka kwa mbwembwe kama senge fulani hivi linalovutia matamshi ili aopolewe. Yaani ananiboa sana.
 
Ujue haya hata watangazaji magwiji ulaya pia wanashindwa tamka majina ya kiafrika vizuri. Mfano wanyama wenyewe humuita WANYIAMA. ni jambo la kawaida kushindwa tamka neno lisilo Lugha yako, mm sion kama ni ttzo na kama n ttzo basi ni ttzo la dunia.
 
Hii shida kubwa hasa kwa watangazaji wa sport! Tatzo Ni kua huwa hawajiandai kabla ya kwenda studio!!
 
Kuna huyu wa Yanga wanatamka Shishimbi... jina lake linaandikwa Tshishimbi.. na namna inavyo tamkwa ni Chishimbi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…