Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Watanzania 173 waliokuwa wakiishi katika Jimbo la KwaZulu-Natal, Afrika Kusini, wamewasili nchini baada ya kuamua kurejea nyumbani kwa hiari, kufuatia vuguvugu la kupinga wageni linaloendelea nchini humo. Kundi hilo lilirejea Tanzania kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, kwa ndege ya Air Tanzania.