Watanzania amkeni, viongozi hawana huruma na wananchi

Watanzania amkeni, viongozi hawana huruma na wananchi

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Nilileta Uzi hapa kuonesha matumizi mabaya ya serikali, au niite matumizi yasiyo na msingi.

Semina ya sensa wiki tatu ilikuwa haina ulazima. Siku 3 tu zingetosha. Sasa ngoja nitoe mfano mmoja tu ili mjue kuwa serikali hii haina huruma na mwananchi.

Mwaka huu serikali ilikuwa na zoezi la post codes (anuani za makazi). Mabilioni yalitumika katika zoezi hili. Na sasa kuna zoezi la sensa nalo limetafuna mabilioni ya pesa.

Cha ajabu katika zoezi la sensa nalo kuna zoezi la kuhesabu makazi. Sasa kwanini zoezi la kuhesabu makazi lisingejumuishwa pamoja na zoezi la sensa?

Au kwanini zoezi la sensa libebe na bajeti ya kuhesabu makazi ilhali ndani ya mwaka huu huu tumetupa mabilioni mengine kwenye zoezi la kuhesabu makazi?

Ni dhahiri serikali hii imejaa watu wenye mawazo finyu na kutokujali.
 
Ndio maana walipambana kufa na kupona washinde uchaguzi 100%
 
Uko sahihi, hii serikali ina matumizi ya hovyo sana
Waswahili wakishaona pesa ipo basi huanzisha vishughuli vya hapa na pale visivyo na tija.

Mara birthday party, mara sijui kipaimara mara sijui kumtunza nani and so forth.

Hivi visensa havina tija yoyote kwa maendeleo ya taifa.

Wana wenyeviti wa vijiji na mitaa na wajumbe ni kazi ya siku moja tu wanakupa data zote.
 
Back
Top Bottom