Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Nimewahi kulizungumzia hili, na nitalizungumza tena. Watanzania bado tuna akili mbovu sana ya kuuona uteuzi kama fursa ya "kuula" au kufaidika kibinafsi.
Tunalaumu ufisadi, huku mtu anaefanya kazi TRA asiponunua gari miaka miwili baada ya kuanza kazi tunamwona mjinga! Ni wazi kwamba kama jumuia tunatarajia watu wanaofanya kazi sehemu kama TRA au trafiki polisi au nafasi fulani ya juu watumie nafasi zao kujinufaisha, nje ya mishahara yao halali.
Inafika mahali watu wanaoteuliwa katika nafasi fulani inabidi wafanye ufisadi kwa kuwa wasipofanya jumuia ya Watanzania itawaona wajinga kwa kutotumia nafasi zao za kazi kujinufaisha! Na dhambi kubwa sana aliyofanya raisi Samia katika kufikiri huku kulikopotoka ni kusema kwamba kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake! Amebariki usemi kwamba yule jamaa alikuwa TRA miaka ishirini kastaafu hana kitu!
Unakuta raisi akitangaza baraza la mawaziri, tunaona January Makamba ameula kwa kuwa amepewa wizara ya Nishati na sio wizara ya Wanawake na watoto. Na akihamishiwa wizara ya utamaduni na michezo akaendeleze vipaji vya uandishi tunaona ameporomoka na aliechukua nafasi yake ameula! Nasikia kuna baadhi ya mawaziri baba zao wenye influence wanashinikiza watoto wao wapewe wizara zenye "ulaji"!
Kama kweli hautubariki ufisadi, kwa nini tuone mtu fulani ameula anapopewa kazi TRA au kuteuliwa waziri wizara ya Nishati badala ya Wizara ya Wanawake? Kwa nini tumseme mtu anaefanya kazi TRA au trafiki polisi ni mjinga ikiwa anaishi kwa mshahara wake halali? Kwa nini nikiteuliwa kuwa mkurugenzi wa Tanesco au REA unaniona mie mjinga kwa kuwa naishi maisha ya kawaida kwa kutumia mshahara wangu?
Halafu tunauliza maswali eti kwa nini nchi yetu haiendelei, wakati akili zetu zimejaa ufisaidi tu. Siku tukiondokana na mawazo haya ya kifisadi, kwa kuona kuteuliwa ni nafasi ya kujenga taifa na sio kuukata au kuula, basi nchi yetu itapiga kasi kubwa sana ya maendeleo.