Watanzania hatuelewi tunachotaka,ni roho mbaya tu

Mkuu subiri matusi sasa , humu ndani ukweli hautakiwi. Unatakiwa uzungumzie kuchoma nchi, Serikali ipinduliwe kama yanayotokea yameanza awamu hii.
Mkuu kwahiyo watu waache mambo yaendelee kama yalivyo kwa sababu yalikuwepo kabla yake?

Tufanye sawa kuwa utekaji ulianza wakati wa Magufuli, watu tukaamini baada ya kufa Magufuli basi hayo mambo hayatokuwepo tena. Ila sasa hivi huo utekaji umezidi kushinda kipindi cha Magufuli na sasa hivi watu wanatekwa hadharani hadi imekuwa kama jambo la kuzoeleka sasa kama tukiliacha sasa hivi akija mwengine tutegemee utekaji kuzidi zaidi. Hiyo wewe unaona sawa?
 
Wewe ni mjinga period
Eti kwasababu utekaji ulianza na jpm basi tumuache Samia aendelee kuteka na kuuwa. Mleta mada wewe ni wa HOVYO
 
Si sawa.
 
Hoja ni mbona kwa magufuli hamkufanya jaribio la kumpindua, ila kwa samia ndo mfanye?
Magufuli aliweza kuwin mioyo ya watu wa hali ya chini kwanza kwa kuwathamini na kuwatambua na ndio maana kwenye mashirika na taasisi za umma mwananchi wa kawaida akienda kwaajili ya kupata huduma anapata huduma kiwepesi. Alifanya vitu vingi vya kimaendeleo vya kumjali mtu wa chini.

Wananchi wa hali ya chini ndio kundi kubwa la watu hivyo ukiweza kuishi nao vyema hupati nao shida ila Samia kashindwa kuishi na wananchi wa hali ya chini na ndio hao wanaoandamana.
 
Baadhi uliyoyaandika ni kweli, lakini umeuacha mkweli mmoja ambao ni muhimu kuliko yote:

Hayati Magufuli alikuwa na tatizo kwenye kuheshimu demokrasia na haki za watu. Lakini kwa upande mwingine, Magufuli alikuwa na mapenzi makubwa kwa Tanzania, ndiyo maana hakuwahi kupora rasilimali za nchi akawagawia wageni kwa malipo ya rushwa binafsi au ya wanafamilia, kama huyu mama.

Pamoja na ukweli kwamba viongozi waliomtangulia walikuwa na makosa yao, lakini hakuna aliyefikia uovu wa hata 25% ya uovu wa utawala wa huyu mama.

Watu waliotekwa na kupotezwa na utawala wa Hayati Magufuli, sidhani kama walifika hata 50, huyu mama ni zaidi ya 180. Hakuna mtawala aliyeua watu kwa maelfu isipokuwa huyu mama. Yaani ni kwamba hakuna utawala katika bara zima la Afrika aliyewahi kuua waandamanaji na wasio waandamanaji kwa maelfu ili tu yeye awe Rais, ni huyu mama pekee yake. Huyu lazima atabakia kwenye historia ya Dunia kama mwanamke pekee aliyewahi kuwa katili kuliko yeyote. Ni katii kiasi cha kutojutia uovu wake uliosababisha maelfu ya roho za watu kupotea. Inaonekana anafurahia sana kuua watu, ndiyo maana watu wakiuawa, majibu yake huwa ni ya kejeli kubwa.
Ulimsikia alipoulizwa kuhusu watu kutekwa? Alijibu kuwa hakuna anayetekwa, huzo ni drama tu.

Alipozungumzia mauaji ya kikatili dhidi ta Ali Kibao, alisema kuwa kifo ni kifo tu. Huyi inaonekana ana roho ya uuaji, haumizwi wala haguswi wala kuimizwa na uhai wa binadamu wenzake kupotea. Bila shaka shetani amefanya makao ndani ya moyo wake. Tulimpenda sana mwanzoni, tukamsifia, kumbe tulikuwa tunamsifia muuaji, tunaomba Mungu atusamehe kwa kosa hilo.
 
Samia ameshindwa kwa mujibu wa tafsiri yako tu, samia kafanya makubwa kumzidi magufuli kwa muda mfupi sana, magufuli anafariki miradi yote mikubwa ilikuwa hata haijaanza, samia kajenga daraja la busisi mwanza, sgr dar to dom kakamilisha, stigler gorge kakamilisha na miradi kibao ya kijamii iliyopunguza adha kwa wananchi, kafungua uchumi wa nchi uliokuwa banned sera mbovu za magufuli, lkn watu msio na shukrani leo samia anaonekana mbaya halafu muovu magufuli ndo anasifiwa, haya tukisema hapo kuna ajenda ya kidini mnalala mbele!
 
Ulichokisema kina ukweli 75% lkn kwa Hali ya sasa hakuna atakaekuelewa.( Hasa hapo kwenye vikundi vya utekaji, kuvuruga uchaguzi,kuminya uhuru wa habari na kujieleza n.k

Kosa lake: alitakiwa kurekebisha haraka sana mambo hayo, vikundi hivyo vilimzidi nguvu samia
 
Sababu ya kwanza umetaja 'UFISADI,' apendwe tu kwa sababu hiyo? Halafu upunguze haraka uweke space kati ya maneno
 
Mtoa maada ni kiazi na hana akili

Kipindi hiki cha mama kila mtu ni billionaire kila waziri....enzi JPM haya hayakuwepo

Ndio
 
Baada ya kuiba uchaguzi ndo anataka aongee,watu walimwambia arekebishe kabla,arekebishe sheria za uchaguzi kabla,yeye akajua akirekebisha hatoboi
Kurekebishwa kabla mlipaswa muanze kumuhimiza magufuli!!
 
Na hapa ndo mnazidi kukosea,huwezi kulazimisha kupendwa,Magufuli alipendwa sana na wananchi haswa wa hali ya chini,na ni kitu alichojijengea tangia akiwa waziri kwa awamu ya Mkapa,huyu mama yako huwezi mlinganisha hata kidogo na Magufuli,nadhani kwa rate ya kuchukiwa ni kubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…