Watanzania hawawezi kuandika

Mkuu,hoja imeeleweka ila kwanza hatutaki lugha ya kiswahili ipotee,ndio maana tumeanza kwa kurekebisha uandishi wake kwanza.
 
Ulichoelezea ndio msingi wa hoja yangu.

Uwezo wa kukosoa unaishia kwenye serufi tu.

Lakini kwa kutumia jukwaa la ‘stories of change’ kama kipimo cha uwezo wa uandishi wa mantiki.

Watanzania atuwezi andika.

Uwezi kujiandikia tu mambo kutoka kichwani hayo mambo ayakubaliki academically.
 
Hupendi kukosolewa
 
Hupendi kukosolewa
Tofauti kabisa, kwa sababu sijui kila kitu. Kwa mtazamo wangu uwezi nikosoa isipokuwa unanifunza kitu kipya.

Likewise sina muda wa kumu-encourage mtu mwenye mtazamo wa hovyo kwa ustaarabu anaotaka yeye.

Kama uwezi kuandika nitakwambia uwezi kuandika hakuna namna nyingine ni uwezi kuandika.

Kiła mtu ana standards zake lakini kwa mtazamo wangu with academic justification asilimia kubwa ya michango ya ‘stories of change’ wachangiaji hawana uwezo wa kuandika.
 
Mkuu,hoja imeeleweka ila kwanza hatutaki lugha ya kiswahili ipotee,ndio maana tumeanza kwa kurekebisha uandishi wake kwanza.
Nadhani mngelifanya hivyo pamoja na kujadili kiini cha hoja yake.

Kwanini ujikite katika hoja ambayo sio kiini cha mada yake?

Hujaona katika kujenga hoja yake ameweka wazi kwamba sarufi sio kiini cha hoja yake kwasasa?

Kwanini usianzishe mada yenye hoja itakayojikita kuboresha sarufi katika machapisho ya 'Stories of Change 2024' ili kuongeza ufanisi wa programu hii?
 
Tunamrekebisha hapa hapa hakuna haja ya kwenda mbali,
Chuma kikipata moto ndio muda sahihi wa kupondwa,huwezi kukisubiri chuma mpaka kipoe.
 
Nakubaliana na hitimisho lako. Una shabaha njema.

Nitoe rai! Mnaoshiriki 'stories of change',Machapisho yenu ni 'pendekezo la mradi', jitahidini kuzingatia usahihi wa kimantiki. Hivyo ni vyema mzingatie uandishi wa kitaalamu.
 
Tunamrekebisha hapa hapa hakuna haja ya kwenda mbali,
Chuma kikipata moto ndio muda sahihi wa kupondwa,huwezi kukisubiri chuma mpaka kipoe.
Sidhani kama upo sahihi. Chuma cha paswa kuwa machapisho ya stories of change ili ya kidhi vigezo.

Mwanzisha mada kafanya kutuamsha katika muundo wa uandishi.
 
mazingira tuliyojengewa ya kukariri masomo toka shule za awali yanachangia kwa kiasi kikubwa uandishi kuwa mbovu na hafifu, unakariri la saba, 4, 6, chuo, research unaandikiwa unanakiri, dissertation unanunua na kumeza, sidhani kama unaweza tegemea uandishi mzuri. Mtoto akiharibu kitu unapiga kama unataka kuua bila kujiuliza kama ndo namna yake ya kujifunza kufanya utafiti. Bila kubadilisha mfumo wa maisha tuliokariri, tuzoee changamoto hiyo kwani ni ya kudumu.
 
Tunamrekebisha hapa hapa hakuna haja ya kwenda mbali,
Chuma kikipata moto ndio muda sahihi wa kupondwa,huwezi kukisubiri chuma mpaka kipoe.

Fuatilia hiyo mada uone mtazamo nilioanza kutokana nauelewa wangu wa nia njema ya waziri (nia njema ambayo bado naiunga mkono).

Na mtazamo wangu kwenye hiyo-hiyo mada baadae; baada ya kuambiwa kuna facts za mgogoro sijashikiliza. Na mtazamo wangu ulivyobadilika baada ya kupata facts mpya

Mimi ni flexible na open to new knowledge/information na kubadili mtazamo wangu. Uwezi kuwa mjuaji wa kila kitu na uwezi jifunza mambo mapya kwa kujiongopea unajua kila kitu.
 
Nakubaliana na hitimisho lako. Una shabaha njema.

Nitoe rai! Mnaoshiriki 'stories of change',Machapisho yenu ni 'pendekezo la mradi', jitahidini kuzingatia usahihi wa kimantiki. Hivyo ni vyema mzingatie uandishi wa kitaalamu.
Kabisa na ndio hoja yangu.

Uwezi kujiandikia vitu tu kutoka kichwani kwako.

With that good morning JF

🙏
 
Mkuu Mayor,
Mimi binafsi sijui vigezo vya hizi stories of change labda wanatakiwa waandike wao wenyewe. Na hizo siyo academic paper. Kumbuka wewe umeweka ushahidi wa article yako ambayo inawezekana imepita kwa editors kadhaa na wasimamizi kadhaa. Hawa wa stories of changes siyo academicians wengi wanaandika kupata mitaji au rizki huo muda na pesa ya kumlipa editor wanatoa wapi na labda siyo kigezo Cha kushinda.
Amin amin nakwambia hata maprofessor na academicians wanakosoana sana ktk hizo academic hata kuitana vilaza wao kwa wao sembuse sisi tusiosoma sana
 
Hata sijaendelea kusoma upuuz wake.
 
Kuna vitanzania vipo pale harvard kutwa kuchwa ni instragram kujianika. Ndio hawa hawa wapuuz.

Yaani kitendo cha kuforce na kuingia pale wanajiona wajanja kumbe marimba tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…