Watanzania huyu Msanii Madebe 'Nabii Mswahili' amewakosea nini? Kwanini mmempuuza sana? Ana kosea wapi? Kwanini asogei?

Watanzania huyu Msanii Madebe 'Nabii Mswahili' amewakosea nini? Kwanini mmempuuza sana? Ana kosea wapi? Kwanini asogei?

Wasalaam wanajamvi!

Kuna wasanii kwenye sanaa yetu wanayo bahati na wengine hawana bahati kabisa!

Kuna wasanii hawajui kuigiza kabisa lakini wanapendwa sana utafikiri wanajua sana lakini sio kweli!
Mfano wasanii Kama Ray Kigosi na Steve Nyerere huwa sielewi wanaigiza nini lakini kusema ukweli wana mashabiki wengi sana pamoja na utumbo wanao igiza bado wanapata attention ya watu na kupewa nafasi ya kusikilizwa!

Leo nataka niwaulize watanzania kwanini mmempuuza msanii Mabede a.k.a Nabii Mswahili?

-Madebe amewakosea nini?
-Madebe anashida gani na watanzania?
-Madebe anakosea wapi?
-Kwanini mmempuuza?

Msanii huyu ana jitahidi sana ana hangaika sana kutafuta attention ya watanzani lakini kusema kweli watanzania wamekataa kabisa kabisa!

Huyu kijana ana jaribu kila mbinu lakini hasogei kabisa bado najiuliza afanye nini hili asogee? Kwanini mmepokea Ray na Steve Nyerere lakini mnashindwa kumpokea Madebe a.k.a Nabii mswahili?

Wana Jf hebu twambieni huyu kijana ana shida gani? Amewakosea nini watanzania? Kwanini ananyimwa nafasi ya kusikilizwa kuangaliwa? Kwanini asigezwi wala kusogea?

Watanzania huyu kijana amewakosea nini?

View attachment 1572362
View attachment 1572363
View attachment 1572364
View attachment 1572365
View attachment 1572366
Yaani huyu jamaa anaweza kuongea vi2 mpk ukajiona umepotea kabisa[emoji3] ukimfuata unaweza ukatembea uchi kwa sababu tu umezaliwa ukiwa uchi
 
Kuna 'audio na visual' na huyu bwana nadhani fani yake ni ya kusikiliza zaidi kuliko kuigiza.

Anachotakiwa kufanya ni kukaa kwenye upande sahihi, yaani awalenge Wasikilizaji wa misemo yake na uigizaji awaachie Waigizaji.

Na sidhani kama umaarufu wa Mtu kama Steve unatokana na uigizaji, kati ya Watu 10,000 ukiwaambia wakutajie filamu moja ya Steve ukimpata mmoja ni bahati sana..umaarufu wa Steve unabebwa na mlolongo wa matukio nje na uigizaji.

Mtu kama Ray alishafahamika tangu enzi za 'Kanumba vs Ray', kwa hiyo hata kama hana jipya lakini bado walau kuna cha kujikumbusha.
Kweli maana jamaa Kila movie ni misemo tu abadilike
 
Kwakweli mi sijawai muelewa hata cd yake iwe bure sibebi najua hana cha kunielimisha haniburudishi bora akina mpoki,mau,tiny white na ringo
 
Mimi naona kadri siku zinavyosonga mbele ndivyo Madebe Lidai anavyozidi kusonga mbele kwa sasa katika wasanii waliopo nyota yake inazidi kung'aa
 
Tatizo hajapata platform,kama ni tv sikuhizi watu hawaangalii sana,,aweke kazi zake utube
 
Yaani huyo jamaa mnampendeaga ninj
Yaani filam anafyatua hovyo hovyo halafu hayaeleweki
 
Kwani ina tofauti gani na za wengine? Kwani ya Steve nyerere ikoje?
Ni mswahili saaana, so waswahili wako Dar tu.

Siyo Kila mtu ni mfuasi wa misemo na maneno meeengi isiyo na maana kama ya Mpoki
 
Ukiwa humuelewi madebe basi utakuwa una ugonjwa wa akili sababu wenye akili timamu hufaidika na fasihi zake mie namfatilia sana hasa movie yake inaitwa matusi iko vyema sana

Sent from my TECNO-W3 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo hajapata platform,kama ni tv sikuhizi watu hawaangalii sana,,aweke kazi zake utube

Anaweka na anakimbiza
Zaidi ya 100k subscribers
 

Attachments

  • IMG_20200919_100356.png
    IMG_20200919_100356.png
    33 KB · Views: 2
Bongo kutoboa kupitia Tasnia ya uchekeshaji ni ngumu mno kama kuwa mwana hip hop vile. Mbaya zaidi ukiwa huna "kismati/Charisma" utasota mnoo 😢. Mchizi aangalie hizo mbinu zake za uchekeshaji je zinavutia kwa wote au zinalenga kundi moja la watu.
 
sijaelewa vizur, yaan leo hii vicent kigosi wakulinganishwa na Madebe?
Duuu..hata kama humpendi Ray sio kwa GUBU hilo mzaz..
Ray tumeanza kumuona tangu kaole miaka ya 2001 huko then unakuja mfananisha na huyu muigizaji wa mipasho..
 
Back
Top Bottom