Watanzania kama Kingereza kimewashinda, mbona msiwe mnatembea na wakalimani ili kuondoa aibu ndogo ndogo

Nchi ya watu milioni hamsini hakuna mtu anayekifahamu kiingereza, Mungu saidia watu wako.
 
Huwezi kunipangia niandike nini kwa kiwango gani; we jamaa wa wapi wewe?! Hata hapa ni wewe umeanza kuni-quote, na hata post ambayo ulini-quote ni ndefu vile vile! Kama huwezi kusoma posts ndefu, acha kuni-quote kwa sababu sijakjuita wala kuku-mention popote! Laptop ya kwangu, vidole vya kwangu kwahiyo usinipangie!

Hilo moja lakini pili, unaboa! Unaboa kwa sababu huelewi! Lakini nasisitiza, ACHA USHAMBA! Watu wanachapia hata lugha yao ya asili, seuze lugha ya kigeni! Non-Swahili Speakers wakiongea Kiswahili wanakivurunda kweli kweli lakini inaonekana poa tu, tena wengine wanafurahi! Kwanini? Kwa sababu wengi wa hawa wanaoongea Kiswahili kibovu wana ngozi nyeupe!! Lakini Mswahili akishindwa kuongea Kiingereza kizuri, kwenu inakuwa nongwa! Acheni ushamba!

Halafu hivi unafahamu tafsiri ya maneno "kuonea fahari?"
 
Nasisitiza kumiliki bando sijui computer sijui nini hakuhalalishi kukukosoa kama ulichoandik ni pumba na hili ni jukwaa huru umechangia ikitegemea like na dislikes,Sasa ukipata changamoto ya kukosolewa vumilia na sitoacha ukiandika pumba
Mshamba ni wewe unaelazimisha lugha usiyoielewa huku unataka uonekane unaijua,huwezi komaa na lugha unayoimudu badala ya kutia aibu kama fulani unayemtetea hapa,umeanza kupotea kwenye reli,rudi kwenye hoja acha kupanic
 
Hapa kiswahili tu ukitaka kiingereza mtafute muingereza muongee naye
Lugha yetu nzuri sana
Sana mzee magu kiswahili hadi kifo
 
Umesema kitaani. Sasa hujui tofauti ya kitaa na kiofisi? Wao walishindwa nini kumuuliza kwa kiingereza? wamejaribu wakaona hawajajibiwa?

Yaani nyie ni vituko, mnajifanya wajuaji lakini hamnaga.... sijaona pahala ambapo mwandishi anazuia asiulize swali kwa lugha ya kwao. Ushamba umewajaa tu. Kuna app siku izi zina translate kwa njia ya voice. Mpo nyuma kimaendeleo na kimatumizi ya brain. Poleni Mkuu
 

Ongeza uwezo wako kifikira, hapo nimekupa mfano wa kitaani ili kuileta kwenye level yako ya uelewa.
Ulitegemea waulize maswali kwa kingereza ilhali hotuba yenyewe hawajaielewa maana imesomwa kwa kilugha cha mgeni aliyekuja. Kawaida mtu huandaa maswali kwa kuhoji alichokielewa kwenye hotuba.

Masuala ya app usilete humu, huwa bora kwa lugha zilizokamilika na kueleweka, utafsiri wa kiswahili kwa kutumia automated process huwa majanga, maneno hayaendani kabisa, usiongee vitu kisa umeviskia kijiweni, jaribu kujiongeza kifikira.
 
Umeonesha uwezo wako wa kufikiria sio kwamba umeonesha uwezo wangu. Umetoa mfano ambao hauendani kabisa. Unafananisha maskani na ofisi? kisha unajiona unafikra pana, wacha utani.

Inabidi Waandishi wa habari huwa hawana maswali mpaka rais asome hutuba tu? Hao sio waandishi wa habari na hawajui wakifanyacho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…