Hiyo ndo kazi mnaweza kuandamana kwa comments mitandaoni ila mtaani hakuna Nyumbu atakaetokea.
Wewe jiridhishe tu na hizo fikra zako. Kwani mapinduzi ya Urusi mwaka 1917 yalikuwaje?
Lumpen Proletariats (walala hoi wa huko) waliingia barabarani, wakamwangusha Tsar Nicholas ambaye chama chake kilikuwa kimetawala kwa karne nyingi. Vuguvugu la mapinduzi lilikomaa mwezi Februari 1917, kutokana na ugumu wa maisha uliosababishwa hasa na vita vikuu vya dunia vya kwanza. Kiongozi mkuu wa mapinduzi alikuwa Vladimir Lenin, akishirikiana na watu kama Rasputin wa Siberia. Tarehe 24-25 Oktoba 1917 walala hoi hao, na baadhi ya wanajeshi, wakasema liwalo na liwe. Wito kwa waandamanaji ulikuwa "huna cho chote cha kupoteza mbali na pingu wanazokufungia". Ni kweli watu walikufa, lakini mapinduzi yalifanyika, bila ya mlala hoi kuwa na silaha za ajabu ukiacha kilio chake cha unyonge.
Hapa kwetu mambo ya leo yanafanana na Urusi ya wakati huo.
1. Chama tawala cha Urusi kilikuwa madarakani kwa karne nyingi. CCM (kikitanguliwa na TANU/ASP) kimekuwa madarakani tangu uhuru.
2. Walala hoi wa Urusi walikuwa wakilalamikia ugumu wa maisha, wakati watawala wanaponda mali. Hapa Tanzania mwananchi wa kawaida analalamika ugumu wa maisha wakati wanaonyeshwa watoto wa Rais wakiendesha magari (siyo moja tu) ya kifahari na kuchezea maburunkutu ya noti, kama vile wakisema raha ipi inashinda maisha ya Tanzania? Hapo hapo mlala hoi huyo anaongezewa kodi na tozo zisizokuwa na mantiki yo yote. Aidha, Rais anasema mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake. Anawatahadharisha watu wake kwamba anajua wanakula lakini wasizidishe mno.
3. Mlala hoi akilalamikia upungufu wa mabasi ya Mwendo Kasi, CCM wanafunga barabara na kuonyesha msululu mrefu wa mabasi yao ya kijani yakipita mtaani matupu wakati watoto wa shule wa walala hoi wanakaa kituo cha Mwendo Kasi mpaka saa 2 usiku wakisubiri usafiri. Vivyo hivyo na wasafiri wa kawaida. Hicho kikazaa vurugu kwenye vituo vya Mwendo Kasi huko Kimara na Mbagala.
4. Mapinduzi ya Urusi yalifanyika tarehe 24-25 Oktoba 1917, baada ya moshi kuanza kufukuta tangu Februari ya mwaka huo. Hapa Tanzania vuguvugu la maandamano limeanza kitambo na kumefanyika vurugu kwenye vituo vya Mwendo Kasi huko Kimara na Mbagala; na pia kwa wafanya biashara kwenye soko la Kariakoo. Tarehe 29 Oktoba inatajwa kuwa siku ya maandamano, ikiwa tofauti ya chini ya wiki moja kutoka tarehe 24-25 Oktoba ya mapinduzi ya Urusi.
5. Kila kiongozi wa Tanzania akizungumza, anasema tudumishe amani nchini na kwamba sisi ni kisiwa cha amani hapa Afrika ya Mashariki. Wakati huo huo, wananchi wanazidi kutekwa na kupotezwa. Hapa tutaje mifano michache:
a). Kijana aliyekuwa na mawazo mbadala, alichoma picha ya Rais. Akafikishwa mahakamni na kupatikana na hatia. Akatozwa faini ya Sh. Milioni Tano ambazo zililipwa na yeye akaachiwa huru. Hapo ndipo kungekuwa mwisho wa shauri hilo kwenye nchi ya utawala wa sheria. Lakini polisi walimteka siku chache baada ya kuachiwa na hadi leo hajulikani alipo.
b). Sativa alitekwa DSM akasafirishwa hadi Arusha na baadaye Katavi ambako aliachwa maporini akidhaniwa amekufa baada ya kupigwa risasi ya kichwa. Mungu si Athumani, jamaa akapona. Kwa kugelesha, Rais aliunda tume ya uchunguzi na akatoa na hela kidogo za matibabu. Hadi kesho hakuna ripoti ya uchunguzi, mbali na kwamba majeruhi alitaja hata baadhi ya polisi waliohusika, akiwemo Mafwele.
c). Basi la kwenda Tanga lilisimamishwa na Ally Kibao akatolewa nje ya basi hilo. Kesho yake maiti yake ikapatikana ikiwa na majeruhi mengi. Rais alitoa mchango wa rambirambi na akasema "kifo ni kifo tu". Hadi leo, hakuna cha uchunguzi wala nini kilichofanyika.
d). Mdude alivunjiwa mlango huko Mbeya usiku wa manane na kuchukuliwa. Hadi leo haijulikani alipo. Polisi wanasema wanafanya uchunguzi.
e). Humphrey Polepole amevunjiwa mlango usiku wa manane na kuchukuliwa, nyumba aliyokuwemo ikiwa imetapakaa damu. Polisi wanasema wanaendelea na uchunguzi.
f). Watu walipodiriki kuomba nchi iendeshwe kwa mujibu wa Katiba, Rais alijibu kwamba "Katiba ni kijitabu tu". Ulimi unaweza kuteleza ukasema vitu ambavyo hukutarajia; lakini kuteleza kwa kiwango hicho kwa Rais si kitu cha kawaida.
Hapa ndipo tulipofika Tanzania. Polisi wanawaona wananchi kama mazuzu au watoto wadogo wa kuwaambia watulie wakati wao wanafanya upelelezi. Likitokea la kutokea, sijui nani atalaumiwa.