Watanzania kushangilia kuangushwa kwa Makonda katika kura za maoni Jimbo la Kigamboni kunaashiria nini?

Anaweza kubebwa huyo ,msikilizeni Mkuu wakaya
 
Attachments

  • Nafasi ya Makonda.mp4
    3.3 MB
Anaweza kubebwa huyo ,msikilizeni Mkuu wakaya
Bado haitabadilisha kuwa wanaccm wa Kigamboni walifanya maamuzi ya kumkataa Makonda, katika kikao chao cha mapendekezo
 
Kuangushwa katika kura za maoni za CCM, katika jimbo la Kigamboni, kwa Paul Makonda na Faustine Ndugulile, kumepokelewa kwa shangwe kubwa sana na watanzania wa nchi nzima

Hivi hali hiyo inaweza ikawa inaashiria nini?

Hivi inawezekanaje kwa mkuu wa mkoa, ambaye mara kwa Mara amekuwa akisifiwa hadharani na Rais Magufuli aliyemteua na kumtaja kuwa ndiye mkuu wa mkoa bora kabisa hapa nchini na wakuu wa mikoa wengine, wanapaswa waige mfano wa uchapaji kazi wa huyo Paul Makonda, wanaccm wa Kigamboni waamue kumnyima kura?

Licha ya malalamiko mengi sana ya wananchi kuwa Mkuu huyo wa mkoa hafai na kumwomba Rais Magufuli atengue uteuzi wake................

Hata hivyo Rais Magufuli amekuwa akiweka pamba masikioni na kutotaka kabisa kusikiliza maoni hayo ya wananchi, hadi wakati fulani aliwahi sikika Rais Magufuli akimwambia Mkuu huyo wa mkoa aendelee kuchapa kazi na asisikilize hizo shutuma zinazotolewa na wananchi walio wengi na akaendelea kumsifia kuwa yeye Makonda ndiye RC bora kabisa hapa nchini, ambapo maRC wengine wanapaswa wamuige yeye Makonda kwa.uchapaji kazi wake!

Je ni kiburi hicho alichopewa na Mheshimiwa Rais, ndicho kilichompa kichwa hadi kuwadharau watanzania wote hadi wakuu wake wa kazi?

Bila shaka wananchi bado hawajasahau lile sakata la namna mkuu huyo wa mkoa, Paul Makonda, alivyoweza kutunushiana "msuli" na waziri wa Fedha, Mheshimiwa Philipo Mpango, kuhusu yale makontena yake ya "fanicha" aliyotaka kuyaingiiza nchini bila ya kuyalipia ushuru, hadi pale Mheshimiwa Rais alipoingilia kati na "kumwamuru" mkuu hiyo wa mkoa ayalipie ushuru stahiki makontena hayo

Kutokana na kiburi chake kilichopitiliza wananchi walifikia hatua ya kumbatiza cheo kisichokuwepo cha "Naibu Rais" wa Tanzania!

Hata hivyo wananchi wote wa nchi nzima, hatuna budi kuwapa pongezi wajumbe wa mkutano wa kutoa mapendekezo kwa Jimbo la Kigamboni kwa kufanya kazi iliyotukuka ya "kulikata" jina la Paul Makonda!

Ni matumaini ya wananchi wote kuwa kwenye vikao vilivyosalia vya juu zaidi vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, vitatia "tiki" uamuzi wa wanakigamboni na kutolirejesha jina la Paul Makonda kuwa ndiye mpeperusha bendera za ubunge kwa tiketi ya CCM na kuunga mkono mapendekezo yaliyotolewa na wanaccm wa Kigamboni kuwa Faustine Ndugulile ndiye apeperushe bendera ya CCM kugombea ubunge huo baadaye mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hapa nchini

Mungu ibariki Tanzania

Mlikuwa mnasema ni mabeberu wanamchukia sasa mtasema nini??
 
Yaaan furaha haielezeki niliyonayo, tangu nmezaliwa sijawahi hata kunywa soda maan nna allergy na vinywaji vya viwandani,
Lakini leo nimedufua heinken nzima. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],
jamani sijui wajumbe wa CCM Kigamboni niwape zawadi gani wallah
Utakuwaje akirejeshwa na vikao vya juu?
 
Kura za maoni zisikupumbaze mimi naamini Makonda ndio mkuu wa mkoa bora kabisa kuwahi kutokea, ni kiongozi mwenye uthubutu na mwenye maono na anayependa kujaribu. Naamini kama Makonda akifanikiwa kuingia kwenye baraza la mawaziri na akapewa wizara ya kilimo ambayo imeajiri watu wengi basi kutakuwa na mapinduzi makubwa sana ya kilimo wakulima watanufaika sana

Nilichokigundua mimi ni kwamba kuna nguvu kubwa sana ya media hasa mitandao ya kijamii inatumika kuaminisha uma kuwa Makonda ni kiongozi mbaya, na hii ni kutokana na ujasiri wake uliochangia kuokoa vijana wengi wa Tanzania waliokuwa wakiteketea, sasa wanufaika wote wakahakikisha wanaelekeza nguvu zao kuhakikisha wanamchafua. Kiongozi mzuri hawezi pimwa kwa wingi wa kura pekee yawezekana wale wajumbe waliopiga kura za maoni wakawa sio wafuasi wake, lakini ikumbukwe wananchi hawapigi kura kwa kuangalia ufuasi, wao huangalia ni kipi kiongozi alichowafanyia au atachowafanyia, na kama hivi ndivyo ilivyo naamini Makonda anaweza shinda jimbo lolote lile ndani ya Tanzania kutokana na kazi kubwa aliyoifanya ya kuokoa kizazi chetu hasa vijana . Ni binadamu wachache sana wenye uthubutu hapa duniani na hawa huwa ni tunu.
Nitajie kazi tatu tu alizofanya huyo basha wako zaidi ya kuua watu
Dark imekua chafu
Kila alichopanga kafeli
Amebebwa kwakua msukuma tuuu
 
Dada uwe na adabu basi huku huwa tunabishana kwa hoja sasa lugha chafu za nini huk sio fb.
 
mimi naamini Makonda ndio mkuu wa mkoa bora kabisa kuwahi kutokea, ni kiongozi mwenye uthubutu na mwenye maono na anayependa kujaribu.
Mkuu wa mkoa bora kuwahi kutokea ? Dogo ulishawahi kumsikia Nsa Kaisi ? Au ulishawahi kumsikia Lawrence Gama ?
Acha kutuandikia upuuzi apa eti Makonda ndiyo mkuu wa mkoa bora . . ni bora kwako ila kwa kipimo cha hao wazee niliowataja hapo juu hajakanyaga kabisa. Ungetutajia RC Mtaka angalau ningekuelewa kidogo.
Hivi unajua mkuu wa mkoa bora anafananaje ? Shenzi kabisa. Kama hujui nyamaza
 
Kigezo kinachotumika kwenye serikali hii ya awamu ya tano, unaonekana bora pale tu unapowakomoa wapinzani, kwa kuwabambikia kesi, kuwateka raia wasio na hatia na kuwanyima raia wako haki yao ya kuishi.

Sijui kama huyo Bashite ana sifa nyingine zaidi ya hizo
 
Kuangushwa katika kura za maoni za CCM, katika jimbo la Kigamboni, kwa Paul Makonda na Faustine Ndugulile, kumepokelewa kwa shangwe kubwa sana na watanzania wa nchi nzima

Hivi hali hiyo inaweza ikawa inaashiria nini?

Hivi inawezekanaje kwa mkuu wa mkoa, ambaye mara kwa Mara amekuwa akisifiwa hadharani na Rais Magufuli aliyemteua na kumtaja kuwa ndiye mkuu wa mkoa bora kabisa hapa nchini na wakuu wa mikoa wengine, wanapaswa waige mfano wa uchapaji kazi wa huyo Paul Makonda, wanaccm wa Kigamboni waamue kumnyima kura?

Licha ya malalamiko mengi sana ya wananchi kuwa Mkuu huyo wa mkoa hafai na kumwomba Rais Magufuli atengue uteuzi wake................

Hata hivyo Rais Magufuli amekuwa akiweka pamba masikioni na kutotaka kabisa kusikiliza maoni hayo ya wananchi, hadi wakati fulani aliwahi sikika Rais Magufuli akimwambia Mkuu huyo wa mkoa aendelee kuchapa kazi na asisikilize hizo shutuma zinazotolewa na wananchi walio wengi na akaendelea kumsifia kuwa yeye Makonda ndiye RC bora kabisa hapa nchini, ambapo maRC wengine wanapaswa wamuige yeye Makonda kwa.uchapaji kazi wake!

Je ni kiburi hicho alichopewa na Mheshimiwa Rais, ndicho kilichompa kichwa hadi kuwadharau watanzania wote hadi wakuu wake wa kazi?

Bila shaka wananchi bado hawajasahau lile sakata la namna mkuu huyo wa mkoa, Paul Makonda, alivyoweza kutunushiana "msuli" na waziri wa Fedha, Mheshimiwa Philipo Mpango, kuhusu yale makontena yake ya "fanicha" aliyotaka kuyaingiiza nchini bila ya kuyalipia ushuru, hadi pale Mheshimiwa Rais alipoingilia kati na "kumwamuru" mkuu hiyo wa mkoa ayalipie ushuru stahiki makontena hayo

Kutokana na kiburi chake kilichopitiliza wananchi walifikia hatua ya kumbatiza cheo kisichokuwepo cha "Naibu Rais" wa Tanzania!

Hata hivyo wananchi wote wa nchi nzima, hatuna budi kuwapa pongezi wajumbe wa mkutano wa kutoa mapendekezo kwa Jimbo la Kigamboni kwa kufanya kazi iliyotukuka ya "kulikata" jina la Paul Makonda!

Ni matumaini ya wananchi wote kuwa kwenye vikao vilivyosalia vya juu zaidi vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, vitatia "tiki" uamuzi wa wanakigamboni na kutolirejesha jina la Paul Makonda kuwa ndiye mpeperusha bendera za ubunge kwa tiketi ya CCM na kuunga mkono mapendekezo yaliyotolewa na wanaccm wa Kigamboni kuwa Faustine Ndugulile ndiye apeperushe bendera ya CCM kugombea ubunge huo baadaye mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hapa nchini

Mungu ibariki Tanzania
Kunaashiria hawakubaliani na aliyemteua
 
UTABIRI: Makonda anaandaliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma ili kuongeza kasi ya ujenzi wa mji huo. Hii yote ni kutokana na uwezo wake wa kusimamia mambo kwa kasi kwa kuwa Magufuli ana hamu ya kuona kwamba kabla hajondoka madarakani Dodoma inakuwa na sura halisi ya makao makuu ya nchi. Jambo ambalo litamjengea historia kubwa.
 
Back
Top Bottom