Watanzania kushangilia kuangushwa kwa Makonda katika kura za maoni Jimbo la Kigamboni kunaashiria nini?

Watanzania kushangilia kuangushwa kwa Makonda katika kura za maoni Jimbo la Kigamboni kunaashiria nini?

Uzima ya waliofanyika kwa mfano wa Mungu unamlilia kwa uchungu.

Mateso na vyote waliyowafanyia naye laana ile i juu ya yule awaapuuzae waja wa mwenyezi Mungu.

Amani yao huchanua kama ua na kunyauka kama jani la nyika.

Waliomsulubu watasitawahi kama mti ukiyopandwa kwenye chemchem ya maji matamu na kuishi milele kama mlima Kilimanjaro.

Sauti hii ya wananchi ni sauti ya aliyewaumba.

Asubuhi njema!
Amina
 
cocastic
Duh...........

Inaelekea kukatwa kwa jina hilo la Makonda, kumekupa furaha isiyo kifani 😁 😆
Kwani makonda amekatwa? Mkutano mkuu wa jimbo au wilaya unapitisha majina matatu ambayo yanajadiliwa na kamati ya siasa ya wilaya, mkoa na Nec wanapitisha jina moja. Unafurahi kwani mchakato umeisha? Kufikiri kwa kutumia makamasi ni tatizo kubwa sana. Kwa nini usisubiri mchakato uishe? Sababu kuwa namba moja sio kupita.
 
Kwa hiyo makamanda wahuzunike kwa kua shxxroga katumbuliwa?!
Na apeleke maniniliu yake mabwaku huko.
Kibur mwisho wake ni fedheha.
Kwa hiyo clouds wahuzunike?
 
Siyo "ku-influence" bali nimetoa rai kwa vikao vya juu viheshimu maamuzi yaliyofanywa na kikao cha mapendekezo cha wanaccm wa jimbo la Kigamboni

Wewe CCM???😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
JPM aliwaambia kabisa kuwa wa kwanza sio kupitishwa

Unabaki unapagawa na maisha ya mwanaume mwenzako kufeli

Una akili kweli?

Kama hapendwi? Kwa nn hakupata zero????
 
Wewe mtoa mada nafikiri kichwani hauko vizuri. Kwani makonda amekatwa? Mkutano mkuu wa jimbo au wilaya unapitisha majina matatu ambayo yanajadiliwa na kamati ya siasa ya wilaya, mkoa na Nec wanapitisha jina moja. Unafurahi kwani mchakato umeisha? Kufikiri kwa kutumia makamasi ni tatizo kubwa sana. Kwa nini usisubiri mchakato uishe? Sababu kuw namba moja sio kupita.
chagu wa malunde
Mbona umepanick sana?

Wewe ndiyo ulikuwa Campaign Manager wa Bashite?

Kwa hiyo umesikitishwa kwa kuona "ulaji" ndiyo umefika mwisho!
 
chagu wa malunde
Mbona umepanick sana?

Wewe ndiyo ulikuwa Campaign Manager wa Bashite?

Kwa hiyo umesikitishwa kwa kuona "ulaji" ndiyo umefika mwisho!

Wewe ndio umechemka unajadili na kuongea kama mass

Wakati unajua kabisa hata mshindi wa tatu anaweza kusimamishwa

Wanasiasa wanapenda watu kama wewe,

Ndugulile ashaondoka kuwa chagua la mkuu, kumbuka hilo
 
Mkuu yani mpaka umepata akili za kujiunga na jamii forum, forum ya watu smart kichwani bado tu hujui msemo uitwao "Siku zote mti wenye Matunda ndo hupigwa mawe"
 
Jamani tuelewane

Makonda hata akipitishwa asubuhi hii na kamati bado haiondoi furaha yetu ya yeye kutokushinda kwenye kura za Jana.

Kuanzia Jana na kuendelea lolote litalotokea iwe jina lake kuteuliwa kuwania ubunge au kuja kuwa mbunge wa kuteuliwa ni sawa na ANABEBWA TU

Makonda achukue matokeo ya Jana Kama funzo, ajijue kwamba yeye si muhimu kiasi alichojifikiria wala Hana ushawishi mkubwa aliojiwekea kichwani kuwa anao.

Ajitafakari kwanini watu wengi wamefurahia anguko lake japo tunajua kwenye maisha binadamu huwezi kukosa maadui na wasiopenda mafanikio ya mtu, aangalie mbona kwake waliofurahi ni wengi zaidi.

Makonda ajifunze kuishi vizuri na watu na ubabe auweke kando

Ana mazuri mengi Sana kayafanya, Ila mabaya makubwa machache mno yaliyojaa kebehi, ubabe na majivuno ndio yamemfikisha hapo.

Amevuna alichopanda.
 
Kuangushwa katika kura za maoni za CCM, katika jimbo la Kigamboni, kwa Paul Makonda na Faustine Ndugulile, kumepokelewa kwa shangwe kubwa sana na watanzania wa nchi nzima

Hivi hali hiyo inaweza ikawa inaashiria nini?

Hivi inawezekanaje kwa mkuu wa mkoa, ambaye mara kwa Mara amekuwa akisifiwa hadharani na Rais Magufuli aliyemteua na kumtaja kuwa ndiye mkuu wa mkoa bora kabisa hapa nchini na wakuu wa mikoa wengine, wanapaswa waige mfano wa uchapaji kazi wa huyo Paul Makonda, wanaccm wa Kigamboni waamue kumnyima kura?

Licha ya malalamiko mengi sana ya wananchi kuwa Mkuu huyo wa mkoa hafai na kumwomba Rais Magufuli atengue uteuzi wake................

Hata hivyo Rais Magufuli amekuwa akiweka pamba masikioni na kutotaka kabisa kusikiliza maoni hayo ya wananchi, hadi wakati fulani aliwahi sikika Rais Magufuli akimwambia Mkuu huyo wa mkoa aendelee kuchapa kazi na asisikilize hizo shutuma zinazotolewa na wananchi walio wengi na akaendelea kumsifia kuwa yeye Makonda ndiye RC bora kabisa hapa nchini, ambapo maRC wengine wanapaswa wamuige yeye Makonda kwa.uchapaji kazi wake!

Je ni kiburi hicho alichopewa na Mheshimiwa Rais, ndicho kilichompa kichwa hadi kuwadharau watanzania wote hadi wakuu wake wa kazi?

Bila shaka wananchi bado hawajasahau lile sakata la namna mkuu huyo wa mkoa, Paul Makonda, alivyoweza kutunushiana "msuli" na waziri wa Fedha, Mheshimiwa Philipo Mpango, kuhusu yale makontena yake ya "fanicha" aliyotaka kuyaingiiza nchini bila ya kuyalipia ushuru, hadi pale Mheshimiwa Rais alipoingilia kati na "kumwamuru" mkuu hiyo wa mkoa ayalipie ushuru stahiki makontena hayo

Kutokana na kiburi chake kilichopitiliza wananchi walifikia hatua ya kumbatiza cheo kisichokuwepo cha "Naibu Rais" wa Tanzania!

Hata hivyo wananchi wote wa nchi nzima, hatuna budi kuwapa pongezi wajumbe wa mkutano wa kutoa mapendekezo kwa Jimbo la Kigamboni kwa kufanya kazi iliyotukuka ya "kulikata" jina la Paul Makonda!

Ni matumaini ya wananchi wote kuwa kwenye vikao vilivyosalia vya juu zaidi vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, vitatia "tiki" uamuzi wa wanakigamboni na kutolirejesha jina la Paul Makonda kuwa ndiye mpeperusha bendera za ubunge kwa tiketi ya CCM na kuunga mkono mapendekezo yaliyotolewa na wanaccm wa Kigamboni kuwa Faustine Ndugulile ndiye apeperushe bendera ya CCM kugombea ubunge huo baadaye mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hapa nchini

Mungu ibariki Tanzania
Huyo akikatwa CCM ataenda kugombea UDP [emoji125][emoji88][emoji88][emoji88][emoji88][emoji88]

Sent from my XT1097 using JamiiForums mobile app
 
chagu wa malunde
Mbona umepanick sana?

Wewe ndiyo ulikuwa Campaign Manager wa Bashite?

Kwa hiyo umesikitishwa kwa kuona "ulaji" ndiyo umefika mwisho!
Wala sio kampeni meneja wala sipendelei mtu. Ila nazungumzia utaratibu wa kupata jina moja bado unaendelea. Na haijulikaani nani atapitishwa huko mbele mbona nyie mnaanza kufurahia upuuzi na Makonda ameingia kwenye mchujo wa majina matatu.
 
Siyo "ku-influence" bali nimetoa rai kwa vikao vya juu viheshimu maamuzi yaliyofanywa na kikao cha mapendekezo cha wanaccm wa jimbo la Kigamboni
Hicho kikao hakina vitendea kazi muhimu. Kinaweza hata kupendekeza watu wasio na ufahamu kwani hakina vitendea kazi (taarifa muhimu za mgombea)
 
Hivi yawezekana rafiki yako wa karibu akachukiwa halafu wewe upendwe wakati matendo yenu yanafanana?
 
Jamani tuelewane

Makonda hata akipitishwa asubuhi hii na kamati bado haiondoi furaha yetu ya yeye kutokushinda kwenye kura za Jana.

Kuanzia Jana na kuendelea lolote litalotokea iwe jina lake kuteuliwa kuwania ubunge au kuja kuwa mbunge wa kuteuliwa ni sawa na ANABEBWA TU

Makonda achukue matokeo ya Jana Kama funzo, ajijue kwamba yeye si muhimu kiasi alichojifikiria wala Hana ushawishi mkubwa aliojiwekea kichwani kuwa anao.

Ajitafakari kwanini watu wengi wamefurahia anguko lake japo tunajua kwenye maisha binadamu huwezi kukosa maadui na wasiopenda mafanikio ya mtu, aangalie mbona kwake waliofurahi ni wengi zaidi.

Makonda ajifunze kuishi vizuri na watu na ubabe auweke kando

Ana mazuri mengi Sana kayafanya, Ila mabaya makubwa machache mno yaliyojaa kebehi, ubabe na majivuno ndio yamemfikisha hapo.

Amevuna alichopanda.
Hilo ndiyo somo kubwa analopaswa kujifunza Makonda

Kwamba katika maisha hakuhitajiki "kujimwambafai" kupita kiasi, kwa kuwa hao hao unaowfanyia hivyo, hujui kesho ndiyo utakaokuwa unahitaji msaada wao
 
Yule Rais wa Iran Mohamed Abdinajad alimtanguliza Mungu katika utawala wake. Sasa hivi u Rais umekwisha amerudia kazi yake ya Ualimu Chuo Kikuu na ana panda treni kwenda kazini. Anasalimiama na watu kama kawaida.
Yule jamaa nilikuwa nakubali kazi yake sana toka nikiwa primary school.
 
Kwa taarifa yako kila ajaye kwa jina la mkuu atapigwa chini, rejea kauli ya Lema watu wanaugulia moyoni. Ni adhabu kwa mkuu
 
Hivi yawezekana rafiki yako wa karibu akachukiwa halafu wewe upendwe wakati matendo yenu yanafanana?
Hilo haliwezekani kamwe.............

Kwa hiyo hilo ni somo zuri sana wanalopaswa kulichikua hao akina Jiwe na Bashite
 
Back
Top Bottom