Watu wengi wamekuwa wakitilia shaka sana kwamba elimu bure mpaka form six haiwezekani! Ninajua kwa viongozi wa ccm wanaomaliza muda wao wa kutawala mwaka huu wanalijua hilo, kwamba elimu bure inawezekana. Lakini maskini watanzania wengine ambao wameshazoea kuishi katika ukandamizi na udanganyifu wa CCM wana amini haiwezekani.naomba nikupe baadhi ya mifano ya nchi za africa, tukianzia na majirani zetu Kenya wanatoa elimu ya bure! na kuna social grants nyingi tu wanazo ambazo sisi hatuna. Nchi kama Namibia pia mwanafunzi anachangia kama Tsh 2500 kwa mwaka, and all other stationery wanapewa bure, Pia wana 'social grants' nyingi sana kwa mfano wazee kuanzia miaka 60 wanapata allowances uwe una kazi usiwe nayo, Ukifa ukiwa kazini watoto na mke/mume wako wataendelea kupata your full salary mpaka utakapotimiza miaka 60. mfano umefariki ukiwa na miaka 30 serilkali itaendelea kuwalipa watoto na mke/mme kwa kipindi cha miaka 30 full salary, Angalia pia Botswana,Swaziland,Cameroon. Namibia ni nchi isiyokuwa na resource kabisa zaidi ya uranium na almas kidogo. Sisi tuna mengi. WATANZANIA WENZANGU KWA NINI UONGO WA CCM MNAUAMINI SANA KULIKO UKWELI WA DR.SLAA UNAOLETA NEEMA?