Mkuu wangu labda unajichanganya.. hakuna mahala popote Dr.Slaa na Chadema wamesema watazifunga shule za Private wala hakuna nchi inayotoa elimu bure wamefunga shule za Private ikiwa ni pamnoja na Canada. Na hata kiuchumi, nchi za Kikomunist hazikukataza mtu kuwa na biashara binafsi kabisaaa, au mtu kuwa na kitu Private kwa sababu ati Ukomunist unasema uchumi wa nchi hizo utakuwa controlled na Government..
Mkuu kabisa Bob Mkandara, naona kama kujichanganya unajichanganya wewe, naomba unielimishe kuna sehemu gani nimesema CHADEMA watafunga shule za private, hii dhana unaipata wapi?
Sii kweli hata huko zilikuwepo biashara za watu binafsi iwe elimu au Hospital na hata wakati wa Nyerere zilikuwepo shule Private nyingi zikiendesha education kama biashara lakini walilazimika kufanya vizuri zaidi ili kuwavuta wananchi toka shule za Serikali (bure). Hospitali vile vile Hindu Mandal haikuanza jana.. na ndivyo ilivyo hata hapa Canada, UK, US au nchi za Nordic zipo shule za Private isipokuwa zinakuwa na ushindani mkubwa toka shule za serikali hivyo bar ya elimu bora inakuwa raised kila ushindani unapozidi toka upande wa bure.
Elimu ya umma inaweza kutoa ushindani kwa private institutions bila kumpa nafasi milionea asome bure, tuna wasioweza kujilipia wengi tu wa kujaza system ya elimu ya umma.
Ndivyo walivyoweza kufadanikiwa wenzetu na sioo swala la Utajiri au nini tena wao ndio naweza kusema Elimu kwao ni Unachukua sehemu ndogo sana ya Bajeti kuliko mipango ya wizara nyinginezo ambapo Exploration au case study pekee inaweza chukua mabillioni ya fedha..Kwa hiyo Elimu kwao ni bure sio kwa sababu ni matajiri laa hasha kwa sababu Elimu ni RIGHT ya kila mwananchi (necessity) ktk maendeleo ya binadamu kwani ndio chanzo cha maendeleo ya nchi. Na wengine wameweka kwamba elimu ni privilege hivyo sii lazima kuwa na za bure kwa sababu wananchi wake walio wengi wanajiweza.
Nimeeleza hapo juu kuhusu rights zenye gharama na zisizo gharama. Free speech as a right is not the same as education as a right.Moja haihitaji resources, nyingine inahitaji.Tukishakuwa na kitu kinahitaji resources tu inabidi tuingie katika budget and maximum allocation of resources, hii hairuhusu kuwapa wawezao kujilipa free ride.
Leo wewe una taifa lenye wananchi wenye kipato cha average ya dollar moja kwa siku, wanashindwa hata kuweka mkate mezani unakuja watoza fedha ikifikiria kwamba unajenga?.. Na how come toka tumefanya hivyo miaka 20 iliyopitya mbona Elimu nchini ndio inazidi kuporomoka..Au kipimo cha Mtanzania ni hicho kiingereza? maanake siku hizi wazazi Bongo akimsifia mwanaye kuwa ana akili sana ni kwa sababu anazungumza kiingereza!.. Elimu Bongo imekuwa lugha ya kiingereza ambacho Ukija huku Canada au USA utachekwa na hizo chicken 'n Chips, I shall, Petrol, Spanner, Trouser na kadhalika..
Hapa ndipo Bob unajionyesha kabisa hujanifuatilia wala kunisoma kabisa, nimerudia mara elfu moja na moja humu kwamba wasiojiweza wasaidiwe, sina tatizo na hilo, ila tatizo langu kuwalipia watu wanaojiweza. Nime argue kwamba elimu bora kwa wote itawapendelea wanaojiweza at the expense of wasiojiweza, kwa sababu wanaojiweza wana option, wasiojiweza hawana option, sasa kwa nini uachie kiti cha bure kiende kwa mtu mwenye option wakati kuna mtu hana option?
Ni sawa na uwe kwenye msiba, mnaenda mazikoni, kuna watu kibao, wengine wana magari yao binafsi na wengine hawana magari yao binafsi. Halafu kunatolewa usafiri wa bure wa mabasi kuwafikisha watu makaburini, halafu atokee mtu kusema ni sawa tu kwa watu wote kupanda basi la bure, bila kujali kama wana uwezo wa kutumia magari yao binafsi au la. Hii system haitumii resources vilivyo kwani wenye magari yao binafsi ambao hawana huruma wanaweza kusema ngoja tupande gari la bure, halafu wengine ambao hawana magari binafsi wakakosa usafiri pekee uliokuwapo kwao. Hii ndiyo beef yangu, nataka hawa wenye uwezo watumie uwezo wao, wasipewe free ride tu.
Mkuu wangu, historia ya Elimu duniani nchi nyingi kama sii zote zimeanza na mfumo huu wa Elimu bure kisha baada yake ndio wameanza kuingia ktk hatua ya kulipa kwa hatua na kama sikosei hata Marekani wenyewe shule bado nyingi sana ni bure. Naweza kusema kuna shule nyingi za bure sawa au zaidi ya za kulipa (To highschool) na wamegundua kwamba hata mfumo wao wa Elimu ni mbaya sana kiasi kwamba wanashuka rank pamoja na kuwa na shule nyingi na nzuri kuliko sehemu yoyote duniani.
Na sisi tulipitia huko kwenye elimu bure, tukaona UPE ya limited resources na na demand kubwa ilivyotupa madarasa ya watu 120, mchizi anasoma mwaka mzima mwalimu wake wa darasa hamjui hata jina. Matatizo yetu ya kielimu ya sasa yamerithi mengi kutoka mfumo huu, kwa nini tunataka kudekeza mambo yaliyopitwa na wakati ? Hususan kama tuna njia ya kupunguza makali ya pressure ya demand kwenye hii system ?
Hapa nikiwa na maana hata hizo nchi zilizoendelea wanazo shule za bure kwa sababu hakuna taifa lolote ambalo tayari limeondoa tabaka za wananchi wake..Elimu sio swala la matabaka ila ni RIGHT ya kila mwananchi hivyo uwe tajiri au maskini haijalishi kipato kama kwenda choo vile. Mkuu wangu it's only less than 10% ndio matajiri wanao control uchumi wa nchi zetu iwe hiyo Marekani, Uingereza, Japan na kokote uendako utakuwa wanao control uchumi hawajai mkononi na Utajiri wa hawa watu unategemea Uzalishaji na Consumers ambao wote wanahitaji elimu kuwezesha..Kumbuka tu kwamba human development inaanza na elimu, hata dini zetu zimetusisitiza hivyo laa sivyo tungekuwa bado tunaamini Mitunga..
Tangu juu umeonekana hukunielewa, sina tatizo na shule za bure, tatizo langu ni eligibility ya kukubalika katika shule hizi. Sikubali mtu mwenye uwezo aende kusoma shule ya bure. Kama elimu ni right, jua pia kwamba inalipiwa na ujue namna bora kabisa ya kuilipia.
Mkuu wangu Tanzania Matajitri hawafiki hata asilimia 1 ya population na hiyo middle class ni chini ya asilimia 10 wakati una maskini wasikipungua asilimia 80. Rais wako mwenyewe amnakataa kuongeza mshahara kufikia Tsh 315,000 kwa mwaka ambazo ni sawa na Dollar 300 (less than), leo unategemea mtu anayepokea Mshahara wa Tsh 120, 000 kwa mwaka kulipia ada ya mtoto au watoto wake inayodzidi Tsh. 50,000? Hii akili kweli mkuu wangu.
Hata kama angekuwa tajiri mmoja tu, jifikirie wewe ndiye maskini ambaye unakosa kusoma kwa sababu tajiri mmoja kachukua nafasi yako, utaona sawa hilo ?
Haya ni kiasi gani basdi tunachozungumzia? Ikiwa leo serikali inamtoza mtoto mmoja Tsh 50,000 hadi 100,000 hizi zinaleta tofauti gani ktk uwezo wa serikali ambayo tunaambiwa inakusanya kodi toka kwa wateja wasiozidi millioni 2!.
Inabidi tujenge utamaduni wa matumizi mazuri ya fedha hata kama ni shilingi moja tu, haba na haba hujaza kibaba waswahili walisema.
Wewee mwenyewe unaona misamaha ya kodi mahotel yanajengwa na kila baada ya miaka mitano ownership inabadilishwa kwa kuwezeshwa na serikali iliyopo. Tender ya bomba la mafuta toka Dar hadi Mwanza wanachukua wao hapa utategemea kodi gani kukusanywa! Haya majuzi tu umeona mkataba wa Umeme toka Millenium unarudi kupewa shirika la kwao badala ya Tanesco, halafu mtakuja sema hata Tanesco haiwezekani.Wala sintashangaa kama ile mitambo ya Dowans inafanya kazi leo na kulipwa mabillioni ya fedha.. Tazama mikataba feki mkuu wangu bado unaweza sema ati sisi ni maskini wakati tunaweza kujenga banki Kuu kwa gharama inayozidi Usd 500, millioni.. twintower zisizozidi ghorofa 20 each. hatufahamu mishahara wala posho za viongozi ni siri kweli hii nchi mkuu wangu... aaah niache miye nisije fika kusikotakiwa...
Two wrongs do not make a right, misamaha ya kodi holela ni mibaya, tuipinge, tusitake kuihalalisha zaidi kwa kuleta mfumo usio na mahesabu ya kiuchumi, tutakuwa tunaongeza tatizo, sio kutatua tatizo