Wakuu,
Katika kuichambua hoja hii ya Elimu bure darasa la kwanza hadi Formsix nimejaribu kutoa mchanganuo ufuatao. Analysis based on matokeo ya kidato cha nne 2009 yaliyotangazwa Feb.2010
Elimu ya O-Level
1.Wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na kufanya mtihani (Shule za serikali + shule za binafsi) =351,152
2.Tu assume wale wa shule binafsi ni 20% ya wanafunzi wote:
Kwa hiyo wale wa shule za serikali = [351,152-(351,152 x 0.2)] = 280922
3.Tumepata wanafunzi wa shule za umma waliomaliza kidato cha nne mwaka jana ni 280922
4.Tu assume tena kuwa katika intake hii ya hawa waliofika kidato cha nne wako ambao waliishia njiani, tuseme 15% hawakufika hapo, kwa hiyo hao 280922 ni 85% ya wanafunzi wote. Ukipiga mahesabu utapata kuwa wanafunzi wote walipaswa kuwa 330496, hawa ni wanafunzi wa kidato kimoja tuseme cha nne.
5.Kwa hiyo kupata wastani wa wanafunzi wote wa kidato cha I-IV, tunazidisha hiyo figure kwa nne. 330496 x 4 =1,321,984.
6. Tuassume tena kuwa kati ya hao wanafunzi wote, 30% ni wa boarding na 70% ni wa shule za kutwa. Wale wa shule za kutwa ada ni sh.20,000/= na wale wa boarding ada ni sh.70,000/=
7. 30% ambayo ni wanafunzi wa bweni ni sawa na (0.3 x 1,321,984= 396,595) kwa hiyo wale wa kutwa ambao ni 70% watakuwa (1,321,984 396595 =925,389)
Gharama za kuwalipia wanafunzi wote kwa mwaka:
Wale wa shule za kutwa = 925389 x sh.20,000/- = 18,507,780,000 (Billion 18.6)
Wale wa shule za bweni =396595 x sh.70,000/- =27,761,650,000 (Billioni 27.6)
PART B: Wanafunzi wa A Level
1. Kwa matokeo hayo ya 2009 waliofaulu kwa division I-III walikuwa 42,672 . Tuassume wote watachaguliwa kwenda Alevel shule za boarding za serikali. Hivyo tungekuwa na wanafunzi wa kidato cha Tano 42,672 na kidato cha sita watakuwa idadi hiyo hiyo. Kwa hiyo jumla ya wanafunzi wote wa kidato cha Tano na sita watakuwa (42,672 x 2 = 85344)
2. Gharama ya kuwalipia hawa wote itakuwa Tsh.70,000/- x 85344 = 5,974,080,000 (Billion 6)
My take:
Jumla ya gharama zote zitatakiwa Billion 52.2 kwa mwaka kugharamia ada za wanafunzi kutoka kidato cha kwanza hadi cha sita. Sijaweka za primary kwani elimu hiyo ni ya bure kwa sasa. Tukiongeza ukusanyaji wa kodi na kubana mianya ya ukwepaji wa kodi hili linawezekana, Elimu bure darasa la kwanza hadi Form SIX
NB: Pitia analysis hii then correct me if Im wrong