Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Mtoto wa mkulima hawezi kwenda Feza Academy, Kenya, Afrika ya Kusini, Uingereza wala Marekani kusoma.Kwa hiyo kimsingi akikosa nafasi hii anarudi kulima, anakosa elimu.
Mtoto wa Mr. X mwenye uwezo, hata akikosa nafasi hii ya elimu ya bure ana nafasi ya kwenda kokote kutafuta elimu, na kukosa nafasi ya kusoma bure hakutamuathiri sana.
Uzuri wa elimu ya bure kwa wote hadi ngazi ya upili ni kuwa hakuna atakayekosa nafasi ya kupata elimu angalau hadi ngazi hiyo, awe mtoto wa mkulima, kuli, msukuma mikokoteni, mbeba zege, au mfanyabiashara.
Kama unataka kuwanyonya matajiri basi wanyonye katika kodi walipazo kwenye mambo mbalimbali.