Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Mtoto wa mkulima hawezi kwenda Feza Academy, Kenya, Afrika ya Kusini, Uingereza wala Marekani kusoma.Kwa hiyo kimsingi akikosa nafasi hii anarudi kulima, anakosa elimu.
Mtoto wa Mr. X mwenye uwezo, hata akikosa nafasi hii ya elimu ya bure ana nafasi ya kwenda kokote kutafuta elimu, na kukosa nafasi ya kusoma bure hakutamuathiri sana.
Uzuri wa elimu ya bure kwa wote hadi ngazi ya upili ni kuwa hakuna atakayekosa nafasi ya kupata elimu angalau hadi ngazi hiyo, awe mtoto wa mkulima, kuli, msukuma mikokoteni, mbeba zege, au mfanyabiashara.
Kama unataka kuwanyonya matajiri basi wanyonye katika kodi walipazo kwenye mambo mbalimbali.
Mkuu mbona unarudia maneno ya Dr.Slaa? kwani kuna mtu kasema Dr.Slaa ataendeleza ya JK?.. Au chini ya Chadema ukusanyaji kodi utaendelea kama ulivyo yaani tukitegemea watu milioni 2 tu. Hivi hujamsoka vizuri Dr.Slaa kwa nini anakubalika na watu wengi tena wengi wao wakiwa wasomi kama wewe (Accountability first)..Kodi yenyewe ipi ? Hii hii ambayo serikali haina hata mfumo wa kukusanya kodi wa kutegemewa ? Hii hii yenye kazi alfu moja na moja ?
Huwezi kutatua tatizo moja kwa tatizo jingine. Na hata ukikusanya kodi hapo kuna swala zima la decentralization of our systems for more accountability.
Watu wengi wamekuwa wakitilia shaka sana kwamba elimu bure mpaka form six haiwezekani! Ninajua kwa viongozi wa ccm wanaomaliza muda wao wa kutawala mwaka huu wanalijua hilo, kwamba elimu bure inawezekana. Lakini maskini watanzania wengine ambao wameshazoea kuishi katika ukandamizi na udanganyifu wa CCM wana amini haiwezekani.naomba nikupe baadhi ya mifano ya nchi za africa, tukianzia na majirani zetu Kenya wanatoa elimu ya bure! na kuna social grants nyingi tu wanazo ambazo sisi hatuna. Nchi kama Namibia pia mwanafunzi anachangia kama Tsh 2500 kwa mwaka, and all other stationery wanapewa bure, Pia wana 'social grants' nyingi sana kwa mfano wazee kuanzia miaka 60 wanapata allowances uwe una kazi usiwe nayo, Ukifa ukiwa kazini watoto na mke/mume wako wataendelea kupata your full salary mpaka utakapotimiza miaka 60. mfano umefariki ukiwa na miaka 30 serilkali itaendelea kuwalipa watoto na mke/mme kwa kipindi cha miaka 30 full salary, Angalia pia Botswana,Swaziland,Cameroon. Namibia ni nchi isiyokuwa na resource kabisa zaidi ya uranium na almas kidogo. Sisi tuna mengi. WATANZANIA WENZANGU KWA NINI UONGO WA CCM MNAUAMINI SANA KULIKO UKWELI WA DR.SLAA UNAOLETA NEEMA?
Elimu bure shule za msingi na sekondai inawezekana kabisa. Lakini binafsi ningependa kuwe na w viongozi wabunifu na wenye mitazamo tofauti ya kufanya mambo.Hawa wa CCM mazoea yamewalemaza.
Mfano. kwa shule za serikali wanaweza kutenga shule kijiografia na kiufanisi kila mkoa.
Shule za vijijini primary na sekoday ikawa elimu bure kabisa.
Shule za mijini ambazo ziko level ya juu kukawa na gharama kidogo ya kulipa may be kwa shule za msingi kama bunge, Tsh 5,000 na shule za mjini nyinginezo elfu 2000. Shule za sekondari zilizo mijini zikapewa madaraja kukawa na na zile za kulipa 20,000 na 40,000.
Karo hizi zawanafuzi wa shule za mjini zinaweknwa kwenye mfuko wa kusadia kuinua kielimu shule na wanafunzi wa shule za vijijini ambazo zina kiwango duni.
Lakini kwa shule zote za mjini na vijijini serikali inatakiwa kuweka bajeti ya jumla kuwa kwa kila mwanafuzi aliyeandikishwa shule husika. Serikali itatoa ruzuku ya shilingi 500 kwa mwezi kwa shule za msingi na shilingi 1,000 kwa shule za sekondary.Ruzuku hizi zitatumiwa na shule kwenye mambo ya kitaaluma tu
Let say shule ya primary kijiweni ina wanafunzi 50 kila darasa na ina madarasa 7. Serikali itatakiwa kutoa ruzuku ya shilingi 175,000 kila mwezi kwa shule hii. kwa shule za sekondari may be yenye wanafuzi 200 serikali itatakiwa kutoa ruzuku ya shilingi 200,000 kila mwezi.
Yaani kifupi sio tu elimu ya bure serikali inatakiwa ilipe kila kichwa cha mwanafunzi aliyepo shule kwa shule husika. hata kama ni shilingi 500 kwa mwaka. Uwezo huo upo.
Mkuu mbona unarudia maneno ya Dr.Slaa? kwani kuna mtu kasema Dr.Slaa ataendeleza ya JK?.. Au chini ya Chadema ukusanyaji kodi utaendelea kama ulivyo yaani tukitegemea watu milioni 2 tu. Hivi hujamsoka vizuri Dr.Slaa kwa nini anakubalika na watu wengi tena wengi wao wakiwa wasomi kama wewe (Accountability first)..
The all issue hapa ni kubadilisha mfumo na tabia nzima ya uongozi kutoka kutawaliwa hadi kuongozwa. Elimu bure ina maana moja tu, nayo ni kwamba kila raia atakuwa na nafasi ya kwenda shule regardless, hata yule asiyejiweza kabisa kifedha bado ataweza kupata elimu bure hadi form 6.
Na zaidi ya hayo najua umesoma Ilani ya chama, sasa nashangaa kwa nini umechukua hili moja badala ya kutazama mabadiliko yote yanayotegemewa ili upate urahisi wa kuelewa.
Hahaha,
Nimecheka nilipoona "winning at all cost".
Kati yangu ninayetaka wenye uwezo washirikiane na serikali katika gharama za elimu, na wewe unayetaka serikali ichukue mzigo wote katika vita dhidi ya ujinga, nani anataka "winning at all cost" ?
Tuseme tuna nafasi moja ili kutolea mkazo na kulielewa vizuri swala la limited resources
Mtoto wa mkulima hawezi kwenda Feza Academy, Kenya, Afrika ya Kusini, Uingereza wala Marekani kusoma.Kwa hiyo kimsingi akikosa nafasi hii anarudi kulima, anakosa elimu.
Mtoto wa Mr. X mwenye uwezo, hata akikosa nafasi hii ya elimu ya bure ana nafasi ya kwenda kokote kutafuta elimu, na kukosa nafasi ya kusoma bure hakutamuathiri sana.
Ndiyo maana nasema nafasi hii ya bure apewe mtoto wa mkulima ambaye hana uwezo, na kama tunataka kumpa mtoto wa Mr. X mwenye uwezo, Mr. X alipishwe ada ili ada hii ama itumike kumsomesha mtoto mwingine wa mkulima asiyejiweza, au itumike katika huduma nyingine za kijamii. Hata huyo Karl Marx aliyetetea mifumo ya serikali kuchukua majukumu ya huduma za jamii alisema From each according to his ability, to each according to his need. Hata Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa ni bingwa wa kutetea elimu ya bure kwa wote mwishoni alikubali kwamba serikali maskini kutaka kumlipia kila mtu katika mtindo wa mtego uwanasao waliokusudiwa na wasiokusudiwa halikuwa jambo la busara, kwa maana ya kwamba wenye uwezo wa kujilipia na wajilipie.
Tunapenda kuamini kwamba elimu bora kwa wote italeta huduma sawa kwa wote kwenye elimu, lakini mimi naona itawanyima maskini zaidi ya itakavyowanyima matajiri.
Kodi yenyewe ipi ? Hii hii ambayo serikali haina hata mfumo wa kukusanya kodi wa kutegemewa ? Hii hii yenye kazi alfu moja na moja ?
Huwezi kutatua tatizo moja kwa tatizo jingine. Na hata ukikusanya kodi hapo kuna swala zima la decentralization of our systems for more accountability.
Hatuzungumzii ukusanyaji kodi wa serikali ya CCM mkuu, its pathetic!! Tunazungumzia posibility ya a new government ya CHADEMA yenye maono katika ukusanyaji wa mapato na kupanua wigo wa mapato, watu ambao wamekusudia kubadili katiba and therefore a completely new system of government with exquisite efficiency.
Kiranga huyo mtoto wa masikini ataikosaje hiyo nafasi ya kusoma wakati ni ya bure? Na kama issue ni kuwa mtoto wa tajiri atachukua nafasi hiyo basi hata kama huyo mtoto wa tajiri atalipia bado hiyo nafasi itakosekana.
Imebidi hapa nirudi kukujibu...
nilichoandika ni hiki:
Nadhani miaka 50 iliyopita inaanzia karne ya 20, au wewe unasema nini? Nani anataka kupotosha hapa?
Kiranga, take time mkuu, haya mambo ya winning at all cost muda mwingine yanaharibu umakini wako.
Mkuu,kwa nchi ambayo huduma sasa ziko katika hali mbaya mno, ni bora kukusanya malipo (japo kidogo) kwa wanaojiweza ili kuboresha huduma hizo hasa ikiwa nchi bado haijajipanga uzuri katika ukusanyaji wa mapato.
elimu bila ya malipo, huduma za fya bila ya malipo zitaendeshwa kwa mapato gani ikiwa bado nchi haijaweza kukusanya hata kodi kwa ufanisi?
Mkuu,
Suala hili ni utashi wa kisiasa tu.Kuna maeneo mengi ambayo ni vianzo vizuri vya mapato lakini serikali hajavitumia ipasavyo kama vile bidhaa za misitu,za bahari.madini n.k.Vilevile kupunguza matumizi ya serikali kama uanzishaji holela wa maeneo ya utawala bila vigezo vya kueleweka.