Watanzania kwa pamoja tuzilinde rasilimali zetu za nchi kwa pamoja na kwa wivu mkubwa sana

Escrowseal1

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2014
Posts
4,618
Reaction score
4,605
Afrika ni bara vulnerable sana linapokuja suala la rasilimali zake. Sababu ni kutokana na viongozi wasiokuwa na uadirifu na kutokuwa na uzarendo.

Leo nimekutana na waraka wa serikali unaoruhusu uuzwaji wa wanyamapori. kwa u vulnerable ule ule ni lazima hii iwe work up call kwani serikali ni serikali hii hii ilifanya zuio hilo. Tulishawahi kupigwa kwa kuwasafirisha Twiga wetu bila kujua wanaenda wapi.

Si ajabu kila mmoja anajua kuwa kwa sasa tushaanza kuwa Darling wa mataifa ambayo hatuna record nzuri tangu enzi za chief Mangungo mpaka leo juu ya rasilimali. No wonder huo u sweetheart na udarling ukatupofusha pakubwa.

Naomba kwa pamoja hili Tangazo la kuuza hawa viumbe wetu aliotujalia mola iwe work up call kuhakikisha kwa pamoja na kwa wivu mkubwa tusifikie kale ka hatua ka kupeleka Twiga kusikojulikana.

Ni kama mwezi tangu jabari la vito linalodhaniwa kutoka Tanzania lilionekana Dubai japo hatujapata mrejesho ulio clear kuwa linatuhusu ama la.

Kwa kuwa prevention is better than cure ,watanzania tufungue mboni zetu maana hii yaweza kuwa loop hole ya kupigwa kivingine .
 
Wanyama wakiondoka watalii watakuja kushangaa upole wa maza. It's a win-win situation.
 
Bahati mbaya mwenye kulinda ni mwenye mamlaka. Wewe na Mimi hata tukimkuta waziri anapakia twiga hatuna Cha kufanya zaidi ya kupost TU.
Kumbe bado hauna habari kuwe kelele za nitandao zina nguvu isiyomithirika. We usijali unapoona ndivyo sivyo we post kwani bahati nzuri hizi kelele zinawafikia walengwa
 
Huwezi kusema watu walale njaa, wakose madawa hospitali wakati wanyama wapo wa kuuzwa na kuingiza kipato. Utazidisha ujangili tuu maana watu watapita njia za mkato. Cha msingi ni kuhakikisha wanyama wanazalishwa vizuri na wanaongezeka kabla ya kuuzwa na kuwindwa.
 
Unalia mapema mno. Hizi ni rasharasha tu, mvua yenyewe bado.

Sijui itakapoanza kutunyeshea kikwelikweli utafanyaje?

Wanyama? Hiyo ni raslimali ndiyo, lakini zipo zitakazokuumiza roho zaidi. Vuta subira.
 
Ruhusa kwa Wafanyabishara kuendelea kuuza Wanyamapori walio hai.
 
Huwezi kusema watu walale njaa, wakose madawa hospitali wakati wanyama wapo wa kuuzwa na kuingiza kipato. Utazidisha ujangili tuu maana watu watapita njia za mkato. Cha msingi ni kuhakikisha wanyama wanazalishwa vizuri na wanaongezeka kabla ya kuuzwa na kuwindwa.
Ukishamuuzia hao wanyama unafikiri atakuja tena kutalii?? Na hivo vya kuuza vikiisha utauza nini tena??!
 
Sidhani kama wanunuzi ni wazungu. Sana sana watakuwa Wachina labda na Waarabu. Na mzungu hawezi kwenda China au Dubai kuangalia wanyama, atakuja hapa tuu.
 
Unalia mapema mno. Hizi ni rasharasha tu, mvua yenyewe bado.

Sijui itakapoanza kutunyeshea kikwelikweli utafanyaje?

Wanyama? Hiyo ni raslimali ndiyo, lakini zipo zitakazokuumiza roho zaidi. Vuta subira.
Mi nadhani itanipa heart attack maana naumia sana nikiwaza maisha wanayoishi hao wanaopelekewa rasilimali zetu kulinganisha na watu ninaowaona vijijini kwetu. Its more than pain.ila la kufanya si kukaa kimya ni kuwaonyesha hao madalali kwamba we have disagreement somewhere.
 
Sidhani kama wanunuzi ni wazungu. Sana sana watakuwa Wachina labda na Waarabu. Na mzungu hawezi kwenda China au Dubai kuangalia wanyama, atakuja hapa tuu.
Mkuu kwenye zoo za ulaya wamejaa wanyapori including Twiga kwani wanazalishwa maabara ? Ila historia ya sellout wa Tanzania connection yao ya kutulaghai ni waarabu hasa viongozi wa kariba fulani .
 
Bahati mbaya mwenye kulinda ni mwenye mamlaka. Wewe na Mimi hata tukimkuta waziri anapakia twiga hatuna Cha kufanya zaidi ya kupost TU.
Hata kupost tu ni afadhali kuliko kunyamaza kama kuna vitu vinaenda ndivyo sivyo !! Maana ukipost vitajulikana kwa watu wengi !! Na vikijulikana kwa watu wengi na mayowe yatakuwa mengi ! Itasaidia. !!!
 
Afrika ni bara vulnerable sana linapokuja suala la rasilimali zake. Sababu ni kutokana na viongozi wasiokuwa na uadirifu na kutokuwa na uzarendo.
Leo nimekutana na waraka wa serikali unaoruhusu uuzwaji wa wanyamapori. kwa u vulnerable ule ule ni lazima hii iwe work up call kwani serikali ni serikali hii hii ilifanya zuio hilo. Tulishawahi kupigwa kwa kuwasafirisha Twiga wetu bila kujua wanaenda wapi.
Si ajabu kila mmoja anajua kuwa kwa sasa tushaanza kuwa Darling wa mataifa ambayo hatuna record nzuri tangu enzi za chief Mangungo mpaka leo juu ya rasilimali. No wonder huo u sweetheart na udarling ukatupofusha pakubwa.
Naomba kwa pamoja hili Tangazo la kuuza hawa viumbe wetu aliotujalia mola iwe work up call kuhakikisha kwa pamoja na kwa wivu mkubwa tusifikie kale ka hatua ka kupeleka Twiga kusikojulikana.
Ni kama mwezi tangu jabari la vito linalodhaniwa kutoka Tanzania lilionekana Dubai japo hatujapata mrejesho ulio clear kuwa linatuhusu ama la.
Kwa kuwa prevention is better than cure ,watanzania tufungue mboni zetu maana hii yaweza kuwa loop hole ya kupigwa kivingine .
Sio "kutokana na "viongozi", kiongozi wako wa kwanza ni wewe mwenyewe. Anza kwa kujiongoza usingojee kuongozwa kama ng'ombe.
 
Wanyama wakiondoka watalii watakuja kushangaa upole wa maza. It's a win-win situation.
Win-win situation !! Haka kamsemo nakapendaga sana !!! Lakini inapokuja kuwa ni kwa ajili ya individuals tu hapo ndipo inapoleta ukakasi !!
 
Huwezi kusema watu walale njaa, wakose madawa hospitali wakati wanyama wapo wa kuuzwa na kuingiza kipato. Utazidisha ujangili tuu maana watu watapita njia za mkato. Cha msingi ni kuhakikisha wanyama wanazalishwa vizuri na wanaongezeka kabla ya kuuzwa na kuwindwa.
Hapo ni sawa na kusema kwa kuwa familia ina njaa basi
Sio "kutokana na "viongozi", kiongozi wako wa kwanza ni wewe mwenyewe. Anza kwa kujiongoza usingojee kuongozwa kama ng'ombe.
Bibie karibu tulikumiss .ila uje kwa staha maana waweza tolewa nishai bure ukarudi chimbo
 
Wtz inabidi tuchukue hatua ya kiwazuia hawa viongozi majangili.tufanya maandamano yasiyo na kikomo kupinga matendo mabaya yanayofanywa na hawa majangili.kwanza hatujawachagua.sudani wameweza,congo wanapambana kwa nini sisi tusiweze?matumizi mabayavya rasilimali sasa basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwenye zoo za ulaya wamejaa wanyapori including Twiga kwani wanazalishwa maabara ? Ila historia ya sellout wa Tanzania connection yao ya kutulaghai ni waarabu hasa viongozi wa kariba fulani .

Wanyama wa zoo huwa wanazaliwa hapo hapo au wananunuliwa kutoka zoo nyingine zenye wanyama wa ziada. Ni vitukuu vya wanyama waliochukuliwa Afrika zamani sana. Tena zoo zingine zilianzishwa enzi za ukoloni.
 
Tuna watawala ambao wana njaa ya hatari, ambayo imewajaza ubinafsi wa kiwango kisichopimika.
 
Tatizo ni kwamba mawazo yetu raia yana nguvu na kuheshimika kipindi cha kampeni za uchaguzi baada ya hapo lolote utakalo ongea utaonekana kama mwenda wazimu

Lolote wanalotaka kufanya haijalishi ni hatari kiasi gani kwa nchi yetu watafanya kwa sababu wanajua raia tumefungwa mikono na hatuwezi kuwachukulia hatua zozote za kisheria

Inabidi tupate katiba ambayo itatupa nguvu na meno raia ya kung'ata pale tutakapo ona mahali kuna shida,
bila kusahau mahakama iliyo huru inayoweza kumu wajibisha kiongozi yeyote wa serikali anapokosea, na pia Kinga walizojiwekea sasa hivi ziondolewe
 
Back
Top Bottom