Afrika ni bara vulnerable sana linapokuja suala la rasilimali zake. Sababu ni kutokana na viongozi wasiokuwa na uadirifu na kutokuwa na uzarendo.
Leo nimekutana na waraka wa serikali unaoruhusu uuzwaji wa wanyamapori. kwa u vulnerable ule ule ni lazima hii iwe work up call kwani serikali ni serikali hii hii ilifanya zuio hilo. Tulishawahi kupigwa kwa kuwasafirisha Twiga wetu bila kujua wanaenda wapi.
Si ajabu kila mmoja anajua kuwa kwa sasa tushaanza kuwa Darling wa mataifa ambayo hatuna record nzuri tangu enzi za chief Mangungo mpaka leo juu ya rasilimali. No wonder huo u sweetheart na udarling ukatupofusha pakubwa.
Naomba kwa pamoja hili Tangazo la kuuza hawa viumbe wetu aliotujalia mola iwe work up call kuhakikisha kwa pamoja na kwa wivu mkubwa tusifikie kale ka hatua ka kupeleka Twiga kusikojulikana.
Ni kama mwezi tangu jabari la vito linalodhaniwa kutoka Tanzania lilionekana Dubai japo hatujapata mrejesho ulio clear kuwa linatuhusu ama la.
Kwa kuwa prevention is better than cure ,watanzania tufungue mboni zetu maana hii yaweza kuwa loop hole ya kupigwa kivingine .