Watanzania kwa pamoja tuzilinde rasilimali zetu za nchi kwa pamoja na kwa wivu mkubwa sana

Lazima tuweke miguu chini tuwaambie hapana si lazima kuandamana ila hata kwa kuoaza sauti hivi naamini wanatusikia. Ki ukweli hii awamu inahitaji uangalizi wetu sote watanzania .hiki ni kitu kizito kwetu
 
Acha upotoshaji Mzee,kama ni twiga wapo Dunia nzima kama tuu kwa aina nyingine nyingi za wanyama..

Pili kama ni biashara ya wanyama hai iko Dunia nzima wala haijaanza Tanzania ndio maana kuna vitalu vya uwindaji na mabucha rasmi ya nyama pori..

Biashara hii ilikuwepo kitambo na ilipigwa marufuku mwaka 2015 kutokana na kukiukwa kwa masharti na uhuni wa kusafirisha Wanyamapori wasioruhusiwa..

Ikumbukwe kwamba miaka hiyo hakukuwa na mbinu thabiti za udhibiti na ulinzi kama ilivyo sasa,mfano jeshi usu ni full combat kwa ajili ya ulinzi wa maliasili..

Kwa sasa ikitokea uhuni kama ule ujue ni mbinu rasmi..Hata hivyo naona serikali imeruhusu Kwa miezi 6 tena Kwa wanyama ambayo waliathirika baada ya ile marufuku Kwa sababu waliooewa vibali walikuwa wamelipia kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…