Mchango wa hiari. Waulize hela za maafa Bukoba, Arusha, Corona zilitumika vipi ndiyo waje hapa? Vyama vimenyimwa kufanya siasa miaka mitano, kutokuwa na mikutano ya ndani na kesi lukuki eti walikuwa wapi? Waulizwe CCM wanatoa wapi hela za kubeba watu kuleta kwenye mikutano. Msafara wa mgombea wa CCM kwenye kampeni kuna magari na vifaa vya serikali vinatumika kama si mali za wananchi? Vifaa vya matangazo vinatoka PPU na siyo CCM hiyo ni pesa za wananchi. Kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria za uchaguzi swali la huyo
Amani Msumari eti upinzani walikuwa wapi, ajiulize Raisi anaruhusiwa kutoa siyo ahadi bali utelekezaji wa kero au kama ilivyokuwa kutoa ajira za walimu wakati wa kampeni kama si utoaji rushwa? Raisi bila kuona aibu anajenga uwanja wa ndege kwao hakuna hata biashara au wasafiri au watalii wanaokuja anajiita kiongozi wa wanyonge ni mwizi tu. Mbona asingejenga air strip ya kawaida tu kama ilivyo sehemu nyingine? Kwanini alete sheria ya kinga ya Raisi, Waziri Mkuu na Spika kutokushtakiwa kwa makosa walipokuwa madarakani kama siyo anajua machafu waliofanya? Huyu mgombea wa CCM hafai kila tone la damu au mateso waliopata viongozi na wafuasi wa upinzani ikiwamo wafanyabiashara kunyanganywa mali zao ipo siku na hata vizazi vyake hiyo laana haitawaacha. Umetishia viongozi wa dini hasahasa waislamu mashehe waliofungwa bila makosa, viongozi kanisa katoliki na hata kunyima na kuzuia Tundu Lissu aliposhambuliwa asifanyiwe ibada ukijua fika serikali yako imehusika na wewe mwenyewe leo hii unaomba uombewe, unadiriki kushiriki chakula cha bwana kanisani ili hali una chuki na maonevu ya hali ya juu kuwahi kutokea Tanzania. Tukiweka ubinadamu mbele hata wafuasi wa CCM wanajua na wanaona matendo ya huyu Raisi ni mabaya na hayo maendeleo makubwa anayosema kafanya yanasaidia nini kama hakuna haki na uhuru?