Uchaguzi 2020 Watanzania lazima tuhoji kuhusu michango hii inayochangishwa na CHADEMA

Tuandamane kudai haki yetu ya kujua mapato na matumizi kwa sababu pesa nyingine uwa tunachangia papohapo vipi kuhusu hizi kwanini wasiwe wanatangaza baada ya kukusanya tutaandamana.
 
Michango ingechangishwa wakati ule kama serikali ingeruhusu mikutano, kwahiyo huu ndio muda mwafaka.Hataivo muda wa ukombozi ni sasa wala sio miaka 4 iliyopita
 
Trump na biden wanaomba michango kwa wamarekani ndio ije kuwa Lissu ambae hana hata chanzo cha kumwingizia pesa?
 
Trump na biden wanaomba michango kwa wamarekani ndio ije kuwa Lissu ambae hana hata chanzo cha kumwingizia pesa?
Lissu hana chanzo Cha kumwingizia hela, dah wewe kakwambia nani kuwa wakili maoni kwa ngazi ya Lissu hana chanzo Cha mapato?

Ungesema tuu kipato chake hakitoshelezi kugharamia kampeni. Hatahivyo, Lissu sio mgombea binafsi, chama chake ndicho kinatakiwa kubeba msalaba huo. Hivi kipindi cha Dr Slaa mlikuwa mnafanyaje?
 

CHADEMA wanahitaji Tshs 17billions kwa ajili ya kampeni...

Any way possible and legal ya kupata fedha, itatumika...

Tuko kwenye harakati za kuikomboa nchi kutoka kwa mkoloni hatari mweusi aitwaye CCM wakiongozwa na dikteta aitwaye Magufuli....

Watanzania wanahamsika sana. Tabora nilikuwepo, watu walichangia sana 500, 1000, 2000, 5000 na wengine 10,000 nk

Hulazimishwi kuchangia kama huoni umuhimu. Ila kwa kuwa umehoji basi, jibu lake in hilo....!!
 

Naomba nikujibu kwa maswali yako mepesi

Chadema wanapokea ruzuku ya 200m kwa mwez, pesa hiyo hiyo ifanye mambo ya fuatayo

1. Kulipa Pango office zote za chama Tanzania

2. Kulipa mishahara ya wafanyakazi inch mzima

3. Kununua magari ya chama, kuendeleza chama wilayan na vijijini

4. Kununua mafuta na vipuri vya magari

Ishu yako ya kuhoji pesa unazotoa kama mchango, nadhani ukienda uwanjan unakuta jukwaa, unakuta PA, unakuta Genereta
 

Wewe inaonekana una akili ndogo sana kichwani mwako....

Sasa fedha yake ya uwakili aitumie kwenye kampeni? Watoto wake wale nini?

Kwani Magufuli anatumia fedha ya mshahara wake wa Urais na posho zake kufanyia kampeni??

It seems that you're totally confused and frustrated to see how this man (Tundu Lissu) is unexpectedly getting support from the mass & public...

That's what pains you most. Mlidhani atashindwa kufanya kampeni kwa kukosa fedha. Cha ajabu mnashangaa jamaa anapepea tu...

Sasa mnajiluliza; anatoa wapi fedha huyu? Kuna "beberu" fulani analipia kampeni zake?

Kwa sintofahamu yenu, mnaishia kuhoji vimichango vidogo vidogo hivi na likely mnaumiza vichwa kufikiri njia ya kui - ban.... Looh, CCM mnatisha kwa kuchanganyikiwa kwenu!!

Mwambie Jiwe aipige marufuku michango hiyo kama unadhani anaweza...!!
 
Ungehoji kodi unayotoa toka uzaliwe inakwenda wapi licha ya kuwa hali yako ya maisha hailewiki.

Unazungumzia michango kitu ambacho ni hiari ya MTU.
 
1.5 Tillion ikiyoibwa na CAG kufukuzwa ulihoji ? Pesa za kununulia ndege bila kuidhinishwa na bunge ulihoji? Uwanja wa ndege was chato kujengwa bila pesa kuidhinishwa na bunge ulihoji ? Au unafiki unakusumbua .
 
Reactions: dkn
Mleta mada anajisikia vibaya kwanini watu wanachangia chadema anatamani awablock ili pesa ziende ccm kitu ambacho hata Shetani hawezi
 
Hivi unajua kuna watu wamechangishwa kwa barua na wametajiwa na kiwango wanachotakiwa kuchanga na CCM?

Na ofisi Fulani waliambiwa Kila ofisi itoe laki moja.

CCM inachangisha Tena ni lazima uchangie, sijui Kama unalijua Hilo.
 
Mchango ni hiari ndugu na hakuna alolazimishwa, cha ajabu wachangiaji wako happy ila wasochangia ndo wana-vijiba vya roho....

Tatizo lako ni hiyo Username uitumiayo, si lazima uwe against opposition kisa tu watumia jina lalo halisi. Wakeup !!
Mchango wa hiari. Waulize hela za maafa Bukoba, Arusha, Corona zilitumika vipi ndiyo waje hapa? Vyama vimenyimwa kufanya siasa miaka mitano, kutokuwa na mikutano ya ndani na kesi lukuki eti walikuwa wapi? Waulizwe CCM wanatoa wapi hela za kubeba watu kuleta kwenye mikutano. Msafara wa mgombea wa CCM kwenye kampeni kuna magari na vifaa vya serikali vinatumika kama si mali za wananchi? Vifaa vya matangazo vinatoka PPU na siyo CCM hiyo ni pesa za wananchi. Kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria za uchaguzi swali la huyo Amani Msumari eti upinzani walikuwa wapi, ajiulize Raisi anaruhusiwa kutoa siyo ahadi bali utelekezaji wa kero au kama ilivyokuwa kutoa ajira za walimu wakati wa kampeni kama si utoaji rushwa? Raisi bila kuona aibu anajenga uwanja wa ndege kwao hakuna hata biashara au wasafiri au watalii wanaokuja anajiita kiongozi wa wanyonge ni mwizi tu. Mbona asingejenga air strip ya kawaida tu kama ilivyo sehemu nyingine? Kwanini alete sheria ya kinga ya Raisi, Waziri Mkuu na Spika kutokushtakiwa kwa makosa walipokuwa madarakani kama siyo anajua machafu waliofanya? Huyu mgombea wa CCM hafai kila tone la damu au mateso waliopata viongozi na wafuasi wa upinzani ikiwamo wafanyabiashara kunyanganywa mali zao ipo siku na hata vizazi vyake hiyo laana haitawaacha. Umetishia viongozi wa dini hasahasa waislamu mashehe waliofungwa bila makosa, viongozi kanisa katoliki na hata kunyima na kuzuia Tundu Lissu aliposhambuliwa asifanyiwe ibada ukijua fika serikali yako imehusika na wewe mwenyewe leo hii unaomba uombewe, unadiriki kushiriki chakula cha bwana kanisani ili hali una chuki na maonevu ya hali ya juu kuwahi kutokea Tanzania. Tukiweka ubinadamu mbele hata wafuasi wa CCM wanajua na wanaona matendo ya huyu Raisi ni mabaya na hayo maendeleo makubwa anayosema kafanya yanasaidia nini kama hakuna haki na uhuru?
 

Lilitokea tetemeko Kagera watz tukahimizwa sana tuchangie, tukachanga zikafika billion kadhaa!
Hivi ulishawahi kuuliza mchanganuo wa zile fedha ulikuwaje!? Ni wangapi walipewa zile fedha...!?
Cdm wanachangiwa kwa mapenzi ya watz wapenda mabadiliko! Labda utuambie wewe umewachangia kiasi gani ndio uulize imetumikaje!
 
Nilikuwa namjibu mwenzako aliyesema kuwa Lissu hana chanzo cha mapato. Kuhusu akili ndogo, usijali Kaka, inakuwa taratibu hasa inapopata changamoto za akili kubwa Kama yako mkuu
 
Sawa
 
Sawa, umesema vyema. Sasa si kuwe na utaratibu mzuri wa michango kuliko hii ya kurushiana kwa simu?
 
CHADEMA inatakiwa ikusanye ada ya uanachama na pia ihamasishe wanachama kujitolea kwenye shughuli mbalimbali za chama

Michango ikusanywe kwa njia nzuri na ambayo italeta uwazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…