Uchaguzi 2020 Watanzania lazima tuhoji kuhusu michango hii inayochangishwa na CHADEMA

Uchaguzi 2020 Watanzania lazima tuhoji kuhusu michango hii inayochangishwa na CHADEMA

Wapendwa watanzania wenzangu,

Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kikiomba michango kutoka kwa watanzania katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazokikabili chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Watanzania tuna utaratibu wa kuchangiana kwenye mambo mbalimbali hususani misiba na harusi. Hata CHADEMA wanaomba michango kutokana na utaratibu uleule wa kuchangiana, hivyo sio mbaya.

Hatahivyo, nina maswali ya kuhoji Kuhusu Michango hiyo:

Je, ruzuku inayopokelewa chamani, inafanya kazi gani?

Je, yale makato ya shilingi milioni moja kwa kila mbunge, yanatumikaje?

Chama hakina utaratibu wa kupata michango kutoka kwa wanachama wao badala ya kulifanya kuwa jambo la kitaifa?

Kuna uwazi gani katika mapato na matumizi ya michango hiyo?

Je, chama hakikujua kuwa kuna uchaguzi unakuja na kuwa una gharama?

Je, kuwaomba watanzania michango ilihali wamekuwa wakisemwa kuwa ni mafukara sana na kuwa wamepigika si ni unyonyaji kama ni kweli?

Je, mbona hatuoni nguvu kubwa ikitumika kuomba michango kwa ajili ya harambee za kujenga vyumba vya madarasa, zahanati na mambo mengine ya kusaidia maendeleo ya watu wao?

#Kuulizasiujinga

Amani Msumari
Tanga
Hiyo ni kama SADAKA Misikitini na Makanisani, kama wewe huna ama huwezi kutoa achana nayo tu Mkuu. Unapoteza muda wako bure tu, badala ya kuhoji matumizi ya anasa huko CCM kupitia kodi zetu.
 
CCM mnatumia magari zaidi ya 60 kwa mgombea mmoja tu; sasa hizi pesa mnazipata wapi?
Kumbuka kwamba JPM bado ni rais hadi pale atakapoapishwa rais wa awamu ya 6, sasa ulitaka rais wa nchi asafiri vipi?
 
Hiyo ni kama SADAKA Misikitini na Makanisani, kama wewe huna ama huwezi kutoa achana nayo tu Mkuu. Unapoteza muda wako bure tu, badala ya kuhoji matumizi ya anasa huko CCM kupitia kodi zetu.
Kama unadhani CCM Inatumia Kodi yako kwa kufanya kampeni, umeshindwaje kuhoji?
 
Back
Top Bottom