Umeandika kwa uchungu Sana mkuu ila ukweli ulio wazi ni kwamba taifa hili lina mazuzu na mazwazwa ambao ni sawa na akili za nyumbu.
Kutwa kushindana kubishana nani bora Kati ya Ali kiba na Diamond,mijadara ya kijinga ya Simba Na Yanga kwa akili hizi unategemea nani atajivika roho ya kupambania taifa?
Leo akitokea mtu akisema Watanzania tuandamane kupinga matumizi mabaya ya pesa ya umma na Kodi zisizo na kichwa Wala miguu majibu yao utasikia "Nani mimi aanze yeye na familia yake" alafu mtu huyo huyo akikaa kimya utasikia ooh kalamba asali mbona kakaa kimya na shida zetu hizi yaani suala la kuhitaji nguvu ya umma unategemea kikundi fulani ndo ki-fight kwa niaba yako ukitaka ku-prove jambo hili angalia hata hapa JF nyuzi za kumnanga Mbowe, Lissu, Zitto nk utadhani ndo washa wapa ajira ya kuwapigania.