Watanzania mna kichaa!?

Watanzania mna kichaa!?

There is also sense in Nonsense, That is why Feyeraband said it is always reasonable to try and entertain unreasonable views.

Can you please tell me why you think i dont deserve to be rational and objective thinker?
Because your not, no matter how hard you will try.
 
There is also sense in Nonsense, That is why Feyeraband said it is always reasonable to try and entertain unreasonable views.

Can you please tell me why you think i dont deserve to be rational and objective thinker?
Tumieni Lugha ya taifa haya mayai wengine tuna toka kapa wakuu sio wote tumekwenda shule jamani[emoji24][emoji24]
 
Tanzania ipo hapa ilipo kutokana na UJINGA, WOGA na UNAFIKI wa sisi Watanzania.
Sisi tunaoweza kuwawajibisha ni Wabunge.
Sisi ni Wajinga kwa sababu hata Viongozi wetu wakitutendea maovu namna gani tunakaa kimya tu, hatuchukui hatutoi majibu ya haraka kuonesha kutokubaliana na mambo ya ovyo ambayo Viongozi wetu wametutendea.
 
Umeandika kwa uchungu Sana mkuu ila ukweli ulio wazi ni kwamba taifa hili lina mazuzu na mazwazwa ambao ni sawa na akili za nyumbu.

Kutwa kushindana kubishana nani bora Kati ya Ali kiba na Diamond,mijadara ya kijinga ya Simba Na Yanga kwa akili hizi unategemea nani atajivika roho ya kupambania taifa?

Leo akitokea mtu akisema Watanzania tuandamane kupinga matumizi mabaya ya pesa ya umma na Kodi zisizo na kichwa Wala miguu majibu yao utasikia "Nani mimi aanze yeye na familia yake" alafu mtu huyo huyo akikaa kimya utasikia ooh kalamba asali mbona kakaa kimya na shida zetu hizi yaani suala la kuhitaji nguvu ya umma unategemea kikundi fulani ndo ki-fight kwa niaba yako ukitaka ku-prove jambo hili angalia hata hapa JF nyuzi za kumnanga Mbowe, Lissu, Zitto nk utadhani ndo washa wapa ajira ya kuwapigania.
Kweli kabisa aiseee ..Watz bure kabisa, yaani kuwatetea ni hasara!
 
Mtoa mada uko sahihi kabisa! Watanzania wengi tuna vichaa! Na kwa bahati mbaya aliyeturoga, ameshafariki! Sasa sijui tunafanyeje!

Maana haiwezekani kikundi cha watu wachache kifikie jeuri ya kututaka kuhamia nchi jirani, kama hatukubaliani na unyonyaji wao!

Yaani sisi kwa uwingi wetu, tunapelekwa pelekwa tu kama ng'ombe na wajinga wachache wenye ujasiri wa kutuamulia hatma ya maisha yetu! Inasikitisha sana kwa kweli.

Na kwa sababu ya huu upopoma wetu, naamini watoto wetu watakuja kutudharau sana siku watakapo amua kwa dhati kabisa, kupambana kuwaondoa madarakani hawa fisi wenye rangi ya kijani na njano.
 
Ujumbe ukweli mtupu, sema umetolewa kwa mihemko... unafoka sana mkuu
 
Back
Top Bottom