Watanzania mnapenda Rais ajaye 2025 awe na vipaumbele gani?

Watanzania mnapenda Rais ajaye 2025 awe na vipaumbele gani?

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2020
Posts
2,091
Reaction score
1,918
Watanzania, Salaam!

Nianze kwa kuwapa hongera nyingi sana kwa jinsi mnavyopambana kila siku, kila wiki, kila mwezi na kila mwaka kuhakikisha mnayakabili maisha. Kwa wale mliokutana na vikwazo kadhaa niwape pole pia.

Wanasiasa wametuaminisha kwamba kuisha kwa uchaguzi mmoja ndiyo mwanzo wa uchaguzi mwingine - na ndivyo ilivyo. Pamoja na mengi mazuri aliyofanya rais aliyepo Kama:
  • Ununuzi wa ndege,
  • Ujenzi na upanuzi wa viwanja vya ndege,
  • Ongezeko la mapato ya Serikali,
  • Uwajibikaji,
  • Ujenzi wa miundombinu ya Barbara, nk

Je, huyu ajaye kurithi kiti na kijiti hiki azingatie vipaumbele gani kwa umuhimu?
 
Kwa Msoto ninaopitia natamani kuona Sekta binafsi ikipewa vipaumbele vingi, na serikali isiwe mshindani wa sekta binafsi, hapo hata tulio na Msoto wa Ajira tutaweza kupata vibarua na sisi tuwe watu miongoni mwa watu.
 
Masilahi kwa wafanyakazi yaendani na gharama za maisha. Miaka mitano sukari imepanda, mafuta, sembe etc mshahara bado ule ule.

Ajira kwa vijana hili kwa sasa ni jipu limeshaiva.

Uhuru wa kuzungmza (wenye mipaka lakini).

Udhibiti wa gharama za maisha hasa kwenye mahitaji ya msingi.

Kodi zimekuwa ni balaa kwa kweli. Tunawezakweli kutoa kodi ila isiwe kukomoana na ionekane ikinisaidia
 
Awe na matumizi bora ya fedha, asiongozwe kwa hisia binafsi bali hisia za taifa, ajali utu wa binadamu wenzake,awe ni mtu wa kupima kauli zake kabla ya kuzitoa na awe mtu anayejali na kutambua mchango wa wenzake (Team work).
 
Nitazingatia mawazo yako na ya wengine pia. Wewe unatamani niwe na vipaumbele vipi nikishaanza kazi?
 
Kilimo, teknolojia na uwekezaji.

Miundombinu Ni janga tungepunguza miradi mikubwa.

Mikopo nafuu, uwepo wa ajira, mazingira mazuri kwa sekta binafsi.
 
Rais yupi unayeongelea hasa ??, mbona sioni dalili za huyu aliyepo kuchia hicho kiti? na wapambe wake wameshaanza kutengeneza mizengwe ya kumuweka hapo maisha yake yote, umeshasahau mkamia na kessy walivyosema?

Jana nimesikia pale bungeni badala ya kujadili shughuli za maendeleo ya mwananchi maskini wanajadili (huku wakilipwa posho ambazo ni jasho letu sisi maskini) eti kubadirisha vifungu vya katiba ili kuharalisha aendelee.
 
mleta mada naona unauliza watanzania mnapenda kwani wewe ni raia wa nchi gani? tufahamine.Sababu ulivyouliza unaonyesha wazi kuwa wewe sio raia wa Tanzania.Usituingilie mambo ya ndani ya nchi yetu .

Maafisa uhamiaji mtu wenu huyo shughulikeni naye anaonyesha wazi sio raia wa Tanzania

Huyo Ni mkenya yupo Nairobi...
 
Mimi ningependa rais ajaye awe na vipaombele vitatu:

1.Elimu na msisitizo ni elimu ya ufundi kwani kwa takwimu za haraka haraka, mwaka huu waliomaliza form four ni karibu wanafunzi laki nne plus only 30% wataenda kidato cha tano ,hawa watoto walimaliza darasa la saba walikiwa takriban laki 8. Sasa basi only 10 %wataweza kuendelea na elimu ya juu.Hawa 90 % ndio wakushughulika nao kwenye secta nyingine ya elimu.

2.Afya

3.Kilimo na viwanda
 
Jambo la kwanza kabisa ni Kuhuisha Umoja, Upendo na kuheshimiana kwa rika na matabaka yote.

Jambo la pili kuendelea na katiba ya Jaji wariba ilipoishia.

Tatu ni Kuunda tume ya kijaji ya kitaifa ya maridhiano. ( Peace and reconciliation)

Baada ya haya sasa ndiyo mengine yafuate ya Elimu ,Kilimo, Afya na kuhuisha uhusiano wetu sisi na mataifa pamoja na kuheshimu haki za binadamu.
 
Afute posho za wabunge. Mishahara ya wabunge take home iwe TZS 1,200,000 tu. Wakatwe PAYE, NSSF/PSSSF. Pia wafuatilie mafao yao huko PSSSF/NSSF kama wastaafu wengine.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Watanzania, Salaam!

Nianze kwa kuwapa hongera nyingi sana kwa jinsi mnavyopambana kila siku, kila wiki, kila mwezi na kila mwaka kuhakikisha mnayakabili maisha. Kwa wale mliokutana na vikwazo kadhaa niwape pole pia.

Wanasiasa wametuaminisha kwamba kuisha kwa uchaguzi mmoja ndiyo mwanzo wa uchaguzi mwingine - na ndivyo ilivyo. Pamoja na mengi mazuri aliyofanya rais aliyepo Kama:
  • Ununuzi wa ndege,
  • Ujenzi na upanuzi wa viwanja vya ndege,
  • Ongezeko la mapato ya Serikali,
  • Uwajibikaji,
  • Ujenzi wa miundombinu ya Barbara, nk

Je, huyu ajaye kurithi kiti na kijiti hiki azingatie vipaumbele gani kwa umuhimu?
Binafsi ningependekeza kwanza kabisa, wagombea wote wa nafasi za Urais wapitie kwenye mchakato mrefi wa kitabibu ili kujiridhisha kuwa wana afya nzuri ya akili.

Pia idara Usalama wa Taifa, wamchunguze kila mgombea tangu utoto wake kuona kama kuna mambo ya ajabu mabaya ambayo mgomvea amewahi kuyafanya yanayotia shaka juu ya hekima, akili na busara ya mgombea.

Taarifa hizo ziwe miongoni mwa vigezo ambavyo NEC italazimika kutumia wakati wa uteuzi.

Mchakato huo pia uhusishe wakuu wa mihimili mingine, Bunge na mahakama, na idara nyeti kama Mkurugenzi wa NEC na msajili wa vyama vya siasa.

Utawala wa awamu hii umetupa funzo sana, na kuona kuwa kumbe kusipokuwepo umakini, mnaweza kuongozwa na watu ambao kuna mashaka makubwa juu ya utimamu wao wa akili, na kama wana hekima na busara.
 
Nikianzia na upande wa siasa: Napenda Rais awe Mwana diplomasia. Akubali kukaa meza moja na wapinzani wake, akubali kurudisha lile Bunge la Katiba na liwe na Wataalamu wengi kuliko Wanasiasa.

Apungunguze mishahara na posho za Wabunge ili tupate Wawakilishi wa kweli wa kuwasemea Wananchi badala ya hawa Nguruwe waliopo sasa pale Bungeni. Huku akiboresha mishahara ya watumishi wa chini na wale wa kati.

Kiuchumi; Akiugeuze kilimo kuwa fursa kwa Watanzania! Kiwe ni cha umwagiliaji huku kikitumia njia bora na za kisasa kabisa. Mabenki yatengenezewe mazingira ya kushusha riba mpaka ifikie walau 10% ili Watanzania wakope na kujiendeleza kiuchumi katika nyanja mbalimbali.

Kijamii; Aifanye michezo kuwa ni ajira badala ya burudani kama ilivyo sasa. Tuwekeze mzigo wa kutosha kwenye mipango mbalimbali ya kuendeleza michezo mbalimbali nchini kama vile football, riadha, nk.

Sayansi na teknolojia: Awe na mkakati wa kuwaendeleza wagunduzi na wale wanasayansi wa ndani. Aweke bajeti kwa ajili ya tafiti mbalimbali na zenye tija kwa Taifa letu.

Kiujumla naomba sana hiyo 2025 itakapowadia, asitokee tena Rais ambaye ni Mkaidi, Mbinafsi, Mkatili, Dikteta, mungu mtu, Mbaguzi, Muongo, na asiye jali haki za wengine. Kiufupi natamani sana kumpata Rais aina ya Dr. Mohamed Ali Shein au Dr. Hussein Ali Mwinyi.

Mungu Ibariki Afrika Mungu Ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom