Watanzania mnapenda Rais ajaye 2025 awe na vipaumbele gani?

Watanzania mnapenda Rais ajaye 2025 awe na vipaumbele gani?

social promotion. watu wawe na mitaji, watu wawe na biashara, watu wawe na pesa mfukoni.

baada ya hapo ndo atushirikishe katika masuala ya miundombinu.
 
Binafsi ningependekeza kwanza kabisa, wagombea wote wa nafasi za Urais wapitie kwenye mchakato mrefi wa kitabibu ili kujiridhisha kuwa wana afya nzuri ya akili.

Pia idara Usalama wa Taifa, wamchunguze kila mgombea tangu utoto wake kuona kama kuna mambo ya ajabu mabaya ambayo mgomvea amewahi kuyafanya yanayotia shaka juu ya hekima, akili na busara ya mgombea.

Taarifa hizo ziwe miongoni mwa vigezo ambavyo NEC italazimika kutumia wakati wa uteuzi.

Mchakato huo pia uhusishe wakuu wa mihimili mingine, Bunge na mahakama, na idara nyeti kama Mkurugenzi wa NEC na msajili wa vyama vya siasa.

Utawala wa awamu hii umetupa funzo sana, na kuona kuwa kumbe kusipokuwepo umakini, mnaweza kuongozwa na watu ambao kuna mashaka makubwa juu ya utimamu wao wa akili, na kama wana hekima na busara.
Sure
 
Wote huwa wanaanza vizuri wakiwa na uchungu na wanyonge kabla ya kulewa,wakishavimbiwa Kodi utoa ushuzi wa kutesa walipa kodi.Wakitoka madarakani huwa na akili tena.
Watawala wa kiafrica huwa na akili mfumo ukishawatupa.
 
Watanzania, Salaam!

Nianze kwa kuwapa hongera nyingi sana kwa jinsi mnavyopambana kila siku, kila wiki, kila mwezi na kila mwaka kuhakikisha mnayakabili maisha. Kwa wale mliokutana na vikwazo kadhaa niwape pole pia.

Wanasiasa wametuaminisha kwamba kuisha kwa uchaguzi mmoja ndiyo mwanzo wa uchaguzi mwingine - na ndivyo ilivyo. Pamoja na mengi mazuri aliyofanya rais aliyepo Kama:
  • Ununuzi wa ndege,
  • Ujenzi na upanuzi wa viwanja vya ndege,
  • Ongezeko la mapato ya Serikali,
  • Uwajibikaji,
  • Ujenzi wa miundombinu ya Barbara, nk

Je, huyu ajaye kurithi kiti na kijiti hiki azingatie vipaumbele gani kwa umuhimu?
Kwani ILANI ya kijani ya 2025 Imeahatoka?🙄🙄
 
Afute posho za wabunge. Mishahara ya wabunge take home iwe TZS 1,200,000 tu. Wakatwe PAYE, NSSF/PSSSF. Pia wafuatilie mafao yao huko PSSSF/NSSF kama wastaafu wengine.
Ndugu konda msafi unataka wabunge waache tena kujadili bajeti wazozane posho ziongezwe😆😆
 
Tunataka aijenge Chato hadi ifikie lile jiji la China alilolisema Prof Kabudi. Hicho ndicho kipaumbele chetu tunachotaka sisi wananchi wanyonge.
Ujamsikia mbunge Msukuma anasema mnajengewa miundombinu siyo kuwapa huduma ila kuwafanya fursa😆😆
 
For sure wengi mmemwagika vizuri - lkn nilipenda kupata uchambuzi wa kisekita - mfano ukisema ajira kwa vijana eleza hapa kipi kifanyike, kilimo kipi kifanyike nk
 
Awe na mahusiano mazuri na jumuiya ya kimataifa.
Ajali watumishi wa umma
Asiue asowapenda
 
Nikianzia na upande wa siasa: Napenda Rais awe Mwana diplomasia. Akubali kukaa meza moja na wapinzani wake, akubali kurudisha lile Bunge la Katiba na liwe na Wataalamu wengi kuliko Wanasiasa.

Apungunguze mishahara na posho za Wabunge ili tupate Wawakilishi wa kweli wa kuwasemea Wananchi badala ya hawa Nguruwe waliopo sasa pale Bungeni. Huku akiboresha mishahara ya watumishi wa chini na wale wa kati.

Kiuchumi; Akiugeuze kilimo kuwa fursa kwa Watanzania! Kiwe ni cha umwagiliaji huku kikitumia njia bora na za kisasa kabisa. Mabenki yatengenezewe mazingira ya kushusha riba mpaka ifikie walau 10% ili Watanzania wakope na kujiendeleza kiuchumi katika nyanja mbalimbali.

Kijamii; Aifanye michezo kuwa ni ajira badala ya burudani kama ilivyo sasa. Tuwekeze mzigo wa kutosha kwenye mipango mbalimbali ya kuendeleza michezo mbalimbali nchini kama vile football, riadha, nk.

Sayansi na teknolojia: Awe na mkakati wa kuwaendeleza wagunduzi na wale wanasayansi wa ndani. Aweke bajeti kwa ajili ya tafiti mbalimbali na zenye tija kwa Taifa letu.

Kiujumla naomba sana hiyo 2025 itakapowadia, asitokee tena Rais ambaye ni Mkaidi, Mbinafsi, Mkatili, Dikteta, mungu mtu, Mbaguzi, Muongo, na asiye jali haki za wengine. Kiufupi natamani sana kumpata Rais aina ya Dr. Mohamed Ali Shein au Dr. Hussein Ali Mwinyi.

Mungu Ibariki Afrika Mungu Ibariki Tanzania.
Analytical capacity yako ni kubwa - ninge
Tunataka ml 50 kila kijiji
Zinaweza kutolewa lkn matatizo yakawa pale pale
 
Awe mbunifu na muungwana pia awekeze zaid keenye sekta binafsi kupunguza makali ya ajira
 
Awe anatoa chakula cha mchana kwa wazee vijijini hasa chips na kitimoto. Jaman kuna watu vijijin hata chips hawajui.
 
Tunataka aijenge Chato hadi ifikie lile jiji la China alilolisema Prof Kabudi. Hicho ndicho kipaumbele chetu tunachotaka sisi wananchi wanyonge.
jamani huyu Kabudi kumbe tangu awali alikuwa anajipendekeza hivyo, badala ataje Dodoma aua Kilosa yey anapepelea Chato
Mama kamrudisha Katiba na Sheria hapo atulie tu sasa
 
Binafsi nataka Rais ajaye awe na hekima na busara
Na mambo mie naona Rais ikimpendeza pia ajaribu ku discourage wale watu na viongozi ambao kila wakipata nafasi ya kuzungumza, inakuwa ni kumpongeza yeye binafsi hata kwa shughuli na majukumu ambayo ni wajibu na kazi inazopaswa serikali kuwatumikia wananchi wake. Mafanikio yapongezwe zaidi kama ya serikali ya awamu ya.....(jointly as a team), na sio kumfanya Rais aishiye kuwa kila mwananchi anamuona ndie anakuwa pekee ndie mtatuzi wa kila kitu kinachowasumbua ktk jamii zao. Viongozi wawajibike na sio kumwachia kila kitu ambacho, wangeweza tatua, inabidi hadi Rais aingilie kati. Inakuwa mwisho wa siku Rais anakuwa na mizigo ya kazi nyingi badala ya kushughulikia maswala makubwa na ya msingi....
 
Back
Top Bottom