Na mambo mie naona Rais ikimpendeza pia ajaribu ku discourage wale watu na viongozi ambao kila wakipata nafasi ya kuzungumza, inakuwa ni kumpongeza yeye binafsi hata kwa shughuli na majukumu ambayo ni wajibu na kazi inazopaswa serikali kuwatumikia wananchi wake. Mafanikio yapongezwe zaidi kama ya serikali ya awamu ya.....(jointly as a team), na sio kumfanya Rais aishiye kuwa kila mwananchi anamuona ndie anakuwa pekee ndie mtatuzi wa kila kitu kinachowasumbua ktk jamii zao. Viongozi wawajibike na sio kumwachia kila kitu ambacho, wangeweza tatua, inabidi hadi Rais aingilie kati. Inakuwa mwisho wa siku Rais anakuwa na mizigo ya kazi nyingi badala ya kushughulikia maswala makubwa na ya msingi....