Watanzania msibabaishwe na maisha ya Marekani. Wamarekani wengi ni choka mbaya, hawana uwezo wa kumiliki nyumba kama ninyi, wanaishi kwenye kota

Na maisha utapata na nyumba utajenga nina uhakika ndugu yangu, hapa Tz utatoboa
Bongodili tele kama ukiwa na pesa,huku fursa tele kuliko USA shida msingi na mifumo kandamizi mifumo yetu inakuvuta chini Kule mifumo yao inakuvuta juu thus USA inaitwa land of opportunities ukiwa na ndoto ni rahisi kutimiza malengo kule
 
mbwa wa marekani kanona kuliko mbwa wa tanzania tena wana hospitali na mahakama tuanze hapo
 
Ila ni kweli,basi tu
Ht sauz hapo kumiliki ardhi,nyumba sio km hapa bongo
Ila fursa za kazi na salary ni Bora huko majuu
 
🤣🤣🤣
 
Ukiwa mtoto wa mama mboga saba bongo huwezi kuishi ulaya na marekani lakn mm mtoto wa mkulima sina ajira mwaka wa nane huu,nimevua samaki Sana,nimechimba maduara kusaka dhahabu,vimeshinda shambani Sana lakn mpaka sasa naishi kwenye kitu wanaita subsistence living.

Kwa hakika nakwambia kama Mungu anatenda miujiza basi kesho niamkie marekani halafu nisipo toboa basi heri nife tu.

Kwann nasema haya jamaa yangu mmoja aliyeshinda green card mwaka 2019 ya kuingia marekani kafanya matusi bongo Kwa miaka hii mitano.

Kuna jamaa kaingia Kwa intern za kilimo marekani mwaka 2020 nae kafanya matusi bongo,lakn hawa wote ni watoto wa makulima wamekulia uji ya chumvi asubuhi,mchana viazi na maji kama lunch usiku ugali na kabichi.

Maisha ni magumu tangu wako bongo baada ya kutua marekani Kwa hakika hawana mchezo.

Sasa wewe mleta mada subiri mdingi afe ugombanie urithi tu maana kupambana huwezi.
 
Nipo ulaya miaka miwili sasa nakazia hii kauli bora uwe mbwa ulaya kuliko binadam kuwa mtumishi wa umma au mfanya biashara wa kawaida bongo. Tusiishie kulaumu hizi kauli tuchukue hatua nasis kupafanya bongo mahali pazuri kuishi kama walivyofanya huku wenzetu mbona tuna nchi nzuri M/Mungu katupendelea ila upumbavu/ubinafisi na sasa uchawa vinazid kufifisha ndoto ya bongo kuwa mahali pazuri kwa kuishi kwa kila mtu.
 
Acha ujinga , kama Marekani ni jehanamu basi Bongo ni jehanamu times 1000
Yaani ugumu wa maisha Bongo na Marekani ulingane ?
Unajua unachoandika wewe ?
Au ndio ninyi parasites wa uvccm na mnaobenefit Kwa uchawa ?
Unajua ugumu wa kuisaka shilingi Bongo hapa ?
Unajua jinsi mamilioni ya watu wanavyoishi substandard life na life la kuunga unga Bongo humu ?
Nchi ambayo mamilioni ya watu hawana ajira wala kipato cha uhakika
Nchi ambayo mamilioni ya raia wanaishi kwenye makazi duni ,afya duni ,maji machafu ,afya mbovu ,barabara hadi vyoo + magonjwa ya milipuko ya kusababishwa na poor hygiene .
Mamilioni ya watu wanakabiliwa na utapia mlo
Halafu ujilinganishe na mtu anayeishi Marekani ,una akili au tope wewe ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…