Ndugu zangu,
Amerika si ya kila mtu.
Hawa wanaopiga miluzi ya kuiponda U.S mitandaoni asilimia kubwa ni wale waliowahi kufika huko.
Lakini walikurupuka kwenda bila mipango madhubuti, walivyofika huko wakalazimisha kubaki lakini kizembe.
Mwishowe wakajikuta wako 'out of status', - Illegals machoni mwa Sheria.
Hapo wanasavaivu wanaume tu.
Watoto wa mama hakuna rangi hataiona.
Kazi utapata lakini unapunjwa malipo na unafichwafichwa, ukiwa fala hata kuzipata za maana kupati.
Ukikumbuka Dingi/Bi mkubwa hana hali mbaya saana Bongo unaona yanini?
Lazima nyani ateme Bungo lakini kwa hasira na makasiriko kama haya sasa.
Challenge:
Nionyeshe Ombaomba mwenye asili ya ya Tanzania au Muafrika wa Asili kutoka Nchi yoyote ambae sio Mraibu au Outlaw.
Unajua kwa nini?
Kulala nje kwa Mmarekani kuna kuhusu nini wewe Mmatumbi kama mambo yako yanenda?
--------------------------------------------------------------------------
MAMBO NI DV-2026.
Nawakumbusha wale ambao wanatamani kuingia U.S kiuhalali,
kiulaini na pia kuwa na nafasi isiyo na shaka ya kufanikiwa kiurahisi
(unaingia na Vibali muhimu vya Kazi kutoka
kwenu)kuna kitu inaitwa BAHATI NASIBU YA KUHAMIA MAREKANI almaarufu DV LOTTERY.
Itachezwa kuanzia wiki ya kwanza ya mwezi wa kumi ( Octoba)
Kushiriki ni bure
(Hulipii kucheza ingawa ukichaguliwa zipo gharama za kulipa kwa Serikali ya Marekani)
Vigezo muhimu:
-Elimu ya Sekondari,
-Umri kuanzia miaka 18+
-uwe na Uraia wa Tanzania.
Kama unaijua hii program hewala, jiandae.
Lakini, kama huijui anza kusoma taratibu zake sasahivi ili muda ukifika unajua inahusiana na nini hasa na utafuata taratibu kama utakavyoelekezwa na wenyewe.
Ukihitaji msaada wangu hapo muda utakapofika,
utalipia muda wangu na nitakuongoza kuanzia unapocheza hadi ukifanikiwa kuchaguliwa.
Na tafadhali tunza namba yangu: +255714591548.
Sasa wewe fanya uzembe usiitunze utaitafuta hii.
Nawakilisha.