Watanzania na unafiki huwezi kuwatenganisha

Wewe ndio nyumbu anaesemwa
Hata tukipata katiba mpya hatuwezi kusema polepole alikufa akipambania katiba mpya. Ndio maana nimesema huyu jamaa kifo chake ni sawa na mbwa koko aliyegongwa na fuso. Inabidi upambanie kitu ambacho hata wakikuuwa utaacha historia. Nakuambia huyu ndani ya wiki mbili tushamsahau.
 


Kwahiyo unahisi au unajihisi umeandika nondo

Issue ni brutality kutoka kwa vyombo vya dola

Waambie wasitumia violence then uone km hatitaandamana
 
Na kila mtanzania analalamika watanzania wana roho mbaya ,hapo ndio kuna maajabu 🤣
Mimi ni mtanzania lakini sio mnafiki wala sina roho mbaya lakini sina tabia ya kushabikia ujinga na upumbavu unaofanywa na watu kama polepole , Gwajima na kapteni TEJA!.
 
Na walivyo wanafiki wanawalaumu wasanii kwanini wanakaa upande wa serikali na wengine Wana unfollow lakini ukweli ni kwamba kwa namna walivyowatanzania hao wasanii wapo sahihi kukaa huo upande maana hawaoni faidi ya kukaa kwa wabongo
 
Utateteaje CCM na unataka mabadiliko ? Huyu alikuwa hana wa kumshauri. Unaacha kazi na unapinga uteuziwwa mgombea urais halafu unakitetea chama chako. Are you serious ? Huyu mbwiga kifo chake hakitakuwa na maana kwenye historia ya Tanzania. Alitakiwa aelezee ubaya wa CCM na mfumo wa serikali. Atetee katiba mpya na kutaka mfumo mpya wa serikali. Sasa mtu anang'ang'ania Samia aachie ngazi na tuelekee kwenye uchaguzi. Mimi nikawa najiuliza huyu ameacha kazi kutaka kubadilisha mgombea wa urais ? Kinachoniuma tukitengeneza kumbukumbu ya watu waliouliwa kwa ajili ya kulipambania, taifa pole pole amepambania nini ? Angeacha kazi na kuongelea katiba mpya tusogeze uchaguzi hata miaka miwili ningemuona wa maana sana.Maana hata kifo chake kitakumbukwa kuwa alipigania Katiba mpya. Lakini nakuhakikishia kama wakimuua ndani ya wiki mbili tushamsahau.
 
Nakubaliana na wewe, Wa TZ ni wanafiki, watekwaji na ndugu wa watekwaji pia ni wanafiki. Fikiria watekwaji wangapi nchi hii waliobahatika kupatikana hakuna hata mmoja aliyewahi kutusaidia kuwajua waliowateka kila anayehojiwa utasikia hiyo ni kazi ya Polisi sababu anahofia watamfuata tena!!!!. Ndugu wanasema waliwaona watekaji wa ndugu yao na wanawataja Kwa Majina wakiitwa kusaidia uchunguzi wanaingia mitini. Ndio maana akina Mwafwele wanaendelea na Maisha yao Kwa sababu hakuna ushahidi. Wanaharakati, watetezi wa haki za binadamu wanaopambana na haya yakomeshwe na tunaowapelekea taarifa mbalimbali wameabaki na lugha za "NASIKIA" , "NIMEAMBIWA", "INASADIKIWA" Lugha ambazo hazina msaada wowote katika kufanikisha kukomesha haya. Tusubiri siku Polisi wetu watakapokuwa Wana uwezo wa Uganga wa Kienyeji wa kujua mharifu alipo!!!!
 
100%
 
vijana msihadaike na maswala ya mtandaoni mkawaumiza wapendwa wenu
 
Kwahiyo unahisi au unajihisi umeandika nondo

Issue ni brutality kutoka kwa vyombo vya dola

Waambie wasitumia violence then uone km hatitaandamana
Huo sasa ni uchawi, umezidi kiwango cha unafki aloo!! 😹😹

Nyie ndo ninaowaongelea mnataka muandamane bila bugudha km mpo America au sio? Utasubiri sana wali kwenye silver plate 😹😹🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…