Watanzania na unafiki huwezi kuwatenganisha

Watanzania na unafiki huwezi kuwatenganisha

Kila siku si nakwambia nyie ni waoga kama nyumbu? Manyumbu ukiyakuta porini yalivyokusanyika unaweza kusema yanaushirikiano kweli ila hata mtoto wa miaka miwili anaweza kushika fimbo na kwenda kuzitoa baru nyumbu zote 400 na zikakimbia.

Sasa wewe Lamomy na keyboard warriors wenzako ndo mnatabia hizo za kinyumbu, ni hatari sana mtu kuwa upande wenu na kama kaamua kuwa upande wenu basi inatakiwa aamue kuwa hahitaji msaada wenu na yuko tayari kukabiliana na outcomes akiwa peke yake.

Na hivyohivyo kesho atatekwa mwingine ila hamtatoka, tarehe 29 hakuna anaetoka pia, na hata wewe unaweza kutekwa na hizi nyumbu mnazojaziana comments za kuwa mtatoka tarehe 29 hazitathubutu hata kuandamana hatua mbili kwaajili yako.

Nyumbu wewe Lamomy.
Tuanze mimi na wewe leo tuandamane tuanzie barabara ipi?
 
Duh simjui huyo mtu bwashee
 
Duh noma
 
Watanzania sisi ni wanafiki sana haijawahi kutokea, mtanzania mnaweza kupanga jambo pamoja lakini mbele akakusaliti sijui ni roho mbaya au wivu?

Ngoja niwaambie, sisi watanzania sio waoga ila tunateswa na UNAFIKI.
Ukitaka kujua mtaani tunapoishi umeme ukatike, cha kwanza ni kuchungulia kama kwa jirani upo? Kama upo basi anawapigia Tanesco kuwauliza “Mbona mmekata umeme kwangu lakini kwa jirani yangu unawaka? Hataki kujua kama kwake inawezekana line ina tatizo ila anachotaka wote wakae na giza..!!

Na huyo jirani yake mwenye umeme naye sio kwamba hana unafiki la hasha.. wote walewale atafurahi ndani kwake kuona mtaa mzima ana umeme. Na kufurahia pindi wanapoteseka kuleta simu zao zichajiwe..!! Hao ndo watanzania.

Polepole inadaiwa katekwa lakini watanzania wamekausha kama sio walewale waliokua wanasema njoo useme ukiwa Tanzania tukiwa wote.
Leo hii hao hao wanasema kwanini alisema mambo yote hayo akiwa nchini..!!
Dah!! Watanzania unafiki unatutesa..
Sasa hivi washabadili upepo wanasema watamkomboa tarehe 29 seriously? 😥

Wengine washajipa uzee wanaomba Gen Z na jeshi liwasaidie ili baadae wapate wa kuwanafkia na kuwabebesha lawama. 😹

Niwaambie tu hiyo tarehe 29 hakuna wa kuandamana sababu sisi sio waoga ila wanafiki..!!
Mama kizimkazi anatujua vizuri na ndiomana alituambia hakuna nywinywii tar 29 zozote tutakazoleta.
Wakuu tuendelee kutafuta school fees za kina nyunyia January sio mbali. 😹

Niliwahi kwenda Turkey nilishangaa sana watanzania hawako karibu na watanzania wenzao wanakwepana. Nilipomuuliza mwenyeji wangu akaniambia Lamomy ni bora uwe na urafiki na mataifa mengine sio mtanzania. Hachelewi kukuchoma au kuharibu msala ukabeba wewe..

Na nyie mnaochekelea haya ipo siku yenu itafika, mkumbuke hata Polepole alikula na kunywa nao high table na alikuwa mmoja wao enzi za ufalme wake lakini sasa imebaki story..!!

NB: Kila afurahiaye maovu atafikiwa kwa muda wake. Ni suala la muda. Waswahili tunasema kutesa kwa zamu
Najivunia kuchanganya utaifa, Sina damu ya kinyumbu
 
Kila siku si nakwambia nyie ni waoga kama nyumbu? Manyumbu ukiyakuta porini yalivyokusanyika unaweza kusema yanaushirikiano kweli ila hata mtoto wa miaka miwili anaweza kushika fimbo na kwenda kuzitoa baru nyumbu zote 400 na zikakimbia.

Sasa wewe Lamomy na keyboard warriors wenzako ndo mnatabia hizo za kinyumbu, ni hatari sana mtu kuwa upande wenu na kama kaamua kuwa upande wenu basi inatakiwa aamue kuwa hahitaji msaada wenu na yuko tayari kukabiliana na outcomes akiwa peke yake.

Na hivyohivyo kesho atatekwa mwingine ila hamtatoka, tarehe 29 hakuna anaetoka pia, na hata wewe unaweza kutekwa na hizi nyumbu mnazojaziana comments za kuwa mtatoka tarehe 29 hazitathubutu hata kuandamana hatua mbili kwaajili yako.

Nyumbu wewe Lamomy.
Wewe Lucas mwashamba wa bei za jioni nitolee ujinga wako hapa..!!

Nyie machawa ndo kundi namba moja la wanafki bata wee 😹
 
Back
Top Bottom