Watanzania na unafiki huwezi kuwatenganisha

Watanzania na unafiki huwezi kuwatenganisha

Watanzania hata ajali hawasaidii majeruhi ila wako busy kushindana kurekodi wawahi kupost. Tumekuwa watu wa hovyo sana..!!
Hivi mpaka kiongozi wa nchi anasimama bila woga wowote anasema hakuna cha nywinywinywi wala nywanywanywa unadhani hiyo jeuri anaipata wapi? Washatujua sisi ni mazumbukuku hakuna kitu tutafanya.
 
Mtoto wa kiume unajisifia kukaa ghetto huku unakuna vi nyanya mshenzi unaacha kupambania nchi yako si ndo unafki wenyewe huo..!!
Kuliko niungane na nyie nyumbu waoga bora nikune hivyo vinyanya mshenzi
 
Niliwahi kumpiga mwalimu Tambaza Secondary (kosa lilikuwa lake mwalinu, si langu), mzazi akaitwa shule.

Nikawekwa assembly. Wanafunzi wakanishangilia saana kwa kumpiga mwalimu.

Mzazi wangu akaniambia unawaona hawa wanaokushangilia hawa? Sasa unapewa adhabu kali sana wote wanaokushangilia hawatakusaidia kwenye hiyo adhabu.

Na kweli. Nikapewa bonge la adhabu nikaifanya mwebyewe bila kusaidiwa.
Hero ukawa zero 😹
Watanzania sio wa kututegemea..!!
 
Watanzania hata ajali hawasaidii majeruhi ila wako busy kushindana kurekodi wawahi kupost. Tumekuwa watu wa hovyo sana..!!
Hahahaha kama ni muandishi wa habari Yuko sahihi kupost na si kusaidia,maana kazi yake kuu ni KURIPOTI MATUKIO na si kusaidia wahanga,😂it's funny lkn ndio Iko hivyo
 
Mie nasubiri kuona reaction yenu, watanzania ktk kujikomboa ,hiyo tarehe si mmetaja nyie ? Mkiweza itakua poa sana na hongera nyingi kwenu
Ona sasa hii pimbi, kwahiyo sisi tuandamane wewe umejifungia ndani unafua boxer za shemeji sio? Nikikuambia tofauti yako na tako ni location tuu nitakua nakukosea mkuu?
 
Ona sasa hii pimbi, kwahiyo sisi tuandamane wewe umejifungia ndani unafua boxer za shemeji sio? Nikikuambia tofauti yako na tako ni location tuu nitakua nakukosea mkuu?
Mie Nina vita vyangu kwetu huko,hii ya kwako imalize tu,Mkuu haina haja ya kugombana, tikishinda tukutane Dubai kwa Glass ya cheers,😂
 
Watanzania sisi ni wanafiki sana haijawahi kutokea, mtanzania mnaweza kupanga jambo pamoja lakini mbele akakusaliti sijui ni roho mbaya au wivu?

Ngoja niwaambie, sisi watanzania sio waoga ila tunateswa na UNAFIKI.
Ukitaka kujua mtaani tunapoishi umeme ukatike, cha kwanza ni kuchungulia kama kwa jirani upo? Kama upo basi anawapigia Tanesco kuwauliza “Mbona mmekata umeme kwangu lakini kwa jirani yangu unawaka? Hataki kujua kama kwake inawezekana line ina tatizo ila anachotaka wote wakae na giza..!!

Na huyo jirani yake mwenye umeme naye sio kwamba hana unafiki la hasha.. wote walewale atafurahi ndani kwake kuona mtaa mzima ana umeme peke yake. Na kufurahia majirani zake pindi wanapoteseka kuleta simu zao zichajiwe..!! Hao ndo watanzania.

Polepole inadaiwa katekwa lakini watanzania wamekausha kama sio walewale waliokua wanasema njoo useme ukiwa Tanzania tukiwa wote.
Leo hii hao hao wanasema kwanini alisema mambo yote hayo akiwa nchini..!!

Dah!! Watanzania unafiki unatutesa..
Sasa hivi washabadili upepo wanasema watamkomboa tarehe 29 seriously? 😥

Wengine washajipa uzee wanaomba Gen Z na jeshi liwasaidie ili baadae wapate wa kuwanafkia na kuwabebesha lawama. 😹

Niwaambie tu hiyo tarehe 29 hakuna wa kuandamana sababu sisi sio waoga ila wanafiki..!!
Mama kizimkazi anatujua vizuri na ndo maana alituambia hakuna nywinywii Oktoba 29 zozote tutakazoleta.
Wakuu tuendelee kutafuta school fees za kina nyunyia January sio mbali. 😹

Niliwahi kwenda Turkey nilishangaa sana watanzania hawako karibu na watanzania wenzao wanakwepana. Nilipomuuliza mwenyeji wangu akaniambia Lamomy ni bora uwe na urafiki na mataifa mengine sio mtanzania. Hachelewi kukuchoma au kuharibu msala ukabeba wewe..

Na nyie mnaochekelea haya ipo siku yenu itafika, mkumbuke hata Polepole alikula na kunywa nao high table na alikuwa mmoja wao enzi za ufalme wake lakini sasa imebaki story..!!

NB: Kila afurahiaye maovu atafikiwa kwa muda wake. Ni suala la muda. Waswahili tunasema kutesa kwa zamu
Japo sikubaliani na wewe lakini niseme jambo moja:

Watanganyika wote wanapenda kupata pesa kirahisi yaani bila jasho, hivyo kila kitu kwao ni dili. Mtu akiambiwa akuwekee sumu katika kinywaji au chakula hataona kuwa anashiriki kuua bali ataona kuwa ni dili la kupata pesa hivyo atafanya.

Jambo la pili, kila mtanganyikq ni CCM hata wale unaowaona vyama vya upinzani ni CCM, ni kama vile kila mchezaji mpira au shabiki hata awe timu gani ni lazima atakuwa anashabikia Yanga au Simba.
Ila mtu akiona kwa kipindi fulani maslahi yake CCM hayako taken care basi atatafuta pointi moja au mbili zenye ukweli na kuanza kuishambulia CCM, akirekebishiwa maslahi yake basi anageuka..

Ndio maana Kigogo, Maria Sarungi, Mange Kimambi naChachakli kuna wakati walikuwa wamoja wote katika kuunga mkono na kupinga CCM lakini kwq sasa wamegawanyika tena ila wote bado ni CCM. Mimi nashangaa watanganyika kuwaamini hao wakati wao wanapigania maslahi yao na wananufaika kwa posts wanazopost mitandaoni na pesa za wafadhili.

Ujue Maria na yule mtoto wa mjini ( (aka msoga) ni kitu kimoja na ipo siku waziwazi ataunga mkono CCM.
Ekewa kuwa,mtanganyika yeyote anaweza kukusaliti wakati wowote maslahi yake yakizingatiwa.

Fanya kazi tafuta maisha kihalali acha kuhadaika na maneno ya key boards. Sali mwombe Mungu basi.

Hakuna wa kuleta vurugu katika nchi hii.
 
Unafiki mwingine ni kushindwa kumchana Polepole kwa aliyoyafanya alipokua kwenye peak ya power yake, sasa hivi kwa unafiki tunaifanya hatukumbuki.

Ndio maana hata watawala wanatufanyia wanayotufanyia sababu wanajua siku wakijifanya wako upande wetu, sisi na unafiki wetu tunajifanya tumesahau.
 
Wallah siku nikiwa platinum member mtu akinikera namkiss 😂

Ukiwa platinum ukawa mgomvi/mswahili swahili unashusha brand 🤣

Hivi mnatoa shi ngapi huko uplatinumzz ili Lamomy na braza Evelyn Salt wafuate
Mimi nikiwa nayo mchana jioni washanivua u platinum mapema nitashindwa vigezo, utakatifu siuwezi kabisa najijua..!! 😹😹
 
Ogopa sana mtu akujue nje ndani. Hao viongozi wameisha tambua wana raia wa aina ipi na wawatale vipi. Wajua fika asilimia kubwa ni waoga, wanafiki na wapenda mambo ya kijinga jinga tu. Ndio maana wana jeuri ya kufanya na kuongea chochote na hakuna reaction yoyote ile itatoka kwa raia.

Nakumbuka uliwahi kuniambia haya mambo ya siasa ukiyafuatilia yanaumiza sana ni kheri ukae kimya tu uendelee na mishe zako.
Hivi mpaka kiongozi wa nchi anasimama bila woga wowote anasema hakuna cha nywinywinywi wala nywanywanywa unadhani hiyo jeuri anaipata wapi? Washatujua sisi ni mazumbukuku hakuna kitu tutafanya.
 
Japo sikubaliani na wewe lakini niseme jambo moja:

Watanganyika wote wanapenda kupata pesa kirahisi yaani bila jasho, hivyo kila kitu kwao ni dili. Mtu akiambiwa akuwekee sumu katika kinywaji au chakula hataona kuwa anashiriki kuua bali ataona kuwa ni dili la kupata pesa hivyo atafanya.

Jambo la pili, kila mtanganyikq ni CCM hata wale unaowaona vyama vya upinzani ni CCM, ni kama vile kila mchezaji mpira au shabiki hata awe timu gani ni lazima atakuwa anashabikia Yanga au Simba.
Ila mtu akiona kwa kipindi fulani maslahi yake CCM hayako taken care basi atatafuta pointi moja au mbili zenye ukweli na kuanza kuishambulia CCM, akirekebishiwa maslahi yake basi anageuka..

Ndio maana Kigogo, Maria Sarungi, Mange Kimambi naChachakli kuna wakati walikuwa wamoja wote katika kuunga mkono na kupinga CCM lakini kwq sasa wamegawanyika tena ila wote bado ni CCM. Mimi nashangaa watanganyika kuwaamini hao wakati wao wanapigania maslahi yao na wananufaika kwa posts wanazopost mitandaoni na pesa za wafadhili.

Ujue Maria na yule mtoto wa mjini ( (aka msoga) ni kitu kimoja na ipo siku waziwazi ataunga mkono CCM.
Ekewa kuwa,mtanganyika yeyote anaweza kukusaliti wakati wowote maslahi yake yakizingatiwa.

Fanya kazi tafuta maisha kihalali acha kuhadaika na maneno ya key boards. Sali mwombe Mungu basi.

Hakuna wa kuleta vurugu katika nchi hii.
Sasa si umerudi palepale ninaposema sisi wanafki mkuu 😹
Tuko same page hao unaowasema km kweli wapo ki maslahi nao wanatufanyia unafki watanzania wenzao.
 
Lengo la uzi sio kukemea unafiki bali kukatisha tamaa mipango ya maandamano kwa usisubiri siku ifike ndio uandike huu utumbo wako!
 
Unafiki mwingine ni kushindwa kumchana Polepole kwa aliyoyafanya alipokua kwenye peak ya power yake, sasa hivi kwa unafiki tunaifanya hatukumbuki.

Ndio maana hata watawala wanatufanyia wanayotufanyia sababu wanajua siku wakijifanya wako upande wetu, sisi na unafiki wetu tunajifanya tumesahau.
Walimchana sema sababu ya unafki wetu tukafunika kombe..!
 
Back
Top Bottom