Watanzania nawauliza ?

Watanzania nawauliza ?

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
4,432
Reaction score
3,013
Mimi ni member wa facebook,nimekuwa nikikutana na watu tofauti katika facebook,facebook imeniunganisha na watu tofati wakiwamo ndugu zangu ,rafiki zangu tulisoma shule pamoja,pia new friends.

Katika facebook kuna watu wa aina nyingi ila katika research yangu nimegundua hivi,kuna watu wako tanzania na ambao wako njee ya tanzania,kama bara la ulaya na America,canada n.k

kwa nini watu ambao wako tanzania hawapendi kuwatumia comments katika picha zao watu walioko njee ya Tanzania kama Nchi mabara wanayoishi hapo niliyoyataja ?

Pia unapokutana na mtu ambaye kwa muda mrefu sana hamujaonana kama utakumbana nae facebook hata kama mtu huyo sio mtu wako wa karibu akishajua tu upo ulaya or outside ya tanzania anakuwa karibu na wewe,pia kwa time ya mwanzo tu kukuona anakuuliza maisha badala ya kukuuliza hali yako,jinsi mulivyopoteana,au mulivyomisiana, na mengine ukitoa ya maisha ?
 
Mimi sijui facebook inafananaje.
Ya fb tuyaache fb labda uedit hapo uweke jf nitoe makoments.
Hata hivyo kwani mtu akikuuliza habari za maisha wakati upo ulaya unafikiri atakuomba nauli aje huko au??
 
Mbona mimi sijaona hiyo!! Ulifanyaje hiyo research ndugu?
 
Kweli kabisa!Mi mwenyewe nna tabia hiyo!Mtu akiniambia yuko nje nampapatikia kama pesa!Hata kama hatukuwahi kuzoeana sana ntajifanya kama vile tu mabeste ili anipe dili!
 
Kweli kabisa!Mi mwenyewe nna tabia hiyo!Mtu akiniambia yuko nje nampapatikia kama pesa!Hata kama hatukuwahi kuzoeana sana ntajifanya kama vile tu mabeste ili anipe dili!
na hili ndilo jibu alilo nalo mtoa mada kichwani alitaka tu kusikkia wengine watasemaje!!
 
fb ya watoto

kweli kabisa, fb imejaa ngonolization tupu,,, zaidi wakina dada wanapost picha zao za uchi,, maada zinazozungumzia maswala mengine ya kijamii ni chache na hupata wachangiaji wachache....... Wengi wana shobokea watu maarufu,,, yaani hata wakipost kaherufi kamoja utakuta comments kibao...

Mimi sijui facebook inafananaje.
Ya fb tuyaache fb labda uedit hapo uweke jf nitoe makoments.
Hata hivyo kwani mtu akikuuliza habari za maisha wakati upo ulaya unafikiri atakuomba nauli aje huko au??

Nakupenda comment yako.
 
mtoa mada ni limbukeni wa ulaya,ulaya ipi unayoiongelea wewe ujue siku hizi ulaya na manzese wala si mbali,najivunia kuishi Mwananyamala:washing:
 
sahivi ulaya kama mbagala. Eti eeh?

Mbagala mbali na mjini labda chang'ombe,zamani mtu ukisikia katoka ulaya yan unaona wivu siku hizi hata hutoi taarifa kama unarudi wanakukuta tu home
 
FB ya watoto
Hadi kikwete ndani ya facebook,lowasa,slaa ndani ya facebook,hata nyerere alikuwemo facebook,obama ndani ya facebook,duh hawa pia watoto ....inaonekana wote washamba hata facebook hamuijuiiii,

Pia ulaya musifananishe na mbagala kabisaa,,,,,,miaka mia tanzania haitofika kiwango cha maisha ya ulaya,bongo ndo kwanza munalia na umeme ikisha munasema mbagala ulayaaa
 
anaepewa sh 500 akala mihogo na anaepewa hela hiyo hiyo akanunua gazeti nani mtoto?
Anaepewa milion 1 na akanunua pamba na bia na anaepewa hela hiyo hiyo akaanzisha biashara nani mtoto?
Utoto hapa hatuongelei maumbo yao na umri. Tunaangalia akili zao na namna wanavyotumia hiyo fb. Watoto wamejaa kule.
Ulaya kama mbagala muda wowote unafika, pesa yako tu.
Nakutakia mabox mema.
 
Au sio??Naona hata mimi nitatafuta nauli then nitaenda ulaya
 
Back
Top Bottom