Watanzania ni wakati wa kuondokana na CCM la sivyo tutakuwa tumechelewa

Watanzania ni wakati wa kuondokana na CCM la sivyo tutakuwa tumechelewa

CCM Itaendelea kuongoza Taifa letu kwa miaka mingi Sana ijayo,CCM haina mbadala na Wala Hakuna mbadala wake kwa miaka yoyote ijayo,CCM ndio Tumaini la watanzania katika kuwaletea maendeleo,ndio chama kilichobeba Sera na ajenda zenye kugusa maisha ya watanzania,ndio chama kinachoaminika katika mioyo ya watanzania,ndio chama kinacho kuja na ilani inayobeba maahitaji ya watanzania yanayogusa Mahitaji na kiu Yao, Ni chama kilicho na mfumo imara wa kiuongozi wenye kuleta matumaini kwa watanzania,Ni chama kilicholeta maendeleo katika kila secta.
Hata marehemu Mobutu Seseseko aliyekuwa Rais wa Zaire aliwahi kuwambia Wananchi wa Zaire kwamba yeye Mobutu ni Rais wao wa maisha. Lakini siku ilipofika mitutu ya bunduki ilipoegeshwa ktk Kijiji cha jirani kabisa na nyumbani kwake Gbadolite, aliamua kukimbia nchi bila kupenda.
 
Kwa kweli muda umefika...,

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
conversations za weakness za kwenye makubaliano ya mkataba zimejadiliwa na kuskika sana na actually mijadala mingi hivi sasa kwenye media ni huo mkataba.

Can you please share atleast few advantages and disadvantages of DP world investments to Tanzanians, Ili kusudi tuone pamoja na mapungufu ya kimkataba yanayoelezwa kwa hasira sana yawezekana kuna faida lukuki pia
 
CCM wanajua kwamba watanzania ni waoga wa maandamano na ndiyo maana wanafanya watakavyo. Kama uchaguzi mkuu waliiba mchana kweupe watu kimyaa - sasa unategemea wapate wasiwasi gani tena wa kuitawala nchi watakavyo ndugu.
Kwa hatua ilipofikia CCM, ipo njia moja tu ambayo ipo ya kuweza kuitoa madarakani nayo ni mtutu wa bunduki.Je, watanzania mmeshajiandaa sawa sawa kuitoa kwa njia hiyo???
 
Tatizo Si kuondoka CCM ,,shida Ni nani ataongoza?

Zimwi likujualo halikuli likakwisha.
Kwa akili hizi, acha bandari iuzwe tu. Itafika kipindi wazungu wataanza kuishi mwezini sisi Afrika bado tunahangaika na kutengeneza kibatari na kukata kuni za kusongea ugali huku ukiimba nyimbo za CCM.
Utakuta huyu naye ni baba wa familia anayetegemewa. Hasara sana
Afrika ni bara giza
 
Tatizo Si kuondoka CCM ,,shida Ni nani ataongoza?

Zimwi likujualo halikuli likakwisha.
Hivi kiwango ilichofikia CCM sasa hivi unaweza kukilinganisha na chama gani hapa nchini?
Huo msemo wa "Zimwi" jaribu kutumia akili yako mara moja moja kuelewa maana ya misemo hii.
Hata wakoloni walikuwa wanasema hatufai kupewa uhuru maana hatuna uwezo wa kujitawala. Hivyo huu mtazamo wako hata wakoloni walikuwa nao. Kama CCM imeweza kutawala hadi leo, tena sehemu kubwa ni bila ridhaa ya wananchi, hakuna chama kitashindwa.
Natamani sana uliyemjibu hapa angekusoma na kukuelewa vizuri.

Halafu ni mtu mpenda mipasho huyu: Eti "zimwi likujualo..." Yeye anataka hilo zimwi liwale waTanzania hadi wapi?

Watu wa namna hii ndio wanaostahili lile jibu lako jingine la "kondoo". siyo waTanzania wengi ninaojua wanao uelewa wa kutosha.

Samia kaizika moja kwa moja CCM. Haiponi baada ya hapa
 
Kwa akili hizi, acha bandari iuzwe tu. Itafika kipindi wazungu wataanza kuishi mwezini sisi Afrika bado tunahangaika na kutengeneza kibatari na kukata kuni za kusongea ugali huku ukiimba nyimbo za CCM.
Utakuta huyu naye ni baba wa familia anayetegemewa. Hasara sana
Afrika ni bara giza
Mimi mkuu sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote,,

Lakini huwa naangalia Sana mwenendo wa vyama mbadala,,..

Bado hakuna chama kilicho serious tanzania chenye uwezo wa kutongoza Zaidi ya CCM..

Nimeona mifano mingi ya sehem ambazo chama pinzani wanaongoza lakini still Hakuna mabadiliko yeyote.,
Zaidi ya kuongeza matatizo.
 
Hii mada ya upinzania umeipata wapi tunazungumza kuhusu bandari

Bandari zetu haziuzwi kama wewe ni ccm mkauze mali zenu achana na bandari zetu.

Bandari lazima iwekezwe wewe piga domo humu mitandaoni yaa maandamano tu yaliwashinda mtayaweza ya Dp world
 
Katiba mbovu

Uchumi mbovu

Utendaji mbovu

Mikataba mibovu

Mipango miji mibovu

Mifumo ya haki mibovu

Uongozi na usimamizi mbovu

Haya yote ndio matunda ya CCM.

Watanzania huu ni wakati wa kuondokana na CCM la sivyo tutakuwa tumechelewa.
Hakika
 
kwa apa tulipofikia nchi ni bora iongozwe na chadema na muda ni sasa ilibidi chadema iingie madarakani 2015 kwasababu ccm ilikuwa imeshajifia akaja mwamba jiwe akarudisha uhai chama cha ccm, saizi tena naona kabisa ccm betry low soon mtambo unazima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom