Watanzania ni wanafiki hasa kuhusu Sakata la BSS

Kayumba ana talent haimaanishi kwamba bila bss usingemjua ..cha msingi Rita arudishe hela ya mshindi wa bss
 
Mimi bro Master J nimekupata kwa nguvu ya tano aisee...
 
Unasema Wafanyakazi wa TRA waendelee kuiba hela za Watanzania kwa kuwa wanafanya kazi kubwa ya kukusanya kodi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila shindano mshind lazima alipwe kulingana na makubaliano huenda hata io m50 pia haimtosh msanii
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani yeye huyo Madam hajanufaika na kuendesha hilo shindano, kwani umaarufu alio nao umetokana na nini?

Wewe ni sawa na umefuatwa na binti akilalamika kuwa Baba yake Mlezi amekuwa anambaka mara kwa mara, nawe ukaanza kumnanga Mlalamikaji kwamba hana shukurani kwa kuwa ametolewa kijijini kwenye dhiki, analishwa vizuri, ananunuliwa nguo, anasomeshwa hivyo amvumilie Baba yake Mlezi.

Ukifanya mazuri utapongezwa na ukifanya madudu utashukiwa tu hamna namna.
 
Lakini na wao kwanini wasituambie ukweli kwamba washindi hawajalipwa?.
Kweli nia yao nzuri ya kusaidia vipaji.
Lakini wasipowalipa tutaona ni matapeli tu.
KUMSAIDIA MTU ISIWE SABABU YA KUMNYANYASA.


"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
BSS ina wadhamini ambao wanacover cost zote za mashindano, inatoa zawadi kwa mshindi na inawalipa kina madam Ritha na majudge wenzie kwahiyo hoja ya kuwa wamefaidika kukaa hotelini na vitu kama hivyo haina mashiko. Yote hayo ni sehemu ya mashindano. Kama mashindano yasingekuwa na zawadi basi wafadhili wasingetoa fungu la zawadi.

Wasanii wanapopata platform, madam Ritha anapata content. Bila wasanii kusingekuwa na content, thus kusingekuwa na wadhamini(pesa). Alichokosea madam Ritha ni kula hata kile ambacho hakikuwa chake. Kwa ufupi ni kwamba anadhulumu washiriki na kujiongezea kwenye bakuli yake and it's not fair.
 
Asante sana kwa ujumbe makini kabisa, na hapa ndipo wanapoyumba wakati kiuhalisia mdhamini alitoa hadi zawadi ya mshindi ili akabidhiwe chake ila sasa Madam kasepa nayo...kama sio utapeli ni nini? mshindi apewe chake full stop.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ghalama wanayotumia kuirejesha no ngumu. Hivyo mambo ya lawama yapungue.
 
Wamlipe pesa yake 20m lkn hiyo 30m kulingana na mkataba wa shindano ni kwa ajili ya promotion. Haiwezekana kwa namna yoyote ile igeuke kuwa mali ya mshindi. Vigezo na masharti ya kuingia kwenye mashindano lazima vizingatiwe.
 
Acha kupoteza muda wako bure kulielewesha tahira mkuu
 
Wamlipe pesa yake 20m lkn hiyo 30m kulingana na mkataba wa shindano ni kwa ajili ya promotion. Haiwezekana kwa namna yoyote ile igeuke kuwa mali ya mshindi. Vigezo na masharti ya kuingia kwenye mashindano lazima vizingatiwe.
Sio kwamba kwa ajili ya promoshen tu na hiyo promoshen ionekane mzee,hv promotion ya 30m kweli jaman,daah madam utapeli umemuumbua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…