Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?

Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?

Mayalla huwa unajinasibu wewe umezaliwa,umelelewa na umekuwa katika familia ya vip3nyo kwa maana ya Baba na Mama yako ni Watu wa vitengo ila sijajua njaa hii umeitoa wapi kiasi Cha kujitoa ufahamu na utu wako kiasi hiki ok anyway siku hizi wasomi ndiyo wachumia tumbo Nchi hii acha niishie hapa🤮🤮
 
Tanzania viongozi wengi wameweka vipaumbele vya chama chake, mkoa wake anaotokea, dini yake, kabila lake na rafiki zake Mungu tupatie viongozi wanaopenda nchi yao kwanza
 
Mimi Sijasoma andiko, mmeishia kwenye Kichwa Cha Habari.


Itoshe tu kusema , Mh Pascal , Kwa Sasa wee ni Pro Chawa unayetumia Kalamu yako kuwatia watanzania kwenye Reli .


Bandari ni suala Dogo?. Suala Dogo ambalo ndio Linaloilisha Bajeti ya Nchi.

Hapana, hata Kama Mama amekurejeshea kile ulichokipoteza Kwa miaka Ile ya Hayati, uchawa umezidi, sio Bora ukae kimya?.



Ati unagusia Uhuru wa watu, Kwa sababumliwaaminisha watanzania kua JPM anabana uhuru wa watu ,Sasa Mama kaurejesha uhuru wa watu??? Kwamba watu wako huru kuongea ? ... WATANZANIA SIO WAJINGA, UHURU ULIKUWEPO.


Kuhusu Katiba Mpya, hili la Bandari pia Wataalam wa sheria , waweka wazi kua Lina chembechembe za Katiba, kwakua tumelipazia sauti , tutaendelea kulipazia sauti .



WATANZANIA TUENDELEE KUPAZA SAUTI ,TAASISI MBALIMBALI, VIONGOZI W DINI, ENDELEENI KUPAZA SAUTI, BANDARI IMEUZWA, TANZANIA IMEUZWA !!.
Kama ungelisoma bandiko lake lote kwa makini, ungegundua kuwa nae ni miongoni mwa wapaza sauti dhidi ya Bandari. Hofu yake kuu ni kuitwa tena kwenye Kamati ya Maadili.

Amezungumzia suala la Katiba. Kama tungekuwa na Katiba iliyo bora na isiyoyumbishwa hili la Bandari lisingekuwepo. Na kama lingetokea basi tungekuwa na uwezo wa kufanya Jambo fulani badala ya kupaza sauti pekee.

Ninachotaka kusema ni kwamba "Pascal" kwa sasa anaanza kurejea ule Upasko wake wa awali. Anasumbuliwa na jambo moja tu "HOFU".
 
Kenya Wana katiba nzuri, bado ufisadi na wizi umetamalaki...bandari ni jambo dogo? Unaumwa!
Punguza mihemko tumia akili mkuu, katiba iliyopo rais hashitakiwi na matokeo ya urais yakishatangazwa na tume aliyoiteua yeye mwenyewe hayapingwi mahakamani. Hebu amka usingizini kutoka kwenye hiyo ndoto ya bandari utoke nje.
 
Kuna mwanafalsafa mmoja anaitwa Yesu,katika kuishi kwake hapa duniani,aliwahi kusisitiza umuhimu wa kutilia maanani mambo madogo,kabla ya makubwa.
La bandari lizungumzwe lakini lisitutoe kwenye jambo kubwa zaidi la katiba mpya, Hiyo ndiyo hoja yangu mkuu.
 
Mkuu Pasco nimegundua kuwa kwenye jina lako ukitoa herufi "a" mbili za mwisho na ukaweka herufi e unakuwa Mayele....uwe na Jumapili njema🐒
 
Back
Top Bottom